Mkapa na mstaafu yeyote yule hawajawahi kuhitaji ruhusa ya Rais kutoka nje ya nchi. Kikwete alikua na bado anaruka kila siku kwenda nje. Ruhusa zilikuwa kwa watumishi wa serikali waliopo madarakani muda huo tena senior officers. Hata mtu wa kawaida mtaani hakuhitaji ruhusa ya rais.
Pili, kitabu kinasema JPM alimnyima pesa sio ruhusa, naona unabadilisha magoli. Ndo maana nimeuliza kwa akili zenu Mkapa hana hela au connection ya kwenda kutibiwa nje wakati hadi watu wa kawaida kabisa wanaenda nje?
Let's play dumb tuamini ana watoto 27 kweli, hao watoto wapo wapi au bado anaendelea kuwaficha? Hii mbona ni ishu ndogo tu watu kujulikana au hao watoto anawajua Kabendera tu ila mtaani hakuna mtu hata mmoja anawajua. Tunawajua watoto wa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK hadi wajukuu zao iwaje JPM watoto 27 wote wasijulikane?
Kuamini Mo Dewji alikua anapelekwa bank ku withdraw pesa ni uzwazwa wa kiwango cha juu. Rais mwenye mamlaka yote at his disposal hahitaji kuteka mtu ili apate hela zako. BOT, TRA, mahakama zote zipo chini yake ni call moja tu kuwaambia wafreeze accounts zako na wafanye wire transfer na watafanya hivyo in a heartbeat. Kuna kipindi accounts za watu zilikuwa frozen zaidi ya kipindi cha Magu? Kama aliweza kwa wengine nini kilimshinda kwa Mo hadi amteke? Nyie watu akili zenu sijui mmezikalia reasoning ndogo kabisa inawashinda.
Itoshe kusema Kabendera kawaona misukule na mlivyo mazwazwa mnaamini kila kitu bila reasoning yeyote ile.