Kutoka Kenya: Mchakato wa wenzetu kumng'oa Naibu Rais unaumbua ubovu wa katiba yetu

Kuna maana gani ya kuwa na mgombea mwenza kama Rais akiamuwa wakati wowote anamtimua ? Hapa kuna katiba kweli?
 
Katiba yetu inatoa fursa kubwa sana kwa chama cha siasa kuwafanya vyovyote viongozi wetu
 

Hivi unaongea theoretically tu, unaijua Kenya wewe? Umefika? Wewe umekuwa kunguni kabisa, hopeless, unaongea online tu, real life in Kenya unaijua? Hiyo Katiba yao unayoisifia imewasaidia kuwapa maisha bora? Wewe nikikupeleka Kenya kuishi utarudi hata wiki humalizi, hali yao ni mbaya sana, kama hujui sbb wewe kazi yako kusoma online tu, Kenya unayosifia ndio namba moja kwa Rushwa kubwa kubwa sanaaa, in Africa, Kenya Corruption is within top 5..!!

Pia maisha halisi ya wananchi wao ni magumu mnoo, hiyo Katiba unaisifia unajua Kenya hata ardhi yote imechukuliwa na matajiri, maskini hawana ardhi, hiyo ndio Katiba unayoisifia?

Tatizo lako huna kabisa uhalisia wa nchi hata za jirani, meaning unasifia tu nchi za jirani kuona mambo yao mazuri kumbe hujawahi hata kufika na kujua maisha yao, kazi yako wewe ni kupinga pinga mambo bila kujua ukweli halisi, sbb uko Tanzania, nyumbani kwako, unaona almost kila kitu hakina maana, na hii ndio tabia mbaya sana, kwani vya nyumbani kwenu unadharau sana unaona vya watu vina maana, na ukifanya hiyo tabia yako kwenye maisha yako ya nyumbani kwako, utaharibikiwa kabisa, kwani huoni thamani ya vitu vyako au vya nyumbani kwako ila vya watu unaona vina thamani sana, hiyo ni akili ndogo sana..!!

Huna maana, nakupuuza sana
 
Kwa hiyo ulitaka rais aondolewe kwa makosa ya makamu wake kivipi?
Kama Deputy President kafanya makosa anatakiwa ashitakiwe mahakamani kwanza.
Nimekuuliza nini maana ya Madaraka ya Serikali kuwa mikononi mwa wananchi? Kiongozi aliyeingia madarakani kwa njia ya uchaguzi hawezi kuondolewa kihuni tu hivyo.

Katiba ya Kenya ni ya Kihuni
 
Kosa la kisiasa linaadhibiwa kisiasa na kosa la kisheria linaadhibiwa kisheria haina maana kwa kuwa ulichaguliwa na watu wengi ndo umisbihave alafu uachwe tu sio sahihi hata kidogo
 
Kosa la kisiasa linaadhibiwa kisiasa na kosa la kisheria linaadhibiwa kisheria haina maana kwa kuwa ulichaguliwa na watu wengi ndo umisbihave alafu uachwe tu sio sahihi hata kidogo
Katiba ni mambo ya kisheria siyo mambo ya kisiasa. Unataka kutuambia katiba ya kenya siyo ya kisheria? Na unathibitisha kuwa katiba ya kenya ni ya kitoto.

Adhabu ya kisiasa ni kwenye sanduku la kura siyo vinginevyo tofauti na hapo siyo siasa.
 
Kosa la kisiasa linaadhibiwa kisiasa na kosa la kisheria linaadhibiwa kisheria haina maana kwa kuwa ulichaguliwa na watu wengi ndo umisbihave alafu uachwe tu sio sahihi hata kidogo
Also kama amefanya makosa ya kisiasa, siyo kumtoa wakati yeye ni kiongozi halali aliyechaguliwa na wananchi. Wenye uhalali wa kumtoa ni wananchi. So wasubiri uchaguzi wao wa 2027 wananchi wataamua wao wenyewe.

Ndio makosa ya kisiasa yanaadhibiwa kwa namna hiyo. Na siyo kihuni huni wanavyofanya wakenya.

Jifunze ujue maana ya Republic usikimbilie tu kwenye demokrasia kabla ya kujua Republic ni nini.
 
Kosa la kisiasa linaadhibiwa kisiasa na kosa la kisheria linaadhibiwa kisheria haina maana kwa kuwa ulichaguliwa na watu wengi ndo umisbihave alafu uachwe tu sio sahihi hata kidogo
Mwisho na kwa umuhimu zaidi. Inatakiwa unapotaka kuwa na mgombea mwenza lazima utafute mtu ambaye mtaenda naye mpaka mwisho. Siyo unaungana na mtu ili wewe upate uraisi kwa sababu yupo na wafuasi wengi kisha unamgeuka baadae. Katiba ikiruhusu mianya kama hii nchi itakuwa na ombwe la uongozi, na itabidi nchi ianze kuongozwa na busara wala siyo katiba.

Unatakiwa kijana uchimbe zaidi na uache kuandika vitu emotionally.

Katiba ya Kenya ni kati ya katiba mbovu hazijawahi kutokea hapa duniani
 
Unadhani katiba yetu ingekuwa ina ruhusu tungeanza kumng'oa nani?
 
Kosa la kisiasa linaadhibiwa kisiasa na kosa la kisheria linaadhibiwa kisheria haina maana kwa kuwa ulichaguliwa na watu wengi ndo umisbihave alafu uachwe tu sio sahihi hata kidogo
Ni lazima nchi ya kenya ikubali kuwa na ustahimilivu wa kisiasa. Kutofautiana kisiasa ni afya ya nchi. Siyo wewe Rais ukitofautiana kisiasa na mwenzako unataka umfukuze mwenzako kazi. 🤣🤣🤣🤣

Rais wa kenya anatakiwa kuwa mstahimilivu. Na kama alimteua Rigathi Gachagua kuwa mgombea wake mwenza na kisha akamsaidia kupata kura kutoka kwa Wakikuyu kisha akamshinda Odinga, anatakiwa kuwa mstahimilivu na wamalize mambo yao kwa mazungumzo, maana wataendeleza na kukuza uhasama wa kikabila. Tunaomba uchaguzi wao wa 2027 yasije yakatokea yale ya Mungiki
 
Katiba inanitosheleza, kwa mfano mnataka kumtoa nani! Utaratibu wa kumtoa Rais upo wazi, sembuse DP na MP!
 
Cha ajabu Ruto alikuwa hamtii boss wake Kenyata, tena utovu wa nidhamu wa wazi wazi.

Kumbe Kenyata hakuelewa matumizi sahihi ya katiba, ndiyo maana walimwita 'Rais mlevi'!

Walikuwa wanadindiana wazi, mpaka nikawa namshangaa Ruto kiburi cha kumdindia Rais anakitoa wapi.

Na kwa upande wa Kenyata naye nikawa namshanga pia kushindwa kumuwajibisha Ruto.

Kumbe sasa Ruto ni mtaalamu wa kucheza na katiba kwa ajili ya kumnufaisha yeye na kuwadhibiti wenzake.

RigG alifuata nyayo zao za utawala uliopita, kasahau kuiga ku*** kwa tembo, ama bahati ya mwenziyo...dadeki.

Na kadhalilishwa hasa, maana hana chake tena, kutokana na sheria yao ya 'impechment' hata mafao ya ustaafu ya uzeeni hapati.
 
Kuna maana gani ya kuwa na mgombea mwenza kama Rais akiamuwa wakati wowote anamtimua ? Hapa kuna katiba kweli?
Si angalau huyo rais kahangaika kutafuta njia za kumwondoa kwa kutokwa jasho? Na bado haijulikani huyo rais mwenyewe atakuwa amepoteza kiasi gani kwa sakata hili. Utamlinganisha vipi huyo na mwingine ambaye yeye kwake "katiba ya nchi ni mkusanyiko wa makaratasi tu"!
 
Hivi unaongea theoretically tu, unaijua Kenya wewe
Wewe hunijui, utaanza vipi kunihoji?
Ndiyo maana watu wa aina yako nawachukulia kama takataka tu zilizojaa ndani ya nchi hii. Sijui mmeokotwa wapi nyinyi?

Kwa taarifa yako, ninaifahamu Kenya zaidi ya ushabiki wa kijinga unao uleta wewe hapa.

Sasa unataka tusemeje hapa; kwamba Tanzania inao mfumo mzuri wa uwajibikaji wa serikali yake kuishinda Kenya ilivyo kwa sasa, chini ya Katiba yao?
 
Huna maana, nakupuuza sana
'Actually', nilikuwa sijaangalia hata jina lako bandia humu JF ni nani? Nilikuwa nikijibu nikidhani ni katika wale majuha wa CCM ambao kutwa nzima wamejazana humu wakiandika takataka.
"Jay One', sidhani kuwa nilisha wahi kukusoma popote humu jukwaani.

Basi ni hivi:
Wewe ni hovyo zaidi hata zaidi ya yale matakataka mengine ambayo mara nyingi huwa sijisubui kujibu maandishi yao.

Kwa hiyo chukulia kuwa nimekosea kujibu chochote ulicho kuwa umebandika hapo nilipo ku'quote'.

Kenya ninaifahamu vizuri sana, na ukitaka kujua, angalia michango yangu kuhusu nchi hiyo humu humu JF. Historia yangu haijifichi, na sijawahi kuififu nchi hiyo hadi haya yanayo tokea sasa hivi. Wamepiga hatua nzuri, pamoja na kwamba bado wanayo matatizo mengi.
Sisi tumeporomoka zaidi, na nahofia sijui tutaishia wapi na kuporomoka huku.

Sina muda tena na wewe.
 
Ta
 
Pengine katika africa yote Kenya wapo vizuri sana kwenye katiba na swala zima la uhuru wa vyombo hivyo.
Bunge, mahakama na serikali yenyewe wapo huru kiukweli kweli sio maigizo.
Mkuu south Africa hivyo hivyo, huku kila mtu anaijua sheria hata mtoto mdogo, huku utakuta polisi anamuheshimu mtoto wa darasa la 5 la kibongo maana anajua sheria,

Bunge la huku lilimtoa zuma madarakani, kupitia mwanasheria mkuu,

Bongo hakuna sheria kuna undugu au usela katika sheria...

Waziri kusema asiyetaka kulipa kodi aende burundi, huyu alikuwa hayupo tena katika huo uwaziri kama angekuwa south Africa
 

Mkimuona The Phylosopher mwambieni namsubiri hapa nimtie adabu, maana anapiga kelele sana.
Lazima katiba itengeneze mazingira rahisi ya kumwajibisha kiongozi wao lakini pia lazima mihimuli ya mahakama ifanye kazi yake bila kuegemea upande wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…