Kutokana na hamahama hii, Mbowe azomewe?

Kutokana na hamahama hii, Mbowe azomewe?

Habari wana jamvi.

Mwaka jana baada ya timu ya Arsenal kufanya vibaya kwenye ligu kuu ,mashabiki wake kote duniani walipaza na kumzomea kocha mkuu Wenger aondoke ili kupisha mabadiliko ya kiungozi kwenye timu hiyo.

Kocha Wenger aliwapuuza sana mashabiki hao lakini mwisho wa siku aliamua kusikiliza kilio chao na kuamua kuondoka kwa kukubali ukweli kwamba timu inapofanya vibaya wakulaumiwa ni kocha na ni lazima hutimuliwa.

Nimetolea mfano wa timu ya Arsenal kwa kulinganisha na ufanyaji vibaya wa chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.
Chadema toka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 imepoteza mvuto kwa wananchi ! Madiwani na wabunge wa chadema wanajivua nyasifa zao ndani ya chama hicho na kuomba kupokelewa ccm.! Yote haya yanatokea kocha akiwa Mbowe.

Kwa hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho hamna namna ambayo Mbowe atazuia anguko la chadema nchini.
Ili kuruhusu mabadiliko na morali mpya ndani ya chadema ni lazima kocha Mbowe azomewe na kufukuzwa kama kocha Arsene Wenger wa Arsenal.

Hoja ya kwamba Mbowe akiondoka chadema itaangukia mikononi mwa wasaliti haina mashiko mbele ya wapenda mabadiliko.
Hata akina Lipumba , Mbatia , Cheyo , Mrema walikuwa wanasema hivi hivi eti wakiondoka chama kitakaliwa na wasaliti . Kiko wapi sasa?

#Mbowe must Go



Sent using Jamii Forums mobile app
Cheap politicians are easily bought and confused
 
Baada ya October 28 ndiyo tutajua azomewe au asizomewe
 
Lazaro Nyalandu alimgaragaza Tundu Lisu kwenye kura za kamati kuu.!

Huyu mzee wa MIGA ,mwanasheria a Acacia anaaminika na nani sasa kama hadi kamati kuu anashindwa kura??
 
Mbowe anasubiri nini? Chama kometoka wabunge 200 hadi kubaki mmoja!
 
Tundu Lisu ameamua kumvaa mazima
 
Back
Top Bottom