Kutokana na ruzuku kupungua CHADEMA kupunguza wafanyakazi. Wafanyakazi waja juu walia upendeleo

Ruzuku kupungua! Kwa hiyo wanavuta ruzuku kutoka kwa wale 19 wa viti maalum na yule mmoja wa Jimbo? Kama la, sasa hiyo ruzuki kidogo wanapateje?
 
Kama michango ya mifuko ya jamii kwa wafanyakazi wao hawaipeleki, tukiwapa nchi si ndo itakuwa balaa watakwiba sana hao majambazi waliojificha kwenye kichaka cha jina DEMOKRASIA NA MAENDELEO
 
Kwani nyinyi mlishawalipa malimbikizo ya mishahara wafanyakazi wenu?

Hatapunguzwa mfanyakazi hata mmoja. Kwa taarifa yako huyo kakulisha matango pori.
Wengi wanaofanya kazi CHADEMA wanajitolea. Hao wa kwako waende Lumumba kuna ruzuku ya kutosha kuwapa ajira.
 
Mwenyekiti wenu anachagua mawaziri vichaa kisa msukuma mwenzake. Mambo ya kitaifa analeta usukuma
 
Kufa kwa chadema hakumaanishi kufa kwa upinzani Tanzania. Tunavyo vyama vingi tu vya upinzani nchini kwetu na bila shaka kimoja wapo kitajitokeza kuwa chama kikuu cha upinzani 2025 baada ya chadema kung'atuka.
Hongereni kwa Kazi nzuri!

Najua kila mwana -CCM sasa hivi ana maisha mazuri mno baada ya Kazi nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…