Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

January atatoa milioni hamsini kwa kila kijiji,jamani Tanzania tuna vijiji vingapi?January atawezesha vyuo viweze kukopesha wanafunzi,Huku akisema kunawili kwa nchi hakutegemei kodi za mapato,bali kunategemea kuwainua watanzania.sasa hizo pesa za kugawa kama pipi atattoa wapi kama hatokusanya kodi ipasavyo?

kasema kunawiri kwa nchi hakutegemei kodi za mapato pekee
 
"tunasema ualimu ni wito lakini haztutaki ualimu uwe adhabu,maana kama saikolojia ya mwalimu haijatulia tusitegemee elimu bora" ndg January Makamba......nikiwa kama mwl wa saikolojia yaani umenigusa kijana apo tuu
 
Aibu....aibu,aibu mpaka mwisho. Hivi ccm hawana akili kiasi hiki? Hivi hawajui....... Hapana huu ujinga mwisho October. Mungu wape ujasili Wa kuachia nchi kwa ustarabu vinginevyo nchi ilipofika imevimba itapasuka kwenye kutangaza matokeo.

hawana akili wapo mirembe au ????
CCM ndo chama mama kwahy hata babu zetu hawakuwa na akili????
watanzania tupunguze uvivu wa kuwapongeza watu wakifanya vyema
 
I am now officially Team January makamba kwa maneno machache ambayo ameongea leo....

Ndugu wanaanchi wenzagu sentensi aliyosema jmakamba apo juu ina Maana sana kwa wagombea uraisi tanzania
 
We wakuja fani za watu hizi unafikiri siku hizi watu wanasoma makaratasi kama lowassa.

Haelewi mambo ya teknolojia huyo. Kama hujui unaweza kudhani hasomi mahali kumbe kuna li screen mbele huko anasoma. Siku moja nilimwona waziri wa fedha Afrika kusini anatoa "bajeti yake bila kusoma" nikashangaa sana. kumbe alikuwa anasoma kwnye scriini ambayo huwezi kuiona km unaangalia TV. In fact hakuna sababu za msingi za kukariri hotuba na ukienda kutoa hotuba kwa watu sirias bila kuwa na kitu kinachokuongoza utaonekana hauko serious. Yaani kwamba akariri ili kutudanganya kwamba yeye ni genious? Acheni ushamba!
 
Na hapo ndo alipomshinda wa mtama kajipanga vizuri hata uzushi haushtukiwi kabisa. Hafu wanapigana madongo wao kwa wao sijui ili iweje.

Mpaka hapa naanza kuona kama muhongo ana akili kuliko wote...yeye alisema kupigana madongo hakutawatoa watanzania kwenye umasikini!
 
January hizi pesa za haya yote uliyoyasema utatowa wapi?umesema utawezesha vyuo kukopesha wanafunzi how jamani?mana kwa sasa vyuo vinategemea ada ndo kama income zao?
Mkuu!, unakumbuka songi la ndio mzee!. Prof Jay anaweza kutangazwa nabii wa siasa!.
 
Kwa kweli huyu ni mgombea wa pili baada ya prof kuchambua mambo kwa kina viva january unanishawishi aisee
 
kasema kunawiri kwa nchi hakutegemei kodi za mapato pekee

Serikali isiyofanya biashara inapata wapi pesa zaidi ya kutoza kodi na ushuru? Yeye hizo fedha aseme atatoa wapi maana hazina ni ile ile sio akiingia yeye itajaa mapesa ya kuwapa wanafunzi na wanavijiji kirahisi rahisi wabongo rahisi sana kudanganyika.
 
Ingekuwa tunachagua kutokana na nani kaongea vizuri na point basi Makamba kawaacha wenzake mbalo sana!! Anaongea mazuri tatizo yuko ktk mfumo uliooza mizizi!
 
Warioba would be the only sensible choice for the Presidential candidacy.
 
We wakuja fani za watu hizi unafikiri siku hizi watu wanasoma makaratasi kama lowassa.
Hata wewe wa kuja tu umekuja mjini hauna hata miaka mitano mjini kutoka Morogoro halafu unatakiwa uniheshimu mimi shemeji yako kauzu wewe.
 
Back
Top Bottom