Nakumbuka mwaka Jana baada ya uchaguzi wa CHADEMA, kundi la G55 lililohamia chaumma lilidai limehama kwa sababu ya CHADEMA kutokushiriki kwenye uchaguzi mkuu kupitia kauli mbiu ya no reform no election. Moja ya hoja za G55 ni kwamba CHADEMA haiwezi kumudu kujiendesha bila Ruzuku, hivyo chama kitakufa. Yeriko Nyerere akadai ya kwamba CHADEMA bila ruzuku hakitaweza kufanya operesheni au mikutano. Akadai viongozi waliokuja na wazo la kususia uchaguzi hawana hekima wanakiua chama.
Nakumbuka mwaka huu CHADEMA iliporudi kufanya siasa, mwandishi wa habari aitwaye Pascal Mayala kupitia moja ya online TVs , alidai CHADEMA haina pesa na wala viongozi waliopo hawana pesa . Akamtolea mfano Lissu na kudai Lissu hana pesa kama Mbowe na wala hana washirika wenye pesa. Na watu wengi wa aina yake walikuwa na huo msimamo ya kwamba CHADEMA haitasimama bila ruzuku.
Cha kushangaza muitikio wa wananchi ulivyoanza kuwa mkubwa kwenye mikutano na kukichangia chama, wakaibuka watu na kuanza kudai pesa inaliwa. Na wanaodai pesa zimeliwa hawataji kiwango cha pesa kilicholiwa au chanzo cha hiyo pesa iliyoliwa.
Swali la kujiuliza, je haya madai yangekuwepo kama mahudhurio ya mikutano ya CHADEMA yangehudhuriwa na watu wachache?. Hawa akina mchome na wenzake ndio wangekuwa wa kwanza kukitukana chama kwamba kimekosa ushawishi.
Hivyo basi, naweza kusema ya kwamba kubadilika kwa hizi semi kunaashiria ya kwamba CHADEMA inaelekea kuzuri. Inaonekana bila ruzuku CHADEMA bado inasimama imara na kuondoa hoja ya G55 ya kwamba bila ruzuku CHADEMA haiwezi kusimama. Na iwapo CHADEMA watamudu kusimamia mpaka 2030, basi watakuwa wamevunja rekodi ya kuwa chama kikuu cha upinzani bila ruzuku, wabunge na madiwani.