BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Anaandika mtanzania mwenzetu Twahir Abasi (kutoka Chuo kikuu cha Sayansi na teknolojia cha Huazhong, huko Wuhan, China).
______
Legacy ya watawala haipo sana kwenye ujenzi wa vitu labda vitu hivyo viwe ni VIKUBWA SANA, vya muhimu sana au vya kipekee sana. Kwa mfano Great wall ya China au Pyramid za Misri.
Lakini watawala wengi huacha legacy na kukubukwa kwa MAWAZO mazuri yanayoishi, yenye manufaa ENDELEVU na UJENZI wa MIFUMO mizuri yenye tija kwa kizazi kimoja hadi kingine katika kupambana na UMASIKINI, UJINGA, MARADHI na DHULUMA.
Thomas Jefferson wa Marekani hakumbukwi kwa visima vya maji alivyochimba, bali anakumbukwa kwa Tamko la Uhuru wa Marekani (Declaration of Independence).
Abraham Lincoln hakumbukwi kwa barabara alizojenga huko New York na Michigan, bali anakumbukwa kwa tamko la kishujaa la kuachia huru watumwa (Emancipation declaration) na Falsafa ya demokrasia (Philosophy of democracy).
Yeye ndiye aliyesema "democracy is a government of the people, by the people, for the people" definition ambayo vizazi na vizazi vimeikariri duniani pote. Mtoto wa form one kule Tunguu (Zbar) au Lutindi (Korogwe) ukimtajia Abraham Lincoln hatakumbuka barabara alizojenga huko Maryland, bali atakumbuka "government of the people, by the people, for the people." Hii ndiyo legacy.
Hata Mwalimu Nyerere hatumkumbuki kwa kujenga viwanda vya nguo vya MWATEX na URAFIKI, au kiwanda cha nyama cha TANGANYIKA PACKERS, bali tunamkumbuka kwa MAWAZO yanayoishi ya kudai UHURU, HAKI, UMOJA na HESHIMA ya MWAFRIKA.
Kizazi kijacho hakitakumbuka Stendi za mabasi, wala madaraja ya juu yaliyojengwa miaka 20 au 50 iliyopita, maana hata chenyewe kitajenga yao. Tena ikibidi hizi flyover za sasa watazivunjilia mbali ili wajenge nyingine zenye ubora zaidi, nyingi zaidi na za kisasa zaidi.
Kizazi kijacho kitaona legacy ya watawala wa sasa kikikuta nchi yenye HAKI na UHURU kama vichocheo vya MAENDELEO YA WATU. Kwa hiyo KATIBA bora ni msingi wa LEGACY imara, Sheria nzuri ni kuta za LEGACY imara, na MIPANGO thabiti ni Paa la Legacy Imara. Legacy sio madaraja au stand za mabasi.
Muhimu zaidi Legacy hailindwi, inajilinda. Legacy haitetewi, inajitetea yenyewe. Asomaye na afahamu.!