Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Good afternoon brothers and sisters 👋

Based on a true story!

Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivyo fuatana nami mpaka mwisho.

Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni mchaga wa Rombo Useri na mama ni mchaga wa Marangu Kirua. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa hapa jijini Arusha wa vitambaa maeneo ya Kilombero na mama yeye alikuwa mtumishi yaani mwalimu katika shule ya Arusha Secondary School kifupi Arusha sec. Tulikuwa tukiishi Sakina maeneo ya Silentini ndipo wazazi walipojenga.

Maisha yetu kwa kweli yalikuwa mazuri sana hapakuwahi kuwa na shida nyumbani upendo ulitawala na ndugu walitupenda sana na kila tukifunga shule basi bibi wa huko kijijini wa pande zote kila mmoja alikuwa anang'ang'ania tukakae kwake. Shule tulisoma nzuri mimi nakumbuka nilisoma st. Constantine iliyopo Arusha, shuleni tulienda kwa school bus na kurudi kwa school bus. Hata shuleni kulikuwa na tour za kwenda mbuga za wanyama mbali mbali na vivutio vingine nchini.

Kwa kweli shida sikuwahi kuzijua maana nyumbani tulikuwa hatuli maharage na dagaa maana mama alikuwa na vidonda vya tumbo. Nakumbuka hata nguo nlikuwa nafuliwa na dada wa kazi ambaye alikuwa mwenyeji wa Singida. Asubuhi ilikuwa lazima tule cornflex na maziwa. Nilikuwa mtoto wa geti kali hata kucheza ni ndani kwa ndani tu.

Mwaka 1995 nakumbuka nikiwa shule alikuja mjomba shule hivyo niliitwa ofisini kwa mwalimu mkuu na kuambiwa nirudi nyumbani. Tuliondoka na mjomba kwenye gari aina pegeout mpaka nyumbani ambapo kulikuwa na watu wengi tayari, sikujua nini kinaendelea kwa hiyo mimi na wadogo zangu tulikuwa na mjomba muda wote, ndipo baadae alipokuja baba mkubwa na kutuambia baba na mama hawapo tena! Mdogo wangu aliuliza wamesafiri watarudi lini? Alijibiwa hawatarudi tena na sasa ninyi ni jukumu letu.

Mimi sikuielewa na hakuna ambaye pia alielewa tukazidi kuhoji na tuliambiwa tu wameenda mbinguni kwa Mungu. Bado kwetu kuamini na kuelewa ilikuwa ngumu lakini tulienda kuzika Rombo na huko tulilia sana ila mdogo wetu wa mwisho Agness yeye wala hakulia ni kama alikuwa haelewi kinachoendelea. Mazishi yalikamilika hakuna aliyekuwa na wasiwasi sana ila ndio hivyo tulishabaki yatima bila kujijua.

Kilichobaki hapo ni mgawanyo wa mali na kwa mila zetu mimi ndio nilimikishwa mali zote za Mzee ikiwemo mashamba huko Rombo na nyumba hapo Sakina. Na huko Rombo pia mzee alijenga nyumba yake. Kule kwa mama Kirua pia napo mzee alimjengea mama mkwe wake nyumba.

Basi baba mkubwa ambaye alikuwa akiishi Dar kwa wakati huo alisema angetuchukua tukaishi kwake huko Dar na kwamba angetusomesha mpaka tutakapokuwa. Ile nyumba baba mkubwa alisema isiuzwe bali waishi ndugu zetu na yeye pia akiwa anakuja Arusha aweze kufikia huko.

Sikuwahi kujua kuhusu hati ya nyumba, mafao yoyote ya mama maana alikuwa mtumishi na wala kujua kama mzee alikuwa na hela benki au akiba yoyote. Mzee alikuwa na magari 3 pegeout ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kupeleka abiria Namanga, defender 110 ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kubeba abiria kutoka Mererani kaza moyo kupitia mbuguni mpaka Arusha mjini na staut nyeupe ambayo ndio alikuwa akiiendesha yeye katika shughuli zake ilikuwa ikimsaidia sana. Ila baba na mama walipata ajali ndani ya hiyo staut maeneo ya mto Nduruma na umauti kuwafika hapo hapo!

Pegeout alibaki nayo mjomba akiendelea na ruti za Namanga na ile defender 110 baba mkubwa aliipeleka kijijini ikafanye kazi ya kubeba maziwa na kuleta Moshi mjini. Statut ilibaki imekaa juu mawe na ilichinjwa ikauzwa.

Je, nini kitaendelea usikose kufuatilia mkasa huu wa maisha ya kweli unaosisimua na kutoa machozi.

SEHEMU YA PILI
SEHEMU YA TATU
SEHEMU YA NNE
SEHEMU YA TANO
SEHEMU YA SITA
SEHEMU YA SABA
SEHEMU YA NANE
SEHEMU YA TISA
SEHEMU YA KUMI
SEHEMU YA 11
SEHEMU YA 12
SEHEMU YA 13
 
Good afternoon brothers and sisters 👋

Based on a true story!
Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivo fuatana nami mpaka mwisho.

Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni ]
Pole mmepitia very hard situations ktk umri mdogo..
 
Sehemu ya 2
Tulienda Dar es Salaam na usafiri binafsi wa baba mkubwa na kufika, ambapo alikuwa akiishi Kurasini karibu kabisa na mizani. Maisha ndani ya jiji ya Dar hayakuwa mazuri sana maana joto lilikuwepo na mbu kwa wingi, haswa ukizingatia Arusha hali ya hewa haswa ukanda wa Sakina una baridi kwa kweli. Ndani ya wiki mbili 2 niliugua Malaria na kwa wakati huo dawa iliyokuwa ikitumika sana ni chloroquine. Ila dada zangu wao hawakuugua Malaria.

Tulikaa Dar na baba mkubwa akatutaftia shule huko Moshi ambayo ni ya bweni yaani kulala ili tusijihisi upweke pale nyumbani. Hivyo tulienda kusoma shule moja inaitwa Moshi Academy maeneo ya Ushirika Kibosho. ( Kwa watu wa Moshi watakubaliana nami ushirika na KCMC zote zipo ndani ya Kibosho).

Kwa maisha ya pale shule tulisoma na mimi nilifaulu ijapokuwa nilipata wakati mgumu sana haswa kwenye kubadili mtaala maana ukumbuke pale Arusha shule tulisoma kwa mfumo wa Cambridge na sio huu wa Tanzania. Nilimaliza darasa la 7 mwaka 1998 nikawaacha wadogo zangu shule ambao nao walilia sana kuwa hawawezi kusoma hapo kama sipo. Lakini walibaki kusoma hapo hapo. Mimi nakumbuka baada ya hapo baba mkubwa alinipeleka Tabora kwa shemeji yake ambaye alikuwa akikaa maeneo ya Bachu. Nilifika Tabora na nilifanyiwa mpango wa kujiunga na Tabora boys.

Nilianza kidato cha kwanza mwaka 1999 na mwaka huo ndio ulikuwa ni kama mwanzo wa mateso yangu. Baba mkubwa alikuwa amechukua mikopo hivyo mambo hayakuenda vizuri na duka lile la vitambaa pale Kilombero lilokuwa la mzee aliliuza pamoja na ile nyumba iliyokuwa halali yangu kwa kisingizio cha elimu yetu ni kipaumbele kumbe alitumia kulipa madeni yake. Hivyo mambo yalianza kwenda kombo mimi nikiwa busy na shule baba mkubwa mambo yalizidi kuyumba sana baada ya hapo mke wake ambaye alikuwa ni mwenyeji wa Tabora maeneo ya Isikizya alimwambia sisi ndio chanzo cha mikosi na mabalaa yanayomkumba hivyo atuache turudi kwa bibi kijijini.

Baba mkubwa alijaribu kukaza shingo akiwa na nia thabiti ya kutusaidia ila shinikizo la mwanamke ukizingatia na hali inazidi kudorora kiuchumi, rasmi mrija wa misaada ulikata kwangu na kwa wadogo zangu, mimi pale nilipokuwa nikikaa nilihama mwenyewe kwasababu ya manyanyaso, kipindi hiko maji Tabora yalikuwa ya shida hivyo unaeza tumwa kwenda kisimani unachota maji na baiskeli ukirudi unaambiwa uende upeleke mchele wa vitumbua mashineni hapo hujala chochote.

Ukirudi unaambiwa uwashe moto na kwenda kutafuta kuni za kupikia ukirudi unakuta wameshakula wamekuachia ugali kidogo na kisamvu cha karanga. Ukishakula hapo ndio basi tena mpaka kesho tena. Mi kiujumla hayo maisha yalinishinda yamanyanyaso haswa ukizingatia sikuyazoea kabisa, nikaomba kuondoka kurudi nyumbani, nilipandishwa basi la NBS na kurudi Dar. Dar napo nikapokelewa mzobe mzobe kwa kisingizio kwamba nimewatukana mama zangu wadogo na mkwe wa baba mkubwa hivyo nikafungashiwa virago na kupandishwa basi la Ngorika kurudi Moshi ambapo nitaenda kijijini Rombo kwa bibi.

Kweli nilifika mida ya 8 mchana njia panda ya Himo nikashushiwa hapo na mizigo yangu. Nilikaa sana nikimsubiri mtu wa kuja kunipokea ndipo kijana mmoja ndugu naye alipokuja na kurudi na mimi mlimani. Kule nilikutana na wadogo zangu na kwa kweli walifurahi sana kuniona nami pia nilifurahi sana kuwaona faraja zilirejea mioyoni yetu kwa muda huo.

Maisha ndani ya Rombo hayakuwa mazuri, bali yalikuwa ni ya shubiri kukata majani ya ng'ombe, kutafuta kuni, kusafisha hori la ng'ombe na fimbo kwa wingi sana yaani ukifanya kosa dogo ni fimbo haswa! Tulikosa mtetezi na ni kama tulitengwa na hilo lilikuwa linaonekana wazi wazi maana hata kuku akichinjwa sisi tutaishia kupewa vikwaru kwaru yaani miguu, kichwa au kibawa kile ambacho hakina nyama. Na hata wakipika nyama basi wengine wanafichiwa katikati ya wali na pale juu inawekwa moja au mbili kama geresha.

Mwaka 2000 niliamua kwenda Tarakea kwa shangazi alipoolewa nikakaa huko ili nijaribu kufungua ukurasa mpya wa masha yangu!

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
Back
Top Bottom