Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

BRV tu zimewatoa jasho,leo kuwaweka watanzania milioni hamsini kwenye data base moja,yaani adresses zenyewe hazieleweki,wengi wanakaa kwenye huts huko,yaani miji yenyewe imejengwa kihohela,jamani jamani January acha kutudangaya
 
Naona wanaparuana wenyewe,Muhongo naye hapa kapigwa dongo live kuhusu gesi,kumbe Muhongo katudanganya.
 
Mapato ya Gesi bado?uongo mtupu kama utaweza kuwaweka watanzania kwenye database kwa nini tutashindwa kuchimba gas?uongo mtupu
 
Naona anampiga kijembe muhongo kama nchi hii gas haiwez kufanya kila kitu kwa nchi hii kwa sasa
 
Pamoja na kwamba uwezekano wa Januarym kuwa Rais kwa awamu hii ni mdogo, ameonyesha umakini, umahili mkubwa katika kuelezea sera zake akimbwaga Prof. Mwandosya ambaye alipotezea watu muda wao.
Hadi sasa CCM wameshapata candidate wawili wa tatu bado yuko kimya huko Mpanda na Januari akiwasindikiza.

Kijana wetu amejipanga akipata uzoefu wa kutosha anaweza kuwa Rais wa awamu ya sita. Atumie hii miaka mitano kujipanga na kuongeza uwezo.
KIla heri Rais Mtarajiwa wa Awamu ya sita
 
Gas hata baada ya miaka kumi from now hatutakuwa tumeanza kuitumia.. .
Atakayekwambia uchumi wa nchi utatokana gas huyo laghai
 
Hii speech imejaa uongo mtupu,January acha kududanganya kabisa,Yaani Tanzania iwe kama USA kwa miaka Mitano,jamani jamani acha kutudanganya

ndo maana nimesema anaongea ndoto...anapenda kuiga kila kitu toka kwa obama..
 
This is the CHOSEN ONE

hilo kubalini
Huyu ni rais wa baadae, sasa hivi atapigwa chini!
Ana ahadi nyingi kweli, ila ni kichwa anavyoonekana na kuongea kwa kujiamini. Sijawahi kumsikia kabla, amekuwa akinisumbua tu na vimeseji ktk simu.
 
huyu bwana nilisoma nae udsm, mjinga mjinga na mpenda sifa flani.

Salim analazimisha ustaa kazi ni kulamba nyeti watu wenye majina nae awe anajulikana na ubwabwa wake.
 
akipita huyu basi smartphone zetu tutaziweka ndani! tutafungwa wengi
 
Hii tabia ya viongozi wa CCM wasio na uadilifu wowote kujifananisha na Mwl Nyerere na Sokoine inakera sana.
 
Makamba kwa nafasi yako japo ungeweza hata kulirudisha shirika letu la simu TTCL mikononi kwa serikali, japo ungesimamia wizi wa makampuni ya simu kwa wateja, japo ungesimamia bei za kupiga simu na bei za kutuma na kupokea pesa kwenye makampuni haya zikawa sawa na hali halisi za maisha, kidogo ningeweka turufu yangu kwako, lakini wewe uko ndani ya system hebu tounyeshe kwa upande wako tu katika nafasi yako ya naibu waziri wa mawasiliano, je umefanya nini?
 
pigo lingine kwa UKAWA maana wao kiongozi na Mgombea Rais wa kudumu ni Slaa na ukimpinga tuu unafukuzwa kama panya!
 
Back
Top Bottom