Kutoka kwa kufuta “orodha hasi” hadi “ushuru sifuri”, China yafungua mlango zaidi kwa dunia nzima

Kutoka kwa kufuta “orodha hasi” hadi “ushuru sifuri”, China yafungua mlango zaidi kwa dunia nzima

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Kuanzia tarehe mosi Desemba, China itasamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa zote za nchi zilizoko nyuma kimaendeleo zaidi duniani ambazo zimeanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Hapo awali, China imetekeleza orodha mpya hasi kwa uwekezaji wa kigeni katika sekta za utengenezaji kuanzia tarehe mosi Novemba. China imefungua mlango zaidi kwa dunia nzima.

Tarehe mosi Novemba, China imeanza kutekeleza rasmi toleo la 2024 la “Hatua Maalum za Usimamizi wa Uwekezaji wa Kigeni (Orodha Hasi)”. Toleo jipya la “Orodha Hasi” limeondoa kabisa vizuizi kwa uwekezaji wa kigeni katika sekta ya utengenezaji nchini China, ambapo baadaye kampuni za nchi za nje zitakuwa na hadhi sawa na kampuni za China katika kuwekeza sekta ya utengenezaji.

Hivi sasa, karibu nchi zote zinazoendelea zinaweka vikwazo dhidi ya uwekezaji wa kigeni katika sekta ya utengenezaji, na hata baadhi ya nchi zilizoendelea zina vikwazo hivyo. Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China, baada ya kuondoa vikwazo katika sekta ya utengenezaji, China pia itafungua mlango zaidi katika sekta za TEHEMA, mtandao, elimu, utamaduni, matibabu na nyinginezo, kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji wa kigeni, ili kutoa fursa kubwa zaidi ya kimaendeleo kwa dunia nzima.

Ikiwa kuondoa vikwazo dhidhi ya uwekezaji wa kigeni katika sekta ya utengenezaji hasa ni kufungua mlango kwa nchi zilizoendelea, kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa zote za nchi zilizoko nyuma kimaendeleo ni kwa ajili ya kunufaisha nchi zinazoendelea.

Kuanzia tarehe mosi Desemba mwaka huu, China itasamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa zote za nchi zilizoko nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China. China itakuwa nchi ya kwanza ya kufanya hivyo kati ya nchi zinazoendelea na nchi kubwa za kiuchumi. Hatua hii itasaidia nchi zilizoko nyuma kimaendeleo kupanua mauzo ya bidhaa kwa China kwa kiasi kikubwa.

Afrika ndilo bara lenye nchi nyingi zaidi zilizoko nyuma kimaendeleo duniani, na pia litakuwa mnufaika mkubwa zaidi wa China kusamehe ushuru wa forodha kwa nchi zlizoko nyuma kimaendeleo. Ili kuzisaidia nchi za Afrika kuongeza mauzo ya bidhaa zao kwa China, kuanzia mwaka 2005, China ilianza kusamehe ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi zilizoko nyuma kimaendeleo. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, China imesamehe ushuru wa forodha kwa asilimia 98 ya bidhaa za nchi 27 za Afrika. Hatua hizo zimetoa msukumo mkubwa kwa bidhaa za Afrika kuingia katika soko la China.

China imepiga hatua kubwa katika kufungua mlango kwa kiwango cha juu. Kama Rais Xi Jinping wa China alivyosema hivi karibuni kwenye mkutano usio rasmi wa 31 wa viongozi wa APEC, China inapenda nchi zote duniani kuendelea kunufaika na maendeleo ya uchumi wa China, na kufanya juhudi kwa pamoja ili kutimiza amani, maendeleo, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja duniani kote.
 
Back
Top Bottom