Mkuu nishapata tatizo kama hilo, nilikunywa metakelfin muda wa saa sita na nusu ya mchana, kuanzia saa kumi mwili uliharibika hasa sehemu hizo ulizozitaja, nilipanic maana nilikuwa sijawahi kufikiria magonjwa ya zinaa, sikuweza hata kuvaa suruali ama nguo za ndani ilibidi nivae LUNGI ya kihindi na kukimbizwa hospitali, kwenda pale madaktari wakaniambia ni allergy ya Sulphur iliyomo katika Metakelfin, kuanzia hapo nikapewa dawa za kupunguza sumu hiyo na kukatazwa kutotumia dawa zozote zile zenye sulphur. Nakushauri nenda kuonana na Daktari atakupa ushauri na dawa ya kupunguza hali hiyo na pengine kukushauri kama walivyonishauri mimi juu ya sulphur.Pole