MR BINGO
JF-Expert Member
- Feb 12, 2016
- 1,164
- 2,500
Habari wanajamvi
Katika kitabu chake cha "My life,My purpose"ndugu mkapa aliyepata kuwa rais wa Tanzania katika kipindi cha miaka 10(1995-2005) ameelezea katika sura ya 11 aliyoiita "reforms and yet more reforms" swala la vyeo mbalimbali vya serikali kufanywa kuwa vya kisiasa wakati vinampa mtu majukumu ambayo yanamhitaji awe na uwezo wa kupambanua vitu mbalimbali kupitia nafasi yake.
Raisi Mkapa katika hoja yake hiyo alitolea mfano wa cheo cha "district comissioner"(DC) ambacho tumeona siku hizi kikitumika kisiasa zaidi na kutoa nafasi kwa watu ambao hawako katika mfumo huo wa uongozi kiujumla na wamekuwa wakitolewa katika sekta mbalimbali kama sekta ya habari,sanaa,michezo.
Kupitia maneno ya Rais Mkapa anauliza "Je kumtoa mtu katika sekta tofauti kabisa na uongozi wa serikali na kumkabidhi wilaya aiongoze kupitia semina wanazopewa ndani ya wiki moja kuna ufanisi wowote?"
Nililete kwenu hili wanajamvi je ni suala lenye afya kumchukua mtu maarufu yeyote na kumpa ukuu wa wilaya ama ingekuwa ndo wakati sahihi wa kuwatumia wanataaluma wanaohitimu katika vyuo mbalimbali nchini katika fani za uongozi? Mfano Chuo cha Hombolo,Mipango,Udom,UDSM n.k