Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA KWENYE SHAJARA YANGU 2 JUNE 1991
Huenda msomaji utakachosoma hapo chini ukaona hakina maana kwako.
Kwangu mimi hayo niliyoandika yamenipa jibu la swali lililokuwa likinitaabisha kwa muda mrefu.
Hapo chini nimeandika sentensi mbili katika diary yangu tarehe 2 June 1991:
"June 2, 1953 coronation of the Queen (Elizabeth the II).
17 April, 1953 AW Sykes v Nyerere TAA Election Arnautoglo Hall Dar es Salaam."
Nimeandika maneno haya miaka 33 iloyopita.
Wakati huu nilikuwa niko katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.
Hiyo sentensi ya pili inaeleza tarehe ya uchaguzi wa kumtafuta Rais wa TAA uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo kati ya Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere.
Bahati mbaya sana historia hii haikuwa inafahamika.
Nyerere hakupata kueleza kama aligombea nafasi ya urais wa TAA na Abdul Sykes mwaka wa 1953.
Hii ni historia muhimu sana kwa Nyerere mwenyewe na kwa TAA kwani baada ya uchaguzi huu mwaka uliofuatia ndipo TANU ikaundwa 1954.
Baada ya miaka mingi kupita ikawa kila ninaposoma kwenye kitabu changu taarifa hii naangalia chanzo cha taarifa hii sikioni.
Hili jambo likawa linanikera.
Nami sikumbuki wapi nimetoa taarifa hii.
Leo nikawa napitia shajara yangu ya mwaka 1991 ndipo nikakutana na ukurasa huu na sentensi hizo mbili na hapo hapo nikakumbuka kuwa ilikuwa kila ninapopata taarifa muhimu tarehe ya tukio nilikuwa naandika kwenye shajara yangu ya mwaka ule.
Taarifa hii nilikuwa nimesoma kwenye Nyaraka za Sykes pamoja na mambo mengine yanayohusu kutawazwa kwa Malkia Elizabeth.
Hii ndiyo sababu ya mimi kuandika hayo katika shajara yangu.
Picha ya kwanza ukurasa katika shajara, Abdul Sykes, Dossa Aziz, Julius Nyerere na Lawi Sijaona wakiwa Ukumbi wa Arnautoglo dhifa ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1956, Ukumbi wa Arnautoglo na shajara katika Maktaba.