Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Naona anakabidhiwa rungu. CCM kwa vituko siwawezi.
 
ukisoma kitabu chake kilichoandikwa na PD karugendo maswali yote hayo yamo na Majibu yake....kwa maana nyingine wauliza maswali wamepangwa
OK jamaa leo katupa sumup ya kitabu chake eeh?January hana lolote kwenye utekelezaji
 
January aandaa watu wa kuuliza maswali.Katika mkutano wa kutangaza nia ambao unaendelea mjini Dar es salaam ,katika ukumbi wa milimani city ,imeonekana wazi kuwa ndugu January Makamba ,ameandaa watu wa kuuliza maswali.Hali hiyo imejitokeza baada ya MC wa mkutano huo kutokuwa tayar kuchagua mtu yeyote aliyenyosha mkono mpaka amtafute kwa uhakika mtu aliyepangwa kuuliza swali.Hali hii inatokana na kwamba kijana huyu,ambaye amekuwa akibebwa sana na marafiki za baba yake ni kiraza wa uhakika ,na ambaye inasemekena alipata sifuri ktk mtihani wa form four
 
Reactions: PPM
January yuko serikalini na CCM kwanini wasifanye hayo au kuandika situation paper kwa Rais na chama chake ikiwa na analysis na mapendekezo mazuri na rahisi kutekelezeka kama anavyotaka tuamini. Au wanahujumu serikali na chama chao. Ebu nisaidie kuelewa mwenye uzi huu, HAMY-D!. Maana maelezo yake ni kama yuko upinzani akionyesha njia mbadala kwa utawala wa CCM.
 
Kijana mdogo umeshaanza kununua watu.. Eti hana kashfa!? Aliiba mradi wa Sugu wa maralia no more akaupeleka kwa ruge then wakagawana nusu kwa nusu fisadi mkubwa huyu.

ulikuwepo wakigawana nusu kwa nusu acha maneno ya vijiweni
 
kwangu mie wagombea walionyesha vision na ufumbuzi wa matatizo ya watanzania ni Makamba na Muhongo.
 
Kijana amejitahidi kuongea.....atleast ameonyesha nuwezo wa kujieleza, sio kama kina Muhongo waliokuwa wanajisifia tu sehem walizotembelea na kufanya kazi na kiwango chake cha elimu kama vile tulimuuliza
 
UKAWA wanaendelea kupata pigo kila mgombea wa CCM ni moto ....


£ndelea kujipa moyo ukifikiria huyo TeamNyweleNyeupe atakuletea maendeleo.

Sisi hatuna shida, ndio maana tupo kimya.. Tukiingia ni kwa kishindo.
 
Nampongeza hapo kwenye kujenga njia ya reli za usafiri wa ndani Dar,hapo kweli katoa idea nzuri tena sana.

..hawa wana-CCM wanatudanganya tu.

..huyu alikuwa mshauri wa karibu wa Raisi Kikwete.

..tena anadai yeye ndiye aliyekuwa akichukua notes za mikutano yote ya JK na watu mashuhuri kama George Bush, Bill Gates etc. Zaidi alikuwa akiandaa taarifa za ufuatiliaji wa mazungumzo kama hayo.

..sasa kwanini hakumshauri JK atekeleze walau robo ya hayo anayodai atakuja kutufanyia?

..hayo aliyoyasema yanafaa kutamkwa na mgombea ambaye siyo mwana-CCM.

NB:

..wengine wanadai watapambana na rushwa lakini miaka yote wako kwenye uongozi wamekuwa baridiiii huku ufisadi ukiendelea kila kona.

..halafu kupambana na rushwa si ni sawa na kupambana na CCM?

cc Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:
Watizedi bhana? ghafla topic humu imehamia kama Makamba na pia Obama hutumia teleprompter au la!!
Vichwa maji sana!
 
Nasema through experience kuwa hatotokea rais mpya toka ndani ya chama cha CCM. Si January pekee ambaye ni muongo kwa kutoa kauli mbiu finyu na ahadi kibao kabla ya kupata urais. Kikwete alikuja na kauli mbiu nzuri ambayo watanzania bila kufikiri walimpokea kwa mbinde na kumpamba kila kona ya nchi. Miaka kumi baadaye ndani ya utawala wake, nchi na wananchi wake bado masikini vile vile na ile kauli mbiu yake mashuhuri ya "Ari mpya, nguvu mpya....maisha bora kwa kila Mtanzania," imefikia wapi? Hawa wote waliotangaza nia hawana jipya endapo wako ndani ya CCM na wamekulia humo, kwani hata wakiwa na mawazo mazuri ya kuendeleza nchi kama Kikwete before, hawatafanya chochote cha maana kwa sababu watafuata mfumo uliopo ndani ya chama chao, hivyo kuichagua tena CCM ni sawa na kujipiga kitanzi kwa miaka mingine ijayo ya mateso. Ni takriban miaka 54 sasa chini ya utawala wa TANU/CCM na hakuna cha maana walichokifanya nchi bado ipo majaribioni na viongozi wanaiba tu mali za nchi na kuwachekea waharifu huku wenzetu ambao hawana mali ghafi kama sie wanapiga hatua na kutuacha mbali. To hell with CCM na viongozi wake.
 
mwislam kapewa bible...hawa wamasai hawako teamlowasa?
 
Watizedi bhana? ghafla topic humu imehamia kama Makamba na pia Obama hutumia teleprompter au la!!
Vichwa maji sana!

Kama Januari kaisoma hotuba kwenye prompter si vyema kudanganya watu kuwa hakuisoma hiyo hotuba popote pale, na kwamba ilikuwa ipo kichwani.

Huo ni uongo.

Sasa swali ni je, ni kweli alikuwa anasoma kwenye prompter au la?

Hakuna mwenye jibu la uhakika mpaka hivi sasa.
 
Nimesikiliza mambo machache aliyoongea, naye anawakilisha idadi iliyo kubwa ya Watanzania ambao tumepoteza mwelekeo na hata hatujui tunachohitaji!
Nimemsikia akitoa shukurani kwa baadhi ya watu waliomsaidia, hapa angelimshukuru baba yake na JK kwa kumzawadia uwaziri na hivyo vyeo vingine. Nimeshangaa anapowashukuru wananchi wa Bumbuli, hebu tuweke sawa historia: kwani kuna mtu hata mmoja aliyempigia kura huyu kijana kuingia bungeni!?
 
Nakubaliana na wewe, ukiangalia kiundani hii ni project ya jumba kuu, just kuharibia wagombea walio serious. Hawa jamaa wanadhani hii jnchi ni ya kifalme na hawakubali yaishe. Watanzania wenzangu plaese pleae say No to third Term of Fourth regime. No to uncle. No to project ya Jumba kuu Aka Membe. Princekubali yaishe, tulia Chalinze usije kujiharibia zaidi
 
Emma anasoma mahali mwangalie vizuri..kuna telemproter kwa mbele yake...ila duuu anaongea ndoto tupu..sijui meli,kila wila kujrnga chuo,mara satelite....

Hahahaha...nyimbo ya prof jizzo
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe, ukiangalia kiundani hii ni project ya jumba kuu, just kuharibia wagombea walio serious. Hawa jamaa wanadhani hii jnchi ni ya kifalme na hawakubali yaishe. Watanzania wenzangu plaese pleae say No to third Term of Fourth regime. No to uncle. No to project ya Jumba kuu Aka Membe. Prince kubali yaishe, tulia Chalinze usije kujiharibia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…