Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa ameuelekeza Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutumia Bilioni 40 fedha za dharura kukarabati miundombinu ya madaraja na barabara zilizoharibiwa na mvua za Elinino zinazoendelea kunyesha nchini.
Akizungumza katika kikao kazi na TARURA, Waziri Mchengerwa pia amewaelekeza Viongozi wote ngazi ya Mikoa, Wilaya na Halmashauri kusimamia na kufuatilia kwa makini na kutoa taarifa za kazi za ukarabati wa miundombinu hiyo.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini,Dkt. Abdulaziz Abood amefanya ziara ya kushutukiza kwenye Kata ya Mazimbu kwa lengo la kujionea athari ya mvua katika miundombinu ya barabara zilizopo katika Kata hiyo. Mhe. Mbunge ameshuhudia namna miundombinu ya barabara hizo zilivyoathiriwa hasa kipande cha...
Barabara ya Banana Kitunda (Dar es Salaam) imekuwa ni kero kubwa sana kama vile hatuna viongozi wanaotusimamia. Barabara ni mbovu na kila kipindi cha mvua usafiri ni shida na magari yanaharibika sana, tunaomba hii taarifa imfikie Mbunge wetu ni Jerry Silaa.