Kutoka kwa wahanga watarajiwa wa Covid-19

Kutoka kwa wahanga watarajiwa wa Covid-19

Huu ni waraka wa wazi kutoka kwetu tulio wahanga watarajiwa wa covid-19 kuja kwenu nyie tuliowapa mamlaka na sasa mnatutoa kafara wakati nyie mko pema.

Ninaandika waraka huu kwa kudra za mola nikiwa ningali hai na nikiwa na imani ya dhati kuwa marehemu wengi mliowatoa kafara wangeandika waraka kama huu laiti wangalipata nafasi au wangalijua au kuyahisi yaliyokuwa mbele yao muda kabla ya changamoto za kupumua kuwafika.

Hii ikizingatiwa hawakujua ni ndani ya muda mfupi kiasi gani wangalishindwa kupumua na kuiaga dunia kimzaha mzaha kama ilivyowatokea. Waswahili wanasema wenzio wakinyolewa zako tia maji.

Ni dhahiri kuwa mmeligeuza janga hili ambalo kwa hakika ni la taifa na dunia kuwa janga letu sisi binafsi katika familia zetu. Mmekuwa mkitumia nguvu zote zikiwamo tulizowapa, ili kuzuia taarifa zozote kuhusiana na athari na uwepo wa ugonjwa huu kwa nia ya kuficha ukweli kwa maslahi yenu.

Matokeo ya ukandamizwaji wa taarifa hizo yamekuwa hakuna ajuaye (isipokuwa nyie) maeneo yaliyo hatari kuhusiana na ugonjwa huu ni yapi, hali ya ugonjwa inakwenda vipi na nini mategemeo ya baadaye.

Pasi na taarifa watu wasiokuwa na majina makubwa wamekuwa wakiugua na wakidondoka kimya kimya kama ilivyo kwa wachuma majanga na kula na wakwao.

Mitaani watu wameaminishwa Corona imekwisha. Angalia jitihada hata za kunawa zilivyopoa. Nani wanavaa mabarakoa tena? Vipi nyomi kwenye mwendo kasi na hata kwenye ma school bus?

Kwani hata mashuleni pana maji tiririka na sabuni tena?

Hali inaendelea hivyo kana kwamba kila kitu sawa sawa kabisa hadi kimya kimya na mmoja mmoja na familia kwa familia wanapo kula janga lao peke yao na kivyao vyao.

Enyi tuliowapa mamlaka kutulinda likiwa ni moja ya wajibu wenu ulio mkubwa zaidi. Tumewakosea nini nyie, sisi tulio wazee na hata wenye magonjwa mengine kiasi cha kutuweka katika hatari kubwa na maisha yetu kiasi hiki?

Suala zima la kuhakikisha makundi yaliyo katika hatari zaidi yanalindwa kwa nini halina umuhimu wowote ule kwenu?

Siyo kuwa kwa sababu nyie taarifa kamili za msingi za uathirika na maeneo yaliyoathirika zaidi mnazo kwa uzuri zaidi, mmezikumbatia wenyewe na familia zenu mkitutoa sisi kafara?

Kwingine wanajali sisi tofauti yetu nini?

Sweden's prime minister orders an inquiry into the failure of the country's no-lockdown coronavirus strategy

Burundi’s President Ndayishimiye: new cabinet, new COVID strategy

Siyo ubinafsi wenu kweli?

Jana mbunge fulani, leo Profesa fulani, kesho fulani nk.

Haiwahusu kwa sababu kimya kimya kila familia inaathirika na janga lake kivyake vyake?
Unaandika kutoka kuzimu au peponi baada ya kufa
 
Kwa Tanzania Corona imefeli vibaya mno vimebaki vitisho tu kama vya huyu mleta maada. Pongezi nyingi kwa Rais wetu mwenye maono na NIMRI kwa kutupa fomula ya kutengeneza dawa ya kutibu na kujikinga na Corona yenye mchanganyiko wa tangawizi,vitunguu swaumu, vitunguu maji, limau na pilipili kichaa.
 
Itapofika kwenye familia yenu ndipo utajua kuwa ingalipo.

Kabla ya hapo wewe kama josepg1998 utajirejea mwenyewe kujipiga like.

Komaa hivyo hivyo.
 
Ajabu ni kwamba mpaka kifo cha Mzee Mkapa kinatokea na hadi siku ya kuagwa corona ilikuwa bado ipo na hata kifo chake wengine walisema ni corona,ajabu watu hao hao wakaenda kumpokea Lissu Airport nadhani hapo ndipo corona ilipoanza kupungua.View attachment 1688077
54339445_101.jpg
 
Lengo la kelele hizi ni lipi? Kama unaona wenzako wazembe jifungie ndani wewe
 
Lengo la kelele hizi ni lipi? Kama unaona wenzako wazembe jifungie ndani wewe

Nikijifungia ndani kodi tokea kwa wale wasiolipa hata ndururu uko pale pale?

Hivi mburula nyie kwanini mnadhani watu wengine ni majuha juha tu isipokuwa nyie?

Pana kipi wezeshi ambacho serikali dhalimu hii imekiweka in place kuwafanya wanaotaka kujifungia wafanye hivyo hata kama ni kwa gharama zao kiasi cha nyie kujinasibu na vihoja hoja uchwara kama hivi?

Kimsingi mnawaambia watu wajifungie ndani kama wanataka huku mkiwawekea mazingira ya kutokuweza kufanya hivyo hata kama ingekuwa uchaguzi ni wao.

Wauaji wakubwa nyie. Bure kabisa!
 
Nikijifungia ndani kodi iko pale pale tokea kwa wale wasiolipa hata ndururu iko pale pale?

Hivi mburula nyie kwanini mnadhani watu wengine ni majuha juha tu isipokuwa nyie?

Pana kipi wezeshi ambacho serikali dhalimu hii imekiweka in place kuwafanya wanaotaka kujifungia wafanye hivyo hata kama ni kwa gharama zao kiasi cha nyie kujinasibu na vihoja hoja uchwara kama hivi?

Kimsingi mnawaambia watu wajifunze ndani kama wanataka huku mkiwawekea mazingira ya kutokuweza kufanya hivyo hata kama ingekuwa uchaguzi ni wao.

Wauaji wakubwa. Bure kabisa!
Acha kulialia jifungie ndani na familia yako hujazuiwa
 
Acha kulialia jifungie ndani na familia yako hujazuiwa

Unanifunga mikono kisha unataka nikapigane?

Hadaeni wa dongobeshi.

Hatarini nani wamo inajulikana. Wewe umo au hujui kuwa umo?

Au wewe ni kutoka katika yale makabila yetu pendwa yasiyokuwa na kuthamini maisha ya wazee wao?
 
Unataka ukiugua mafua serkali ije nyumbani kwako? Fuata kanuni za afya

Wako wapi mburula kama huyu?

Waraka wa July 4, 2020 ungali unaishi leo.

Maalim Seif, Balozi Kijazi na wengi wengine waliotangulia na hata tuliopo ungali unatuhusu sana.

Itakuwa hivyo hadi pale tutakapo pumzishwa kwa amani na Corona Virus kwa hisani na udhalimu mkubwa tokea pale Lumumba.
 
Waraka huu ulituhusu wengi. Wengine walidhani hauwahusu kabisa.

Ninakazia: waraka huu kama ulivyo mtego wa panya ungali unatuhusu sana!
 
Unataka ukiugua mafua serkali ije nyumbani kwako? Fuata kanuni za afya

Pole pole, tutaelewana tu hata kama tutaita cardiac arrest, ajali ya boda boda au hata surua.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwa Tanzania Corona imefeli vibaya mno vimebaki vitisho tu kama vya huyu mleta maada. Pongezi nyingi kwa Rais wetu mwenye maono na NIMRI kwa kutupa fomula ya kutengeneza dawa ya kutibu na kujikinga na Corona yenye mchanganyiko wa tangawizi,vitunguu swaumu, vitunguu maji, limau na pilipili kichaa.
Hakika imefeli vibaya pongezi
 
Back
Top Bottom