Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Sehemu ya 11
Nilikaa pale makuburini, na muda uliyoyoma sana nikaamua kusubiri muda uzidi kusonga maana niliona hapa ndio salama yangu. Kausingizi kalinipitia kidogo nikaja kuamshwa na wanga waliokuja kufanya yao makaburini, wao hawajiona ila mimi nimewaona. Nikaamka kuwafata ili kujua natokaje tokaje hapa, naona wao pia wananikimbia kwa hofu sijui walihisi mfu kafufuka au vp.
Nikaendelea kujibana na vituko viliendelea nikaona busara nisisumbue tena watu nkaja kamatwa hivo nilijiongeza kusubiri adhana ilie ili niende uelekeo huo huo. Macho nayo yalikuwa mazito ila adhana niliisikia nami nilifata uelekeo huo huo mpaka masjid pale nikajiziguzisha maeneo yale na kwakuwa mabomba yapo nilinawa. Mida ya sala ilivyoisha nikiwa na hang hang mitaa hiyo kwa kutosomeka nilisikia stori watu wanapiga. Yameuwawa wote, mengine yamekatwa, yule muarabu haingiliki wale wameyakanyaga.
Nikajua hapa kishanuka, kulipambazuka na stori kubwa town ilikuwa ni hiyo ukipita vijiweni au stendi watu wanasimuliana. Hapo sina hata ndururu (sina hela) nikawaza naondokaje huu mkoa wa kigoma. Nikaenda stendi kuzengea zengea nikamwona konda ananichangamkia, nikamuuliza unaenda wapi jomba? Akasema kasulu! Nikamwambia namimi naenda huko huko ila sina nauli msaada namimi ntapiga debe, akasema sawa kwanza fanya usafi ufagie ndani ya gari hilo utoe taka zote ukamwage. Nikafanya kama nilivoambiwa, gari lilikuwa kwenye kilo abiria walivyojaa likaondoka njiani mambo yalikuwa mengi sana ila nilifika kasulu na kuanza kufanya kazi za day worker sokoni. Nakulala ilikuwa ni kambi popote nilikaa kama wiki mbili kisha nikaondoka na kwenda kibondo maeneo twabagondozi ambako huko napenyewe ni vibarua vya mtaani tu. Huko nilibahatika kupata rafiki anaitwa ulokoze, huyu naye tulizoeana na katika kupiga soga za hapa na pale aliniambia mishe kuu kwa huku nikuteka magari au mabasi utaweza? Nikawaza nikaona hizo mishe ni ndogo ndogo sana nikamwambia hamna za hela ndefuu? Akasema labda wewe utupe sisi uzoefu wetu ni huku kibondo mpaka kasulu. Nikamuuliza silaha ipo? Akasema hana ila kuna mtu anayo nikitaka inapatikana. Nikamwambia basi hamna shida tuliachana na baada ya siku 3 alinifata nakuniambia wanaenda chimbo, yaani kutesa rizki za watu. Mi nikamwambia hizo za pesa ndogo achana nazo naendelea kusoma mazingira. Wao walienda na walifanikiwa kweli kutesa rizki. Alivyorudi nikamwambia anifanyie mpango wa silaha kuna chimbo naenda namimi kutesa rizki. Tulienda nae nikachukua silaha na kuondoka jioni nikampitia nikamwambie twende kuna hela za kutosha, tulipofika mitaa ya kanyamhela yeye alikuwa anaendesha pikipiki mimi nyuma amenipakia nilimpiga na kitako cha bunduki kwa nguvu pikipiki iliyumba tukaanguka wote chini, nikamsogeza pembeni ya barabara na kurudi kule kule kwake nikamvamia mkewe nakuwapora hela zote ambazo zilikuwa kama milioni 1 na chenchi kidogo. Mimi nikaamua sasa kukimbia na ile silaha niliitupa. Hapo ni usiku ukumbuke.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Vipi ile kazi ya muarabu hamna aliefanikiwa kutoroka zaidi yako? Kwa maana hio hamna mgao wowote uliopatikana kwa hio kazi? Maana umeelezea upande wa rav 4 vipi wale waliokuwa kwenye hilux double cabin nao wao waliuwawa wote?
 
It's the brain work to find fault, mistake,error, negative,danger etc so no wonder.
So Kama amedanganya si uachane naye ama akuhakikishie Kama Ni ukweli itaongeza namba yoyote kwa maisha yako,ama kipato chako??
Na je story una uhakika gani Kama Ni ya kutunga ama uwongo ama ukweli,tangiapo ikiwa ukweli,uwongo ama kutunga wewe itakusaidia Nini ama kupunguza nini. Is there anything you wanna trade with this story?
Jibu hoja yake, acha porojo...
 
Sehemu ya 6

Tulisubiri ishara bila mafanikio ikabidi turudi location yetu tukiwa tumefura hasira ile mbaya. Asubuhi palikucha na Mankah ndo alikuja wa kwanza na kuanza kulalama sana juu ya Warombo kuwa mama huruma na kwamba Adela amesema hatoshiriki na sisi kwenye huo mpango kwa kuwa ameahidiwa kuolewa na Ima pamoja na kujengewa nyumba, hivo tuliambilia hela ya nauli ya kuondokea Mererani. Wote tulitawanyika na kila mtu alishika 50 zake mchongo ulifeli.

Siku ya Jumamosi nikiwa mitaa ya Ngusero napuyanga huku na huko Palangyo alinifata na kuniambia twende Iliboru karibia na shule ya Iliboru ilipo kuna ramani tuliondoka na gari aina ya pegeout504 mpaka Iliboru. Kule tulimkuta Mroso na mimi na Palangyo na Fidee ambaye ndio alikuwa anaendesha hiyo pegeout.

Mchongo tuliusuka vizuri baada ya kupata taarifa kuna Wakenya wamekuja kununua maparachichi Tanzania, na wapo mizani pale back town Ngarenaro.

Tuliondoka na kwenda mpaka mitaa ya kona ya Eso ambapo tulipaki na kwenda kuzengea zengea ili kujua kunaingilika? Na dere naye alienda kuweka full tanka pamoja na mengine kwenye dumu kama dharura. Kweli fuso ile aina ya tandam ilikuwa imeshiba na walikuwa ni Wakenya ambao walikuwa wanasubiri jua lizame waanze safari ya kurudi kwao Kenya kupitia Namanga.

Sisi tuliamua kutangulia na gari ilikuwa ikipepea haswa mpaka tulipofikaOldonyosambu tukapaki pale huku tunachanja gomba na kushtua bangi ili akili zikae sawa tulipoteza kama nusu saa kisha tukaendelea mbele mpaka Longido, pale tulikuta road block tukasimamishwa kwaajili ya ukaguzi kwa kuwa tulikuwa tuna gomba na bangi tukaona tusipotezeane muda tukampooza askari kiasi cha pesa akatabasamu na kututakia kila la kheri.

Tulienda mpaka mbele kuna kamsitu pale tulisimama na kupaki gari barabarani kana kwamba limeharibika tulikaa kama masaa mawili kisha tukaliona gari la wakenya tandam likija lilikuwa kwa juu pale limeandikwa Michelin Naivasha. Gari iliwashwa na kusogezwa katikati ya barabara halafu likazimwa kama limeharibika tena huku tukijaribu kulisukuma.

Dereva alianza kupunguza mwendo mdogo mdogo upande huu mwingine gari za kutoka Namanga zilikuwa zinakuja tukaona hapa ndio penyewe tukalirudisha saiti yetu kuyapisha magari yanayotoka Namanga kwenda Arusha yapite. Palangyo alienda kwa Wakenya yule dereva kuomba msaada yule dereva aligoma ndipo Mroso akaona muda unazidi kupotea akazumguka upande wa abiria siti nyingine hizi akachomoa bunduki ambayo tuliikodi hapo hapo Arusha. Akapiga moja juu na Palangyo naye alichomoa ya kwake kumtisha dereva maana alikuwa ameshaanza kuingiza gia.

Dereva naye wa Pegeout hakuwa mzembe aliirudisha reverse gari mpaka ikaigonga ile tandam kwa mbele kidogo.

Tuliwashusha wote chini na hakukuwa na kupoteza muda kwani tuliwapiga na kuwataka watoe pesa, pesa ilikuwa kwenye mkoba nyuma ya siti maeneo ya cabin. Tuliibeba na kupiga risasi moja juu tena kisha tukatimua vumbi kurudi Longido, kufika Longido tulishika njia moja ya vumbi ya kuelekea Kiserian ili kukwepa polisi ambao wangetufata.

Gari ilikuwa inatembea haswa tulikuja kutoboa Lariboro na kuelekea mpaka Olmotoni kisha kuelekea Mateves ambapo tulipaki mitaa hiyo na kusikilizia kwanza. Tuliamua kutafta nyumba ya kulala wageni maalum kwaajili ya kuhesabu pesa hizo ambazo zilikuwa milioni 27 na chenchi zake. Mgawanyo ulikuwa 6*6*6*9.

Palangyo ndio alikuwa na mchongo hivo alikuwa anakula cha juu zaidi. Hakukuwa na ubishi sana katika mgawanyo kwani mapatano ya mwanzo ni kuwa mwenye ramani ndio mshika hela na ndiyo atagawa kutokana na ugumu wa kazi.

Je nini kitafata usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Aisee[emoji39]
 
Back
Top Bottom