Mafanikio ya China ya kupata "ushindi kamili" kwenye vita vyake vya kutokomeza umasikini uliokithiri kunatajwa na wasomi wengi kama matokeo ya mpango kabambe, utawala bora na nia njema ya kisiasa nchini humo.
Dk. Beatrice Matiri-Maisori ambaye ni mshauri wa maswala ya uchumi na diplomasia kati ya China na Afrika anasema uondoaji wa umaskini imekuwa ni lengo la muda mrefu la Rais wa China Xi Jinping.
China imefanikisha lengo lake la kumaliza umaskini uliokithiri mbele ya ratiba yake ya awali ya mwaka 2030.
Dk. Beatrice Matiri-Maisori anasema kasi ya utekelezaji wa kazi za kuondoa umaskini zimeshuhudiwa hata wakati nchi hiyo ikikabili janga la corona ambapo hospitali na miundo mbinu husika ilijengwa ndani ya muda mfupi.
Anasema hata hivyo, mfumo wa kisiasa na utawala bora na kuwa na malengo vimechangia pakubwa uondoaji wa haraka wa umaskini nchini China.
Anaona kuwa nchi za Afrika zinaweza kushirikiana na china na kujifunza njia za kukuza uchumi.