Katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira ulimwenguni, serikali na wadau mbalimabli husisitiza dhana ya kujiajiri. Jamii inaamini kuwa kujiajiri ndiyo tiba mbadala ya janga la ukosefu wa ajira. Ukisikiliza maoni ya vijana wengi kuhusu kujiajiri ni lazima utakumbana na changamoto ya ukosefu wa mitaji. Ndiyo, changamoto ni mtaji! Lakini mtaji si changamoto pekee iliyopo inayokwamisha vijana kujiajiri……
Ili kutekeleza dhamira yangu ya kujiajiri, nilianza kuweka akiba mara baada ya kuoa. Si unajua tena harusi zilivyo na mambo mengi, hivyo nililazimika kujichanga upya. Tulikubaliana kuweka akiba ya 200,000/- kila mwezi. Kama ilivyo kwa vijana wengi, kichwani mwangu tayari nilikuwa na wazo la biashara hivyo niliamini kilichobaki ni kutafuta mtaji. Nilitamani sana kufanya biashara ya kuuza nafaka.
Nikiwa bado sijakusanya mtaji wa kutosha, kazini kulitokea mgogoro ulionilazimu kujiudhuru. Kwangu mimi niliona ni fulsa ili nipate muda wa kutekeleza wazo langu la biashara. Ikumbukwe kuwa hapo awali sikuwahi kufanya biashara yeyote ile. Huu ulikuwa ni uthubutu wa pekee katika maisha yangu.
Baada ya kuacha kazi, mwezi huohuo nilisafiri kutoka Geita kwenda Mbeya kununua mahindi. Wakati huo familia yangu nilikwisha ihamisha kutoka kwenye nyumba ya kampuni kwenda kwenye nyumba ya kupanga. Nililipa kodi ya miezi sita (720,000/-) kutoka kwenye akiba niliyokuwa nimeiweka.
Nikiwa Mbeya, mambo yalikwenda kinyume na matarajio kwani haukuwa msimu wa mavuno. Bei ya mahindi ilikuwa ghali na upatikanaji wake ulikuwa mgumu. Dalali alinitafutia mzigo pamoja na usafiri wa kwenda Dar Es Salaam. Kwa sababu ya bei kuwa ghali na mtaji mdogo (4,000,000/-), niliweza kununua magunia ya mahindi 85 tu.
Nikiwa Manzese (Dar Es Salaam) dalali aliniuzia mzigo wangu, tukiwa kwa mteja ilionekana baadhi ya mahindi hayakuwa na ubora hivyo nililazimika kuyauza kwa bei ya chini na kupata hasara ya Tsh. 200,000/-. Pamoja na kupata hasara lakini nilirudi tena Mbeya kununua mzigo mwingine. Niliongeza umakini katika kuchagua mahindi yanayokidhi ubora wa soko. Nilipofika sokoni nilikuta kuna mahindi mapya kutoka Handeni (Tanga) hivyo soko la mahindi ya zamani liliendelea kushuka siku hadi siku.
Baada ya kupata hasara mara mbili mfululizo huku soko la mahindi likiyumba, niliamua kugeukia biashara ya maharage. Pale Mbeya ulikuwa ni msimu wa maharage na nilishafuatilia soko lake Tandika. Nilipanda gari kwenda kununua maharage. Kwa kuwa mtaji wangu ulikuwa umepungua sana, nilinunua magunia 19 tu kwa thamani ya 160,000/- kwa gunia. Bei ya maharage sokoni ilikuwa nzuri ila changamoto ni kwamba baadhi ya maharage hayakukauka vizuri hivyo nililazimika kuwalipa watu fedha ili wayaanike na kuyachambua vizuri. Kutokana na urefu wa safari na joto kali baadhi ya maharage yaliharibika na nililazimika kuyatupa.
Kwa kuwa maharage yalikuwa yanachukua muda mrefu sokoni, ilinilazimu kuchukua fedha kidogo iliyopatikana na kwenda Handeni kununua mahindi wakati huo nikisuburi dalali anitumie fedha inayopatikana kutokana na mauzo ya maharage yaliyobakia sokoni.
Nikiwa Handeni, madalali walinitafutia mzigo nikajikuta nimetumia kiasi chote cha fedha niliyokuwa nayo. Huko Tandika (sokoni), dalali alidai kuwa biashara siyo nzuri hivyo fedha hakuna. Hapo nilijikuta kwenye wakati mgumu kwani sikuwa na pesa mfukoni. Nililazimika kuomba hifadhi kwa watu japo kwa usiku huo tu bila kujali kwamba nilikuwa nimeshinda njaa. Tatizo halikuwa njaa tu kwani siku hiyo nilikuwa nimetembea umbali wa takribani kilomita 10 katika harakati za kufuatilia mzigo.
Asubuhi ninaamka baada ya usiku mrefu usio na matumaini ya kuifanikisha kesho mara nakutana na SMS kutoka kwa mke wangu akiomba fedha ya matumizi. Ikumbukwe kuwa sikuwa nimeonana na familia yangu kwa miezi 3 sasa na wakati naondoka tulikuwa tuna mtoto wetu wa kwanza mwenye mwezi mmoja. Nililazimika kukopa fedha pasipo matarajio ya kuilipa.
Pamoja na kupoteza biashara na ajira lakini kuna shule nilipata. Haya ni baadhi ya mambo niliyojifunza; mosi ni uthubutu wa kuweza kuanzisha biashara, pili ni kuweza kuishi nje ya mfumo rasmi wa ajira, tatu nilijifunza mnyororo wa thamani katika mazao ya nafaka na kubwa zaidi ni kuweza kuitazama fedha kwa jicho la kiujasiriamali, hii ilinijengea uwezo wa kuthamini fedha kwa nidhamu kuliko hapo awali. Hali kadhalika niligundua kuwa mtaji siyo takwa pekee ili vijana waweze kujiajiri. Ili majasiliamali kijana aweze kufanya vizuri anahitaji wazo la biashara, elimu ya biashara, mtaji, eneo sahihi la biashara, usimamizi madhubuti na kuwa mbunifu kulingana na mwenendo wa soko.
Wazo pekee lenye nguvu lililonijia ni kuanza upya, watu husema kuanza upya siyo ujinga! Niliamua kuuza mahindi yote ili nipate nauli pamoja na fedha za kujikimu. Nikiwa nyumbani na familia yangu nilianza kutuma maombi ya kazi katika kampuni mbalimbali na baada ya miezi mitatu ya machozi na damu nifanikiwa kupata kazi Dar es Salaam.
Huu ndiyo ulikuwa wakati pekee wa kudhihirisha kuwa nilishapitia mafunzo kwa vitendo na kufuzu katika maeneo ya nidhamu ya fedha na kutafuta mtaji ili kuendelea na safari ya kujiajiri. Niliweza kuishi kimkakati kwa kuweka 65% ya mshahara kama akiba. Hii si rahisi hata kidogo! Iko hivi, kama mshahara ni 500,000/- inabidi utenge 325,000/- kama akiba na kiasi kinachobaki (175,000/-) ni kwa ajili ya matumizi mengine. Hili haliwezekani isipokuwa umejikana kwelikweli! Lakini pia mkoa niliokuwa nafanyia kazi ulikuwa ni wa kimkakati kwani niliweza kufanya kazi ya kuajiriwa na baadae kujiajiri pasipo kuihamisha au kutengana na familia yangu.
Baada ya miezi 15 tayari nilikuwa nimepata fedha ya kutosha, mara moja nilianzisha biashara huku nikiendelea na ajira. Nilifungua biashara ya kuuza mchele kwa jumla na rejareja pale Tandika sokoni. Mke wangu ndiye alikuwa msimamizi wa biashara yetu na mimi nilikuwa nikifanya ufuatiliaji kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila kitu kipo sawa. Biashara iliendelea kustawi hadi kufikia hatua ya kuuza mpaka tani 30 za mchele kwa mwezi. Faida iliyopatikana kwa mwezi ilikuwa ni mara tatu zaidi ya mashahara wangu.
Kadri biashara ilivyozidi kukua ndiyo niliona umuhimu wa kuongeza usimamizi. Hii ilinilazimu kuacha kazi ya kuajiriwa ili nipate muda wa kutosha wa kusimamia biashara yetu na kupanua wigo wa masoko. Ninalenga kujenga ghala la nafaka na kusimika mashine za kisasa za kuongeza thamani zao la mpunga na mahindi jijini Mbeya. Sanjari na hilo, kwa upande wa masoko ninalenga kuzifikia taasisi za elimu kama vile vyuo na shule ili niweze kuuza nafaka kama mzabuni.
Picha: Mashine ya kukoboa na kusaga mahindi (Chanzo: afi_green)

Picha: Mashine ya kukoboa mpunga (Chanzo: maizewheatmill.org)
Upvote
18