Akotia
JF-Expert Member
- Dec 16, 2016
- 528
- 1,241
Ohaa Wana jukwaa
Jf imeendelea kuwa mtandao muhimu ambao umekuwa kama mkondo wa pili wa habari kwa jamii ya Tanzania, na sasa unaonekana kama kama sehemu ya kuongelea masuala kedekede,Sababu ya uwezo wake wa kuchapisha habari haraka na kwa urahisi, na pia kwa kuwa jukwaa la user-generated content, inaruhusu watu kuchangia habari wajinga na werevu na maoni yao in real time.
Habari nyingi zinazopostiwa kwenye Twitter na Instagram, ambazo mara nyingi ni za upotoshaji, zimekuwa zikichapishwa pia kwenye Jamiiforums. Uhaba wa credible, passionate and open minded moderators husababisha inaruhusu watu kuchapisha habari bila ya ukaguzi mkali, na hivyo kuruhusu habari potofu kusambaa kwa urahisi. Jf inakosa habari za kisayansi, intelligent , investigation,jiografia na masuala muhimu ya kijamii, JF imekuwa ikijikita zaidi katika mjadala wa mambo madogo ya jamii, badala ya kuzingatia masuala makubwa ya kijamii ambayo jamii inaweza kuyataka.
Jamiiforums imegeuka zaidi kuwa jukwaa la malumbano na majibizano ya mambo madogo yakidini,ukabila na utamaduni badala ya masuala ya muhimu kama uchumi,viwanda na uzalishaji mdogo mdogo. Matokeo ya utandawazi na mabadiliko katika utamaduni wa mawasiliano ambapo watu wanapendelea kuzungumzia mambo ya kila siku kuliko masuala ya msingi ya kijamii.
Kwa hivyo, Jamiiforums inaweza kuonekana kama jukwaa ambalo linachangia katika upotoshaji wa habari na pia kuchangia katika kubadilisha mwelekeo wa mjadala wa kijamii kutoka masuala muhimu kuelekea mambo madogo ya kijamii, jambo ambalo linaweza kusababisha jamii kupotoshwa na athari za utandawazi. Kwaherini