KUTOKA ZANZIBAR: Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi awaaga madaktari bingwa wa kichina waliomaliza muda wao

KUTOKA ZANZIBAR: Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi awaaga madaktari bingwa wa kichina waliomaliza muda wao

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Sehemu ya matukio katika picha ambapo mheshimiwa rais wa Zanzibar Dr. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na madaktari bingwa kutoka nchini china walipokuja Ikulu Zanzibar kumuaga baada ya kufanya kazi ya kutoa huduma ya Afya katika kisiwa cha Unguja kupitia hospitali ya Mnazi mmoja na Kisiwa cha Pemba kwenye hospitali ya Abdalla mzee.

_DSC5053.JPG

☝🏾RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Madaktari Bingwa benchi ya 30 kutoka Nchini China waliomaliza muda wao wa mwaka mmoja Zanzibar kutoka huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba, kwanza Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyika kazi zake Zanzibar

_DSC5085.JPG

☝🏾MADAKTARI Bingwa kutoka nchini China waliokuwa wakitoa huduma ya Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar na Abdalla Mzee Mkoani Pemba waliomaliza muda wao wa mwaka wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wa Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani)


_DSC5068.JPG

☝🏾WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jljamii wazee jinsia na watoto Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt.Fatma Mrisho, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani

_DSC5107.JPG

☝🏾RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya mlango wa zanzibar balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Zhang Zhisheng , wakati wa hafla ya kuwaaga Madaktari hao.

_DSC5116.JPG

☝🏾RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Visiwa vya Unguja na Pemba Kiongozi wa Madaktari Bingwa wa Benchi la 30 kutoka China Dr.Wang Yiming , baada kumaliza muda wao wa mwaka mmkoja kutokwa huduma za Afya visiwani Zanzibar.


Picha zote na Ikulu.
 
Back
Top Bottom