Kutokana na matamshi yake, Prof. Kabudi ataondolewa Wizara ya Mambo ya Nje kama ilivyokuwa kwa Mkurugenzi wa SSRA kutokana na issue ya Kikokotoo

Kutokana na matamshi yake, Prof. Kabudi ataondolewa Wizara ya Mambo ya Nje kama ilivyokuwa kwa Mkurugenzi wa SSRA kutokana na issue ya Kikokotoo

Usichokijua ni kwamba mawaziri wa Magufuli hawafanyi kazi kwa utashi wao wala kwa kuwa huru.Huwa wanafanya kazi kwa kuangalia boss wao anataka nini na huwa anafurahishwa na kitu gani.Ile siyo akili ya Kabudi,ile ni akili ya Magufuli ipo kwenye kichwa cha Kabudi.Usipokuwa makini unaweza kufikiri kuwa ni Kabudi anaongea kumbe anaeongea pale ni Magufuli.
Mkuu, upo sahihi! Nakumbuka yule naibu wa Wizara ya Afya, (Ndugulile) alipojidai kuleta taaluma yake kwenye suala la korona, akamfurusha!
 
Haya matusi tungeyaweka kwanza mpaka pale tutakapokuwa tayari Wananchi wetu wote wana maji safi na salama, nyumba bora, vyumba vya madarasa sambamba na elimu bora, huduma za afya zinazofikika na kila raia n.k.

Baada ya hapo ndio tuanze kuwaporomoshea tukiwatumia Watu wenye uwezo na vipaji hivyo kama huyo Prof.
 
Kwa hiyo minyoo unakubaliana Kabudi anasimamishwa kazi kwa kuwaita Wabunge wa EU ni wahuni? km Mada inavyotaka.
Mimi nasisitiza Uchaguzi umeisha na tunaona Demokrasia Duniani haipo tena, hata Taifa la Russia, sembuse huko kwa Trump hatambui matokea licha ya kumuweka Jaji wake siku za mwishomwisho au kutaka kuishambulia Iran sasa hivi?
namaanisha tuache ndoto, mbabe kajenga uwanja wa ndege na wa mpira kwake turidhike tafuta mlo wako, huko Rwanda ameongeza miaka 7 na Uganda pia, nimemalizia msiiponze JF kwa kutokukubali matokeo, Mada ya Uchaguzi ilishafungwa tusubiri mingine mi5
Hao CCM waache watamalizana wao kwa wao wameanza na Mikopo ya magari bado watibuana wao km G55 ilivyokuwa
Uchaguzi unakuja upya kabla ya 2025 kwani laana ya wapiga kura itaanza kufanya kazi kuanzia miezi 6 mpaka mwaka na ikishika vizuri lazima uchaguzi ururidiwe upya pasipo uchakachuaji wa CCM
 
Yani hapa unapondea mabeberu then unaanza kulia Lia ukiulizwa matumizi ya hela yao unaanza kuwatukana, mabeberu hao hao ndo wanatengeneza vitu unavyotumia kuanzia technology na kila kitu hata ndege mnazojisifia mumenunua kwao, so mabeberu ni Kama maji usipoyaoga utayanywa. Tuache kibri Cha kijinga kwa watu waliotuzidi akili kila kitu Hadi dhambi
Uwezo pekee wa akili waliotuzidi hao mabeberu ni kwamba wametushinda sisi katika kukushawishi wewe kwamba wana uwezo mkubwa wa kukuhadaa kwamba wewe una akili ndogo kuliko wao. Ukinielewa nitag, pls!
 
Yani hapa unapondea mabeberu then unaanza kulia Lia ukiulizwa matumizi ya hela yao unaanza kuwatukana, mabeberu hao hao ndo wanatengeneza vitu unavyotumia kuanzia technology na kila kitu hata ndege mnazojisifia mumenunua kwao, so mabeberu ni Kama maji usipoyaoga utayanywa. Tuache kibri Cha kijinga kwa watu waliotuzidi akili kila kitu Hadi dhambi
CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu wizi ufisadi wa CCM ndipo hugeuka na kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
 
Uchaguzi unakuja upya kabla ya 2025 kwani laana ya wapiga kura itaanza kufanya kazi kuanzia miezi 6 mpaka mwaka na ikishika vizuri lazima uchaguzi ururidiwe upya pasipo uchakachuaji wa CCM
Kwa hiyo maandamano yasiyo na ukomo "mmeyakoli offu"??? Thanks for choosing the path of peace once more. Nadhani mnakoelekea sasa ni katika hatua za awali za uzalendo halisi!
 
Uchaguzi unakuja upya kabla ya 2025 kwani laana ya wapiga kura itaanza kufanya kazi kuanzia miezi 6 mpaka mwaka na ikishika vizuri lazima uchaguzi ururidiwe upya pasipo uchakachuaji wa CCM
Kurudiwa jamani ni ndoto kabla ya 2025 hata km ikitokea nini wapo watakaorithi lkn ICC haina ubavu
pia hawa wajumbe wapiga kura mnawajua? wengi wamejificha kwenye mitumba, mama lishe, wapiga debe, wafanyakazi wote, include masoldier, sasa njoo wanamtandao na wapiga kelele hawafiki 1% na hata ukiwaambia tokeni barabarani ni vitisho tu bora haka Mange Kimambi peke yake alitingisha.
Tulishaelezana hapa Watanzania hawaujui Uchaguzi wanafikiri ni mabox KURA NI KUHESABU NA KULINDA
 
Mbona unajibu out if context inaonyesha una arrogance behavior, na hyo picha ya mzee wa watu inahusikaje sasa na huu Uzi, cdu si chama tu Cha ugermany Kama kilivo ccm, au Chauma so sioni jipya, kulinganisha na mada inayohusu EU hapa
Ila kabudi hyo wizara imemshinda uwezo na akili kulikuwa Kuna haja gani kuwaita hao wabunge wa EU wapuuzi wakati EU michango yake kwa taifa ni muhimu, ni Bora hyo wizara ingempata January Makamba naona anafaa ana exposure flani hivi
Huu si ndiyo mchango wako wa mada iliyotolewa? Nimi nimekujibu accordingly. Sasa inakuwaje mimi niko out of the context? Ukifuatilia mazungumzo ya hiyo kamati ya Bunge lako tukufu la Ulaya utaona mchangiajia hoja mmoja wapo mkubwa kwenye huo mjadala wa hiyo kamati alikuwa Penner mmoja wa kutoka chama cha CDU cha ujerumani na yeye wewe ndiyo unamwona amechangia hoja ya maana sana kiasi kwamba matamshi ya waziri wako wa mambo ya nchi za nje unamwona ameshindwa kazi yake.

Na ndiyo maana nimekuuliza kama umesha mwona huyo mchangiaji wa hoja wa kutoka hicho chama cha CDU cha ujerumani anavyo onekana? Kwa watu walio au wanaoishi ujerumani na kuwajua wajerumani walivyo, appearance ya huyu politician inaonyesha moja kwa moja kuwa ni Penner.

Kama huwajui wajerumani walivyo ningekushauri ukae kimya kwani unadandia mabasi ambayo hayakupeleki unakotaka kwenda. Hii itakuwa ngumu sana kwako ku argue na watu wenye kuwajua hao wahuni.
SmartSelect_20201122-095356_Gallery.jpg

Na ndiyo maana nika kuambia kuwa huyu ni Penner, kwani hata kupiga meno mswaki hajui na mtu yuko Ulaya.

Lakini kwa mkoma kama wewe unaona sawa maadam ni mzungu. Nyie ni washamba sana na malimbukeni wa wazungu.
 
Kwa hiyo maandamano yasiyo na ukomo "mmeyakoli offu"??? Thanks for choosing the path of peace once more. Nadhani mnakoelekea sasa ni katika hatua za awali za uzalendo halisi!
waongo wanamageuzi na wakereketwa
ni Mange Kimambi tu ndiye aliyewahi itisha maandamano
safari hii wamewawahi waaandamanaji, ambao ni wamachinga, wamewapa biashara bila kodi wala leseni
 
Kwa hiyo maandamano yasiyo na ukomo "mmeyakoli offu"??? Thanks for choosing the path of peace once more. Nadhani mnakoelekea sasa ni katika hatua za awali za uzalendo halisi!
waongo wanamageuzi na wakereketwa
ni Mange Kimambi tu ndiye aliyewahi itisha maandamano
safari hii wamewawahi waaandamanaji, ambao ni wamachinga, wamewapa biashara bila kodi wala leseni
 
CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu wizi ufisadi wa CCM ndipo hugeuka na kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
Hapana. Mabeberu ndio wakiona nchi yetu inakubali tu kuonewa, kukandamizwa, kubagazwa, kudharauliwa, rasilimali zetu kusombwa ughaibuni na kuhonyolewa hovyo, vibaraka wao kushika hatamu za uongozi kwa maslahi yao, wakati tukiwanyenyekea na kuwalamba migongo, wanatusifu sana wakidai eti tumekomaa katika diplomasia ya kimataifa, demokrasia & utawala bora; ila tukiwa responsible na rasilimali zetu na kuchakata maendeleo na ustawi wetu sisi wenyewe bila kuwategemea wao, watatupachika lakabu nyingi za uzushi pamoja na kutusakama na kujaribu kutuwekea vikwazo vya kiuchumi. Hatutakubali this time!
 
waongo wanamageuzi na wakereketwa
ni Mange Kimambi tu ndiye aliyewahi itisha maandamano
safari hii wamewawahi waaandamanaji, ambao ni wamachinga, wamewapa biashara bila kodi wala leseni
Sikuelewi, kwa sababu maandamano yamebuma kwa vile raia wameona hamna mashiko, vinginevyo yasingezuilika. Mkubaligi kushindwa basi, siyo ugonjwa, sawa???
 
Umesema sahihi katika context ya historia ya ubabe duniani. Lakini kwa sasa strategy hiyo haina nafasi. Na hilo lilikuwa valid katika kipindi ambacho dunia ilikuwa ikitafuta mbabe. Ukiniambia kwenye battle hiyo Tanzania nayo imo, nahisi kama ni kujidanganya wenyewe. Dunia imefunguka sana wakati huu na neno "Diplomacy" limekuwa likijitwalia umaarufu siku hata siku. Tujisahihishe
Diplomacy huwa ni lugha inayotumika pale tu wanapoona hakuna alternative ya coercion ama hakuna sababu kubwa ya kushurutisha. Kwa maneno mengine, diplomatic language is just diplomacy. Period! Ndiyo maana walipotuvunjia diplomancy, nasi tumelazimika kuwajibu in kind. Vinginevyo tungetafsirika kipolitikia kama koloni na wahanga wa EU. Kuwa na viongozi sampuli ya JPM & Kabudi wenye sera za "no nonsense" ni ufahari sana! Kenya walijaribu kugusa waya wa umeme, hatimaye wakaishia kuomba radhi mara mbilimbili.
 
CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu wizi ufisadi wa CCM ndipo hugeuka na kuwaita wanaume wenzao mabeberu utazani CCM ni mbuzi jike
Na wewe je ni kodoo jike? Wewe vipi? Mbona hueleweki?
 
Diplomacy huwa ni lugha inayotumika pale tu wanapoona hakuna alternative ya coercion ama hakuna sababu kubwa ya kushurutisha. Kwa maneno mengine, diplomatic language is just diplomacy. Period! Ndiyo maana walipotuvunjia diplomancy, nasi tumelazimika kuwajibu in kind. Vinginevyo tungetafsirika kipolitikia kama koloni na wahanga wa EU. Kuwa na viongozi sampuli ya JPM & Kabudi wenye sera za "no nonsense" ni ufahari sana! Kenya walijaribu kugusa waya wa umeme, hatimaye wakaishia kuomba radhi mara mbilimbili.
Umepitia literature vizuri kujua kwanini Baba waTaifa aling'atuka mapema? Mi nilikuwepo na mambo yalianza hivi hivi. Self seclusion haina nafasi duniani. Kitu kizuri ni kwamba wazungu wanatuchukulia poa tu kwamba waafrika hatujui tulitendalo
 
Wewe umesoma historia kujua kwa nini kisiwa kidogo cha Kyuba kiliamua kusimama kidete dhidi ya hyperpower kama Marekani na kukataa kabisa kusalimisha uhuru wake???
 
Kama ambavyo yule mama aliekuwa Mkurugenzi wa SSRA alivyoendolewa katika nafasi yake kutokana na issue ya kikokotoo, ndivyo hivyo Waziri wa Mambo ya Nje, Prof. Kabudi atavyoweza kuondolewa kwenye hiyo wizara kutokana na matamshi yake juu ya wabunge wa Bunge la Ulaya.

Kama ambavyo sitaki kuamini yule mama aliekuwa boss wa SSRA alifanya maamuzi yale bila baraka za wakubwa, ndivyo ambavyo sitakuwa tayari kuamini Prof. Kabudi kaongea aliyoyaongea bila baraka za wakubwa wake, ila kama alivyopigwa chini yule mama, ndivyo ambavyo hata Prof. Kabudi nae anaweza kupigwa chini.

Kwa sasa ninahakika mzee Baba atakuwa anasoma upepo na akiona unavuma vibaya, basi ni swala la muda tu kabla hatujaona Msigwa akija na Press release ya mtu kutenguliwa ingawa bado anaweza kupewa wizara nyingine baraza kamili litapotangazwa.

Hata hivyo, kwa siku hizi za mwanzo, msishangae Mzee Baba nae akaja na kauli kama za msaidizi wake, ila moto ukiwaka, atageuka na ataanza kwa kumtoa huyo msaidizi wake katika hiyo nafasi.

Kwahiyo hapa tutegemee scenario mbili: moja ni Kabudi kuondolewa kulingana na upepo utavyovuma, na scenario ya pili ni boss wake kuja kupigilia msumari matamshi ya Kabudi na baadae kugeuka na kuchukua hatua iwapo bwana wakubwa hawa watakuja juu. Ni swala la muda tu kabla haya hayajatimia.

Yakitokea kama navyotabiri, hawa MATAGA ambao leo hii wanamshangilia Kabudi, ndio watakuwa wa kwanza kumpongeza Mzee Baba na kuanza kamponda Kabudi.

Kabla sijamaliza, naomba niwape na scenario ya tatu: Kabla jua halijazama, Kabudi anaweza kujitokeza hadharani na kusema amenukuliwa vibaya ingawa hii haitamsaidia litapokuja swala la kutolewa mbuzi wa kafara.

Time will tell.
Amewaita bunge la EU watu wahuni wachache., natamani hii kauli waipate wale mabeberu wanaoenda wakipigiwa magoti
 
Back
Top Bottom