Kutoka Tunduru: Wakulima wa Korosho wapokea zaidi ya Sh. Milioni 500

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Wakulima mjini Tunduru wakiri kipokea fedha zao kwenye akaunti zao baada ya kuuza korosho kwa jeshi.
Kiasi cha zaidi ya sh. milioni 500 zimeshapokelewa na wakulima bila usumbufu wowote.

Aidha vibega na wafanyabiashara ya usafirishaji wa korosho wameendelea kufanya kazi zao na kupata ujira wao bila matatizo yoyote.

Hongera JPM kwa uamuzi sahihi.

Sasa tuhamie kwenye FOREX ...!!

Nchi na wananchi lazima tukae sawa!

source:ITV NEWS
 
Hichi kigengo cha propaganda huwa kinalipwa na nani[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]

Jiwe kafeli wallahi
 

x = 500,000,000/3,300 = 151,515 = ~151 Tones

Nakukumbusha kuna Tani laki 221.

% ya walionunua = 151/221,000 = 0.068%

Zero Brains wa Lumumba wanapenda namba lakini hawajui hesabu.
 
Mafisadi kama wewe ndiyo mnalalamika kafeli kwa kuwa amewabana kwenye ufisadi wenu!! Badilikeni acha ufisadi mkuu la sivyo hutaonekana uraiani.
Hivi ndio huyu aliiba 1.5 trillion mkuu?
 
ungekuwa uzi wa kumsifia ndanda kosovo au mkimbizi wa ubelgiji ungeona unavyokimbiza!
 
x = 500,000,000/3,300 = 151,515 = ~151 Tones

Nakukumbusha kuna Tani laki 221.

% ya walionunua = 151/221,000 = 0.068%

Zero Brains wa Lumumba wanapenda namba lakini hawajui hesabu.
Zero brain wa ufipa mna kihoro kama bao la kwanza...hiyo ni Tunduru tu na sio Tunduru yote hayo ni mauzo ya siku hizi chache.
Hamna hoja ya kujifichia ...Magufuli anachoma vichaka vyote.
 
Haya maamuzi ya kununua korosho yatatugharimu mosi yatakutosesha fedha za kigeni.Pili yatatuongezea gharama kwakuwa ni jambo ambalo hatukuliwekea bajeti.
Nimalizie kwa kusema tunaposifu na kushangilia tuwe tunakumbuka na athari zilizoko mbele yetu baada kufanya maamuzi haya
 
million 500 kati ya billion 600...au billion 2 kati ya billion 600.. si mwaka utaisha hawajamaliza kununua?
gervase

 
TUNDURU AU Tunduma sijaelewa maana Tunduru unayosema. Hali mbaya sana ya Kibiashara ..
 
Mkuu Inawezakana Unachokiongea Ni Sahihi, Lakini Tunaomba Utuambie Ni Chama Gani Cha Msingi Kilichopokea Hiyo Hela??
Mana Malipo Yote Ya Wakulima Hulipwa Kulingana Na Chama Cha Msingi Kilichopokea Korosho....!!
 
Huku Tandahimba hadi leo tar 21 Nov hakuna mkulima yeyote aliyelipwa pesa. Imedhihirika kwamba, kwa utaratibu huu wa ulipaji, wakulima wataendelea kusotea pesa zao hadi mwezi Mei 2019. Hebu fikiria, mkulima mmoja tu wa Tandahimba anavuna korosho hadi tani 35 ambayo thamani yake ni zaidi ya mil. 100 hali ambayo inaakisi kwamba kama serikali itatoa hizo mil. 500 kila awamu basi ni wakulima watano tu watakuwa wananufaika kati ya wakulima zaidi ya 50,000. Msimu uliopita chama cha TANECU (Taxdahimba na Newala) kiliuza korosho zenye thamani ya Tsh. Bil 600, halafu leo hii Magufuli anatoa bil. 2 kwa vyama vya msingi 35 then wapuuzi wanashangilia. Kwa mtazamo wangu ni kheri wangeachiwa wahindi kununua korosho. Serikali itaumiza wakulima kwa kuwasotesha kwa miezi mingi bila malipo. Korosho zinahitaji mtaji wa zaidi ya bil. 800 halafu Magufuli na benki ya TADB wanatoa bil 2 kwa awamu, hivi itachukua miezi mingapi kulipa wakulima wa korosho katika mikoa yote ilimayo korosho ambao thamani ya korosho zao inafikia zaidi ya bil. 800? Magufuli kachemka kwenye suala hili. Anaua wakulima. Hadi sasa ni vilio tu wakulima wakisotea malipo yao. Hataweza hii biashara.
 
Sio kila muda upost kitu,tsh 500 million ni sawa na wamenunua tani 152 tu.Sasa sielewi unajaribu kuwaeleza nini watanzania juu ya hatma ya zaidi ya tani 200,000 za mavuno ya korosho.
 
Huku tunalima mtama mambo ya korosho hatujui tunayapanda kwa ajili ya kivuli
 
TUNDURU AU Tunduma sijaelewa maana Tunduru unayosema. Hali mbaya sana ya Kibiashara ..
Huna TV wewe?Hali ya kibiashara kwa wana Kangomba lazima iwe mbaya Serikali imeamua kuwalinda wakulima wake.
 
Sio kila muda upost kitu,tsh 500 million ni sawa na wamenunua tani 152 tu.Sasa sielewi unajaribu kuwaeleza nini watanzania juu ya hatma ya zaidi ya tani 200,000 za mavuno ya korosho.
Watanzania wenye uelewa wapo wengi ...hizi ni updates za zoezi la uuzaji na ununuzi wa korosho chini ya JWTZ.
Mlidhani Serikali inatania sasa things are happening.
Wivu unawaondolea fikra ila tutawaelimisha na wivu wenu huo huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…