The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
M/KITI mpumbafu babu aliyekufaZidumu fikra za mwenyekiti.
Pengine katika africa yote Kenya wapo vizuri sana kwenye katiba na swala zima la uhuru wa vyombo hivyo.Kwa kadri nilivyofuatilia Mchakato wa kumng'oa Naibu Rais wa Kenya nimejifunza kwamba tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili kupata katiba inayolinda maslahi ya wananchi...
Mkuu 'Phylosopher', siyo "ubovu wa katiba" pekee kama unavyo eleza wewe.Kwa kadri nilivyofuatilia Mchakato wa kumng'oa Naibu Rais wa Kenya nimejifunza kwamba tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili kupata katiba inayolinda maslahi ya wananchi...
Na usifikiri uhuru huo umekuja kirahisi rahisi tu. Watu wamepoteza maisha kwa kazi hiyoPengine katika africa yote Kenya wapo vizuri sana kwenye katiba na swala zima la uhuru wa vyombo hivyo.
Bunge, mahakama na serikali yenyewe wapo huru kiukweli kweli sio maigizo.
Hata hapa kuna siku viongozi wa ccm watayakanyaga na utaona kitachotokea.Na usifikiri uhuru huo umekuja kirahisi rahisi tu. Watu wamepoteza maisha kwa kazi hiyo
Watu kufikishwa kwenya mahakama ya dunia usifikiri ni kazi ndogo hiyo.
Hapa kwetu tunaomba CCM ituruhusu!!!!
Kwa kadri nilivyofuatilia Mchakato wa kumng'oa Naibu Rais wa Kenya nimejifunza kwamba tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili kupata katiba inayolinda maslahi ya wananchi.
Yaani hapa kwetu ukiwa wewe ni Mbunge Rais hata Diwani ukikosana na mwenyekiti wako wa chama akakufukuza uanachama basi wananchi walioridhishwa na wewe wakakupigia kura kama ulivyo kama mwakilishi wao sahihi, hawana cha kufanya ili kukupata tena wewe kama mwakilishi wao.
Kwa Kenya haipo hivyo katiba inalinda sana uamuzi wa wananchi.
Na bado.Hata hapa kuna siku viongozi wa ccm watayakanyaga na utaona kitachotokea.
Viongozi wa wetu wanaweza kushitakiwa kama waalifu wa kibinadamu..
Sema hawa vyama vya upinzani navyo havipo serious sana rasivyo kwa kilichotokea hapo nyuma tekateka na mauaji ya viongozi wa upinzani kingetosha kabisa kuwanyoosha.
Haya yatafanyika vipi wakati kuna mtu mmoja yupo juu ya Katiba yenyewe.Utekelezaji ndio kazi kubwa, tunahitaji watu waambiwe kabisa kwa uwazi ukikutwa na rushwa mfano kuanzia mil 200 unakamatwa na kufungwa maisha, au ukikutwa na rushwa upande wa ardhi, yenye thamani kuanzia mil 500 au zaidi utafungwa maisha ili watu waogope kabisa kabisa
Hata huyo gachagua kang'olewa na chawa wa rutoMkuu 'Phylosopher', siyo "ubovu wa katiba" pekee kama unavyo eleza wewe.
Tatizo kubwa ni katika uelewa wa katiba yenyewe kwa wananchi na vikundi mbalimbali, ambao wapo tayari na kuhakikisha kuwa katiba hiyo inafanya kazi kama inavyo takiwa.
Hao wakenya, pamoja na kuwa na matatizo yao mengi mengine, kama ya ukabila, lakini sasa wameondokana na tabia mbovu za kuabudu mtu anapo kuwa kiongozi. Chawa hawana nguvu tena huko Kenya. Vyama vyao vya siasa navyo sasa hivi hakuna hata kimoja cheny mwonekano kama CCM ilio nao hapa kwetu.
Kwa hiyo raia wapo huru zaidi ya hapa tulivyo sisi.
Sisi bado tunatawaliwa na CCM kwa kutumia polisi. Kenya hilo sasa haliwezekani.
Kwanini Rais hajagiswa?Haya yatafanyika vipi wakati kuna mtu mmoja yupo juu ya Katiba yenyewe.
Sasa hivi Kenya hakuna mtu yeyote aliye juu ya katiba yao. Yeyote akiikiuka katiba hiyo inamwajibisha; kwa sababu taratibu zote za kufanya hivyio zipo wazi na taasisi zote zinazotakiwa kuhakikisha inakuwa hivyo zipo zinafanya kazi.
Kwani katiba unataka inyang'anye mashamba ya watu iwape wengine hata hapa kwetu katiba haigawanyi mashamba tunachosema ni kuwa katiba inatakiwa itoe haki kubwa sana kwa raia wa kawaida kuwawajibisha viongozi wao.... katiba nzuri kisiasa lakini iko sambamba na sera mbovu zinazomilikisha raslimali, kama ardhi, kwa wakubwa wachache ni KIINIMACHO TU!
... DON'T COMPARE OUR BONGO WITH SHITHOLE COUNTRIES!
Kwa hapa Tanzania ni ngumu kwa vyombo vya ulinzi na usalama kukataa chochote kutoka serikalini maana toka wanaingia humo wanapelekwa kichama zaidi screening inafanyika kama unaviashiria vya uhanaharakati hupati kitu ila ukiwa mwana ccm ni faster..Na bado.
Tayari dalili zote zinajionyesha jinsi CCM walivyo pania kunyang'anya uongozi katika chaguzi hizi zinazo fuata; na hakuna wa kuwazuia!
Kule Gabon, Omar Bongo alipo bainika anaiba uongozi, wanajeshi wakakataa upuuzi huo. Hapa kwetu hakuna mwenye uwezo wa kuwakatalia CCM lolote wanalotaka liwe. Maajabu yetu ni hayo.
Sahihi, Kenya wana katiba bora Africa kwa sasa, wasipovuragana watazidi kwenda mbali sana.Pengine katika africa yote Kenya wapo vizuri sana kwenye katiba na swala zima la uhuru wa vyombo hivyo.
Bunge, mahakama na serikali yenyewe wapo huru kiukweli kweli sio maigizo.