Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Kutoka Ukumbi wa Mlimani City: Mkutano wa January Makamba Kutangaza nia ya Urais

Hebu mkuu yeyote mwenye CV ya January makamba , aitupie hapa...
 
Kadondosha NONDO, kwa sera kawa K.O wote waliozumgumza, alafu hasomi!
Tatizo letu siyo yupi anaweza kumeza nondo bila kusoma...tunataka mtu akataye simamia rasilimali za taifa hili ziweze kutusukuma katika maendeleo na kutunufaisha kila mmoja kwa namna yake.
 
Huyu anasoma sana vitabu,sasa kwa hii speech iliyojaa ndoto za alinacha basi Watanzania ndo tunaona anafaa hakuna lolote linalotekelezeka kwa caracter yake Makamba hana ubavu wa kutekeleza hayo
 
Kwa kuwa umesema the guy iz your favourate candidate haina shida, kwangu baado sana kwa kweli.
 
vyanzo vya mapato ya ziada ya january makamba bila kuzungumzia gesi huyu jamaa anafaa kuwa raisi
ImageUploadedByJamiiForums1433687810.154450.jpg
 
"sigombei nafasi hii kupambana na mtu bali kupambana na changamoto za watu"JM
 
Hotuba ya kusadikika,hakuna lolote la maana analozungumza.
 
Watangaza nia Wengi ni mawaziri lkn nao wanalalamika kama sie raia tu,hivi huo uwaziri ni kwa kazi gani?
 
Wanabodi,

Mengi yamesemwa na wagombea urais kupitia ccm wakati wakitangaza nia lakini jamani tuwe wakweli Bwana Mdogo Januari Makamba yupo juu. He has delivered a very sensational speech.

King Cobra.

Team ACT yote inamshobokea Januari
 
Teh Teh huyo ni mzee wa makontena ya kura na kuibiwa kura na usalama wa taifa ...
Mwambie pro-Chadema yeyote ajitokeze kutia nia kama ajafukuzwa kama panya ni marufuku kumpingana na fikra za Dr.Slaa na Mbowe.
 
Hawa watu kweli wanania ya dhati ya kuwaendeleza watanzania au wanania ya kuendeleza matumbo yao na ya familia zao?.
 
Huyu Makamba anatakiwa awe kitengo cha mipango na kutoa ushauri kwa taasisi ya Rais. Ni mzima sana katika kupanga ila kwenye utekelezaji anahitajika kiongozi makini na mkali kwa wakati tulionao. Amejitahidi kwa kutaja maeneo yote muhimu yanayogusa wanajamii
 
Mwambie pro-Chadema yeyote ajitokeze kutia nia kama ajafukuzwa kama panya ni marufuku kumpingana na fikra za Dr.Slaa na Mbowe.

Ritz unapanic nini? Pata supu ya pweza ujiandae ka Magharib
 
Last edited by a moderator:
KAULI MBIU YA JANUARI MAKAMBA: TANZANIA MPYA

-Ikiwa ni muendelezo wa watangaza nia kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa ni zamu ya January Makamba kutangaza nia kutokea Mlimani City.

-January Makamba anaomba ridhaa ya chama kusimamishwa kuwa mgombea wa urais kufuatia wana CCM 15 kutangaza nia hiyo ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM.

-Hivi sasa kinachoendelea ni ushuhuda wa watu mbalimbali juu ya uongozi wa Januari Makamba.

-Mmoja wa wananchi wa jimbo la Bumbuli ametamka kuwa, "Januari ana kama Unyerere Unyerere hivi". Hii ana maanisha kuwa kijana ana ufuatiliaji wa hali ya juu na ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia watu.

-Januari ameanza kuongea na amejielekeza moja kwa moja kutanga nia yake ya kuwania nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM, pia amesema kesho kutwa ataenda kuchukua fomu ya urais kutoka kwenye ofisi za CCM, Dodoma.


- Januari anasisitiza kuwa Tanzania MPYA itajengwa na viongozi wenye fikra mpya.

- Januari ahaidi kuwa na mawaziri wasiozidi 18 tu katika baraza lake la mawaziri endapo chama chake kikimpa ridhaa ya kugombea urais kupitia CCM.


-Januari Makamba anaorodhesha ajenda tano kuu atakazo simamia endapo chama chake kitampa ridhaa ya kugombea na hatimae kuunda serikali.

............Update............

....Januari ahaidi kuwa serikali yake itatoa mikopo maalumu kwa vijana watakaomaliza vyuo vikuu ambao watapata changamoto ya ajila ili na wao waweze kufungua makampuni yao ili waweze kujizalishia kipato.

....Pia amesema katika serikali yake atahakikisha sekta ya nyumba ina mchango wa zaidi ya 25%, wakati sasa hivi ni chini ya 4% ikimaanisha Watanzania wengi hawana makazi. Hivyo katika uongozi wake hilo la makazi atalipa kipaumbele tofauti na ilivyo sasa.

....Uvuvi, serikali yake itaanzisha mifuko maaalumu ya kukopesha wavuvi ili waweze kununua vifaa vya uvuvi ili isaidie kuboresha vipato vya wavuvi na pia kukuza sekta hiyo kwa kasi.

....Serikali yangu itaongeza udahili wa walimu haswa kwa masomo ya sayansi. Pia ameahidi kutatua changamoto za walimu kama vile mishahara yao kuwa duni, kukosa posho na stahiki mbalimbali. Ahaidi serikali yake kutatua kero hizo kwa kukuza na kuboresha maslahi yao.

.... RUSHWA, amesema kuwa kulizungumza na kulipigia kelele tatizo la rushwa sio njia ya kulimaliza tatizo hilo.

....ARDHI, jinsi ya kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Serikali yake itabainisha kisheria maeneo ya kilimo, mifugo na makazi. Pia amesema wakulima na wafugaji watamiliki maeneo yao kisheria. Atatumia teknolojia mpya ya satellite kutekeleza hayo kupitia kituo maalumu kitachoundwa chini ya serikali yake. Lakini pia kituo hicho kitasaidia pia na mambo ya kiusalama.

....AFYA, kila Mtanzania lazima awe na bima ya afya, kila Mtanzania lazima apate huduma bora ya afya bila ya kujali kipato chake.
 
Tatizo letu siyo yupi anaweza kumeza nondo bila kusoma...tunataka mtu akataye simamia rasilimali za taifa hili ziweze kutusuma katika maendeleo na kutunufaisha kila mmoja kwa namna yake.

Mkuu mtazamo wako kama wangu, tatizo la nchi yetu sio mtu anaeongea sana au msomi sana laaa,
Hao tunao toka uhuru wasomi ma prof wamejaa, watu wenye madigrii wamejaa, waongeaji wamejaa, lakini Leo 50+ ya uhuru hata hatueleweki sijui tunakwenda mbele au tunarudi nyuma,
Nchi inahitaji mzalendo mwenye kuwa na uchungu na rasilimali zetu na mwenye kulinda maslahi ya nchi kabla ya maslahi ya tumbo lake na family yake
 
Back
Top Bottom