Kutoka Mazda Atenza to Honda Fit Hybrid: Nini unapoteza na nini unagain?

Kutoka Mazda Atenza to Honda Fit Hybrid: Nini unapoteza na nini unagain?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
35,566
Reaction score
104,386
Wakuu.

Baada ya kukaa na Mazda Atenza kwa karibia 2 years, nikaona nibadirishe niende EV ndoto ikiwa Nissan Leaf ila ushuru ukanikata maini nikasema sio mbaya nikienda Hybrid, moja kwa moja nikaangukia Honda Fit Hybrid.
2017_Honda_Jazz_EX_Navi_i-VTEC_CVT_1.3_Front.jpg

Ni gari ndogo, isio na mambo mengi kwa mtu ambae ana misele mingi ya mjini, na michache ya highway.

Gharama za kununua
Gari niliagiza Japan kwa CIF ya takribani $4200 na Ushuru wa TRA wa Tsh Mil 7.5 hivi.

Muonekano wa Nje
Ni gari fupi, nikifananisha na magari mengi niliowahi endesha. Ina urefu na upana sawa na Toyota IST (2nd generation).
2017_Honda_Jazz_EX_Navi_i-VTEC_CVT_1.3_Rear.jpg

Muonekano wa Ndani
Kwa muonekano wa ndani mi nimeona ipo perfect kasoro touch buttons za AC na radio sijazipenda.
1280px-Honda_FIT_HYBRID・F_Comfort_Edition_(DAA-GP5)_interior.jpg

Ila nimeona ina nafasi sana kufananisha na magari mengine ya size hii au ata makubwa zaidi.

Engine & Transmission:
Inakuja na engine ya cc1500 na DCT transmission system ya 7-gears.

Performance
Ni hybrid, kwahiyo ina engine na hybrid battery. Kwa maana iyo ina drive mode tatu:
Eco mode
Sport Mode
Normal Mode


Kupitia Eco Mode, gari inajitahidi kutumia mafuta kidogo as possible. Na kuna muda engine inazima na kutumia battery kabisa (EV mode). Hii inatokea ukiwa na speed ndogo (below 40kph) katika barabara flat, au mteremko na inaweza kwenda hivi ata kwa 3+ km.

Fuel Consumption
Kama tulivyosema ina modes tatu, mimi tokea day 1 niliweka Eco mode. Na kwakua kwa hizi siku nimekua na misele ya mjini tu, ninachezea average ya 19 km/L.
PXL_20250331_155311697.jpg

Service
Kama ambavyo magari mengine yanategemea kudumu sana kutokana na service.

Inamfaa Nani?
Hii ni gari nzuri kwa mtu anaefanya kazi kwenye busy town kama Dar es Salaam au anaekaa nje kidogo aya mji (Mfano Chanika uku unafanya kazi Posta).

-Mazda ilikua Diesel, kwakua matumizi yangu makubwa mjini, ilikua inanitaka kila weekend niendeshe kwenda Bagamoyo kwa DPF (regeneration), Fit hamna kitu iko.

-Mazda ina fuel consumption nzuri ya 12km/L mjini ukiwa makini, ila 19km/L ya Fit ni zaidi.

-Highway Atenza nimewahi kua na average ya 22km/L ila Fit sijaitembeza highway bado ila inauwezo wa kuvuka 30km/L.

-Muonekano wa Atenza ni mzuri, ni kubwa na ndefu. Inekaa ki-premium. Fit imekaa ki-normal car.

-Technology ya Mazda ya i-Loop na i-Stop kusave mafuta ni nzuri sana ila haiwezi kuzidi EV Mode ya Fit.

-Atenza ilikua full leather seat, Fog Lights, Angel Eyes, LED light, DRL, ila Fit napata vimulika usiku tu (normal taa).

Kwa ufupi nategemea Fit itasave kwenye wese na service, huku nimepoteza premium look.

Shukrani.

Alternatives za Fit:
-Nissan Note e-Power
-Honda Fit Freed Hybrid
-Toyota Aqua & Prius
-Honda Insight
 
Aisee hongera sana najua ndoto zako za kuingia kwenye EV zipo karibu maana kwenye ishu ya mafuta hautaumiza kichwani kabisaa!!!
Ukiweka full tank unatoboa mbeya bila shida. Huu ndiyo muda sasa WA kupambana uwe na SUV Kwaajili ya safari na ukiwa mjini unatumia Hybrid yako kama kawaida
 
Hiyo Honda fit highway itatumia mafuta zaidi kuliko kwenye foleni. Tegemea chini ya 19km/l kwa highway sababu ya technology ya hybrid inakuja na fuel consumption kwenye foleni na speed ndogo
Tulia, nipo njiani naenda Morogoro. Hatuandikii mate.
 
Aisee hongera sana najua ndoto zako za kuingia kwenye EV zipo karibu maana kwenye ishu ya mafuta hautaumiza kichwani kabisaa!!!
Ukiweka full tank unatoboa mbeya bila shida. Huu ndiyo muda sasa WA kupambana uwe na SUV Kwaajili ya safari na ukiwa mjini unatumia Hybrid yako kama kawaida
Hapo umenena. Ukikaa fresh mtu unachukua magari 2.
 
Where is the joy in it ...kama hakuna ile harufu ya petrol na roaring sound ya Engine wakati wa kuchange gear. Nawasikitikia kizazi kitachohadithiwa kuwa tulishawahi tumia petrol na Diesel 😭😭 with their Silent lazy Ev Motor.
Huko tuendako sijui itakuaje na magari ya UMEME,
Barabarani hakuna mlio wa engine ni mwendo wa kimyakimya tu
 
Kama shida sauti, wameshakusikia. Utasikia hadi sauti ya gear shifting. Ldabda harufu ya wese ndio tatizo.

EV are faster, cleaner, efficiency, safer. EV are future 😁
Kaka leta mrejesho umeenda hatujakutuma moro bure😅
 
Back
Top Bottom