M2WAWA2
JF-Expert Member
- Aug 15, 2014
- 3,285
- 5,598
Asante Mungu!!!
Ni miezi 18 tangu Mahakama kutengua ndoa iliyofungwa miaka 8 iliyopita.
Na huu ukawa mwanzo wa maisha mpya, maisha ya utulivu wa akili, amani moyoni na huru wa maamuzi.Na ukawa Mwisho wa maisha ya mateso ya Kihisia, kiakili, na kisaikolojia-hapa wanaume wengi wanapitia mateso ya hivi.
Maisha yale, yalikuwa ya ushindani, upinzani, kesi za uongo na vikao vya kila mara vya usuruhishi, bila kusahau zile dharau na jeuri na kiburi vyote hivi vikitakaswa na utetezi wa "Hata biblia inasema tuishi na wanawake kwa akili".
washauri wako wakuu kwenye kila kitu ni wale wana kikundi wenzio, wakifuatiwa na ndugu. Hawa waliweza kutoa ushauri na maamuzi makubwa ya ndoa yako bila hata ya kujua ya upande wa pili. bila Kujali una ongeza thamani gani kwenye familia.Walikuona wewe u mtakatifu na kusahau kwamba "kila matokeo, yana sababu zake", "kila mtu huvuna kile alicho panda". Walikushauri na ukatenda Ogopa sana wajumbe wa kwenye ndoa! Wakiharibu hutawanyika
Ninachotaka kusema ni hivi:
1. Ulitoa nafasi kwa wale watu kuwa washauri na wasemaji wakuu wa ndoa yako.Naam nao walikuwa nawe bega kwa bega, mpaka pale ndoa ilipo vunjika na sasa kila mtu kachukua njia yake na kuendelea na maisha yao na watoto wao. wengi walikushauri mambo ambayo hata wao hawawezi fanya kwenye ndoa zao!
2. Kwamba ule uzuri wa sura na maumbile na elimu na kazi nzuri na ile biashara yako, ilikufanya uonekane wewe ni wewe, ule wajibu na majikumu ya mke uliona ni takataka, hata majukumu ya unyumba hukuona kama ni muhimu kujitoa. Biblia ina sema tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala mwanzo 3:16
Ni kupitia drama zako na kipaji cha uongo ndoa ilifika tamati na nina amin uko uliko uhalisia wa maisha unauona sasa!
Je unajisikiaje kutoka kuwa mke wa mtu na kuwa mchepuko wa kitaa?, na umri ndio hivyo tena.
Wakati Mwanaume ni mbegu!, na mashamba ya kupanda ni mengi, mengine hayajatumika kabisa.
Funzo: Ulicho nacho kitunze!

- Nasikia ile nyumba umejenga kwa nguvu, nguvu ya uchi, nguvu ya kutembea na waume za majiran zako, ili kuniumiza!
- Nasikia hata yule aliyetelekeza mke wake kwa ajili yako naye amekutelekeza wewe pia. Malipo ni hapa hapa
- Nasikia hata yule kijana dereva unaye tembea naye, alikwenda kuoa mwanamke kwao, na kukuacha wewe mwenye sifa zote za uzuri na kipato! nasikia kijana huyu huyu anatembea na msichana wako wa kazi, na ndio mtoa taarifa zote hizi.
- Nasikia sasa unatafuta danga litakalokupa pesa za kutosha , milion milion tu, na uko mbioni kumkamata yule mwalimu wa chuo kikuu.
- Nasikia unatumia maji ya upako siku nikija kuona watoto nirudishe moyo nyuma!
- Nasikia hata kuroga umeroga sana ili turudiane, bila shaka ni baada ya kusikia makubwa niliyofanya kwa kipindi kifupi. Nawe umeshuhudia ustawi wangu wa kiuchumi, kijamii,na kiimani. Hata wale ulio kuwa unanilinganisha nao sasa hivi si kitu.