Kumbe wewe ndio Ngongoseke? Mpunguze basi hizo ID.
Muulize huyo Al Alama Mohamed Said kuhusu mahusiano ya karume na hiyo EAMWS? Na unajua nani alianzisha hiyo EAMWS na kwa nini waswahili katika TANU waliipinga?
Unazungumzia ule msingi uliokuwa Chang'ombe, pesa mkazinywa na baadae mkadhulumiana wenyewe.
Au unazungumzia Chuo Kikuu chenu kinachotia fora mlichopewa baada ya Kafir mmoja kuchukua mali ya umma na kuwapa?
Amandla.....
Fundi Mchundo,
Mimi hupenda kuandika jambo kwa makini na bila mzaha kwa kuwa siko hapa
kufanya mchezo.
Nakusihi unichukulie hivyo ili tuwe na mjadala wa manufaa utakaoelimisha na
labda Allah akipenda kuinusuru nchi yetu.
Katika kitabu changu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism,'' bila hofu
nimezungumza mengi ambayo yalikuwa mwiko kusemwa.
La kwanza ni kuwa
Nyerere hakuasisi TANU na muaisisi wa chama kile ikiwa
tutamchukua mtu mmoja katika lile kundi la ile kamati ya ndani basi aliye aula
zaidi ni
Abdulwahid Kleist Sykes.
Hili lilizua kishindo kikubwa sana na bado vumbi lake halijatulia kote nipitapo hili
swali lazima litajitokeza.
La pili nililosema ni kuwa kumekuwa na njama ya kuivuruga historia ya uhuru
wa Tangayika.
La tatu na hii ni mwisho wa kitabu nilieleza kuwa Kanisa Katoliki na
Nyerere
kutoka uhuru upatikane wamekuwa katika vita dhidi ya Uislam Tanzania na
hapa ndipo unapoingia mgogoro wa EAMWS.
Haya ni maneno mazito na ukiyasema kama nilivyoyasema mie lazima uwe na
ushahidi madhubuti.
Kitabu changu kimejaa ushahidi wa haya.
Kila aliyejaaliwa kukisoma kitabu hiki alibaki kinywa wazi.
Ndiyo maana hadi leo kutoka kitabu kichapwe mwaka 1997 hajatokea mtu
yoyote kukipinga kwa kuandika huo unaosemekana ni ''ukweli.''
Palikuwa na ugomvi kati yangu na mchapaji (publisher) nilianza kitabu kwa
kuanza na maneno haya:''Bismillah Rahmani Rahim,'' akaniuiza kwa nini nataka
kuanza ''an academic work with religious undertones?''
Mhariri wa kitabu hiki alikuwa Prof. mmoja mwanamke wa Kiingereza.
Nilimjibu nikamwambia haya ninayosema nataka Allah ndiye awe shahidi yangu
wasije watu wakasema kuwa mimi ni muongo.
Ushauri wake kwangu ulikuwa kitabu kimejitosheleza hapana haja ya kufanya
hivyo.
Mimi niliamini kuwa eyote amuaminiye Mungu akiona nimemtanguliza katika kauli
yangu atajua kuwa sifanyi mchezo nisemayo ni kweli na kweli tupu.
Sasa kisa cha
Nyerere na EAMWS na
Karume umtajae ni kisa nakijua vyema
sana.
Katika mkasa huo wa EAMWS
Karume alifikia kumkufuru mola wake.
Karume yuko mbele ya Allah itoshe tu kuuombea dua Allah amsamehe madhambi
yake.
Ndiyo maana
Nyerere kafa hakutaka anasibishwe na
Abdu Sykes wala na mdogo
wake
Ally katika kuuunda TANU pamoja na wazalendo wengine takriban sasa wote
wako mbele ya haki.
Katika mazingira kama haya ndiyo maana historia ya TANU haimtaji popote
Sheikh
Hassan bin Amir wala
Sheikh SuleimanTakadir...
Ndiyo maana hadi leo hakuna historia ya uhuru ukitoa kitabu changu ambacho
''publishers'' wote nchini walikiogopa nikaenda kukichapa Uingereza.
Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Haroub Othman na
Dk. Kamata walikuja kunihoji
kuhusu
Nyerere kwa kuwa wao wanaandika maisha ya
Mwalimu Nyerere.
Tulifanya session tatu na mazungumzo yetu yanakaribia dakika 180.
Mimi niliwashauri kuwa waende kwa
Mama Maria Nyerere atawaeleza historia
ya TANU kama alivyoishuhudia kwa jicho lake kuanzia mwaka 1953.
Hiyo itajazilia mazungumzo yangu.
Nikawaambia kuwa kwa kuwa siku nyingi zimepita wanaweza kuamsha kumbukumbu
za
Mama Maria kwa kumkumbusha mashoga zake wawili
Bi Mwamvua bint Masha
(Mama Daisy) na
Mwalimu Sakina bint Arab kwani mengi walifanya pamoja wakati
wa kudai uhuru.
Fundi Mchundo,
EAMWS haikupingwa na Muislam yoyote na ushahidi upo.
Wakati wa mgogoro ule mwaka 1968 hapo TANU New Stret Baraza la Wazee wa
TANU lililokuwa chini ya Mwenyekiti wake
Mzee Iddi Tulio lilikuwa lishavunjwa na
Nyerere mwaka 1963 kwa kisingizio cha ''kuchanganya dini na siasa.''
Hawa ndiyo waliompeleka Nyerere Umoja wa Mataifa (UNO) mwaka 1955.
Hapakuwa na watu wa maana tena pale.
Yako mengi lakini haya niliokueleza nadhani yameshakupa picha unazungumzana
nani.
Napenda kumaliza kwa kukueleza kuwa jana nilitembelewa na mwanafunzi ambae
anafanya shahada ya uzamili na katika kukamilisha shahada yake anatakiwa aafanye
utafiti.
Alinihoji kuhusu Sheikh Hassan bin Amir.
Nilimwekea mhadhara mmoja niliotoa Zanzibar kuhusu
Sheikh Hassan bin Amir.
Ghafla nimemuona kijana kajiinamia machozi yanamlengalenga.