Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kila mtanzania ana bima ya afya,pesa mtatoa wapi?milioni hamsini kwa kila kijiji,wavuvi kununuliwa boti na majokofu,kila wilaya kujengewa chuo cha ufundi,huyu anatudanganya
 
Mpaka hapa naanza kuona kama muhongo ana akili kuliko wote...yeye alisema kupigana madongo hakutawatoa watanzania kwenye umasikini!

Yani wengi kupigana madongo utafikiri ndo yanasaidia kupunguza umaskini nchi hii. Hawa watia nia sijui wakoje nao. Mhongo si anajielewa.
 
WanaJF,

View attachment 258214

View attachment 258215

KAULI MBIU YA JANUARI MAKAMBA: TANZANIA MPYA

-Ikiwa ni muendelezo wa watangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa ni zamu ya January Makamba kutangaza nia kutokea Mlimani City.

-January Makamba anaomba ridhaa ya chama kusimamishwa kuwa mgombea wa urais kufuatia wana CCM 15 kutangaza nia hiyo ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM.

-Hivi sasa kinachoendelea ni ushuhuda wa watu mbalimbali juu ya uongozi wa Januari Makamba.

-Mmoja wa wananchi wa jimbo la Bumbuli ametamka kuwa, "Januari ana kama Unyerere Unyerere hivi". Hii ana maanisha kuwa kijana ana ufuatiliaji wa hali ya juu na ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia watu.

-Januari ameanza kuongea na amejielekeza moja kwa moja kutanga nia yake ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM, pia amesema kesho kutwa ataenda kuchukua fomu ya urais kutoka kwenye ofisi za CCM, Dodoma.

JANUARI ATATOA HOTUBA HII BILA YA KUSOMA POPOTE. HOTUBA YOTE IPO KICHWANI.

- Januari anasisitiza kuwa Tanzania MPYA itajengwa na viongozi wenye fikra mpya.

- Januari ahaidi kuwa na mawaziri wasiozidi 18 tu katika baraza lake la mawaziri endapo chama chake kikimpa ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM.


-Januari Makamba anaorodhesha ajenda tano kuu atakazo simamia endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuunda serikali.

............Update............

....Januari ahaidi kuwa serikali yake itatoa mikopo maalumu kwa vijana watakaomaliza vyuo vikuu ambao watapata changamoto ya ajila ili na wao waweze kufungua makampuni yao ili waweze kujizalishia kipato.

....Pia amesema katika serikali yake atahakikisha sekta ya nyumba ina mchango wa zaidi ya 25%, wakati sasa hivi ni chini ya 4% ikimaanisha Watanzania wengi hawana makazi. Hivyo katika uongozi wake hilo la makazi atalipa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa.

....Uvuvi, serikali yake itaanzisha mifuko maaalumu ya kukopesha wavuvi ili waweze kununua vifaa vya uvuvi ili isaidie kuboresha vipato vya wavuvi na pia kukuza sekta hiyo kwa kasi.

....Serikali yangu itaongeza udahili wa walimu haswa kwa masomo ya sayansi. Pia ameahidi kutatua changamoto za walimu kama vile mishahara yao kuwa duni, kukosa posho na stahiki mbalimbali. Ahaidi serikali yake kutatua kero hizo kwa kukuza na kuboresha maslahi yao.

.... RUSHWA, amesema kuwa kulizungumza na kulipigia kelele tatizo la rushwa sio njia ya kulimaliza tatizo hilo.

....ARDHI, jinsi ya kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Serikali yake itabainisha kisheria maeneo ya kilimo, mifugo na makazi. Pia amesema wakulima na wafugaji watamiliki maeneo yao kisheria. Atatumia teknolojia mpya ya satellite kutekeleza hayo kupitia kituo maalumu kitachoundwa chini ya serikali yake. Lakini pia kituo hicho kitasaidia pia na mambo ya kiusalama.

....AFYA, kila Mtanzania lazima awe na bima ya afya, kila Mtanzania lazima apate huduma bora ya afya bila ya kujali kipato chake.
Jamaa yupo vizuri sana bt kamfumo ketu Kanawa favor dini ingine ile, wewe waweza kuwa Waziri kamili wa Tamisemi ijayo.
 
We wakuja fani za watu hizi unafikiri siku hizi watu wanasoma makaratasi kama lowassa.

Mkuu naomba nimsaidie ndugu yetu. Mtangaza nia anatumia "autocue" au "teleprompter". Kwa hiyo Mkuu Emma usibishe, kubali ueleweshwe.
 
Serikali isiyofanya biashara inapata wapi pesa zaidi ya kutoza kodi na ushuru? Yeye hizo fedha aseme atatoa wapi maana hazina ni ile ile sio akiingia yeye itajaa mapesa ya kuwapa wanafunzi na wanavijiji kirahisi rahisi wabongo rahisi sana kudanganyika.
Kwani Dr.Slaa anavyotoa ahadi uwa anasema pesa atatoa mfukoni kwake?
 
Tuchague kiongozi ambaye hatokuwa na deni lolote la kulipa...
 
ila wakifufua reli mambo yatakuwa safi sana kiuchumi
 
Yani wengi kupigana madongo utafikiri ndo yanasaidia kupunguza umaskini nchi hii. Hawa watia nia sijui wakoje nao. Mhongo si anajielewa.

M/kiti wao aliwaambia wasichafuane watashindwa kuombeana kura!..
 
January atatoa milioni hamsini kwa kila kijiji,jamani Tanzania tuna vijiji vingapi?January atawezesha vyuo viweze kukopesha wanafunzi,Huku akisema kunawili kwa nchi hakutegemei kodi za mapato,bali kunategemea kuwainua watanzania.sasa hizo pesa za kugawa kama pipi atattoa wapi kama hatokusanya kodi ipasavyo?
Vijiji elfu 12 hivi
 
Kwa ahadi hiz tanzania itakuwa juu kuliko hata marekani
 
Hata wewe wa kuja tu umekuja mjini hauna hata miaka mitano mjini kutoka Morogoro halafu unatakiwa uniheshimu mimi shemeji yako kauzu wewe.

Hahahahahah leo nimekuwa sio mkinga tena? Unganisha unganisha kuna siku utapatia..
 
Nipo namsikiliza mgombea uraisi January Makamba kupitia CCM na nimejifunza kitu kimoja, mipango mingi anaowaambia vijana wenzake HAITEKELEZEKI. Kama kujenga chuo cha ufundi kila wilaya na kukopesha million 50 kila kijiji kudeal na umemployment. Sidhani kama hili ni suala realistic kwa kutokomeza unemployment, mabilion ya kikwete yalienda wapi? Na je Veta mbona zipo!! turudi nyuma kidogo..unmeployment imekuwa caused na nini?
1. Mfumo wa elimu ( quality ya eduation imeshuka sana.)
2.viwanda makampuni mengi kuwepo miji mikuu 5. basi je watu kutoka mikoa yote Tanzania husafiri kuja mikoa hiii (miji) kutafuta kazi hii inaitwa push n pull factor (kwa waliosoma GS ) na kwanini vwanda makampuni yako miji hii 5? kwasababu miji hii ina easy access to port, miji hii ina maji, miji hii ina umeme wa kutosha miji hii ina infrastructure. Je? Kusolve unemployment kwa kugawa mikopo ni halisia? sio halisi..kusolve unemploment ni kutengeneza ajira. Na tutafanya hivi kwa kusolve tatizo la viwanda makampuni kusambaa Tanzania nzima kwa kutengeneza barabara. kurudisha reli, kuwepo kwa maji na umeme na kuwaconvince viwanda watapakaeee Tanzania nzima au kwenye eneo linalotoka raw materials ili watu wa mikoani wapate fursa ya kufaidika na ajira na bidhaaa za viwanda hii, na pia kodi ipunguzwe kwa viwanda hiv ili bidhaa zao zishandane na bidhaa za nje ziweze kununuliwa zaidi na watanzania kufaidi zaidi. Jamani mbona simwelewi kijana menzangu jamaniii....Nyie mnamwonaje Bandugu
 
Kikwete kaiharibu ikulu SAA hiizi Kila MTU anazani anapawezapalee so kwamba sioni January hapawezi ila January ungesubili kudogo vitu anavyo viongelea kama viturahisi na wana Ccm wanashangilia enyi watanzania vitu visiwe vinaingia kichwan kidogo kidogo ila do go huyu mnjanja atamsumbua low as a anausha wishiii Kwa mbaliiiiiii n
 
Back
Top Bottom