Kichuguu mkuu wangu, tatizo letu wa TZ ni kuogopa kusema ukweli na kujawa na unafiki.
Bila kumuambia bwana mkubwa kaa pembeni kwa hiari uachie ofisi umeshindwa hakika tutateketea tunajiona au shurti itumike alazimishwe kwa kukosa imani.
Huyu bwana anaendesha mambo mengi kwa mizaha na ukali upo pale tuu pasipo na sifa binafsi.
Watu wanadhani katia woga katika utendaji kumbe katia woga katika uteuzi, watu wanaogopa kupoteza nafasi sio kupoteza weledi.
Corona imechukuliwa kizembe sana hapa kwetu tena kuliko Italy au US na hata matokeo yanafichwa utadhani kwa kufanya hivyo ndio wanakinga wengine.
Hatua ya mwisho eti tuombe kama taifa! Hivi hill huwa in agizo LA Rais au viongozi wa kiroho ndio wajibu wao? Na walikuwa wanatuhimiza na tunafanya kila siku. Lakini kasema yeye kumbe hizo siku tatu zimekuwa sio za kumtukuza na kumuomba Mungu bali kumsifu yeye na kumtukuza kwamba ndiye kiongozi wa kipekee duniani mwenye majibu ya corona. Nini hii??
Tuambiane ukweli, Magufuli ashukuriwe kwa yote aliyofanya kama mtumishi wa umma lakini aambiwe apumzike. Tena hakuna haja ya kusubiri October, aache Mama Samia awe acting hadi uchaguzi vinginevyo tunaweza kuyapata ya Italy na kusaga meno. Kwani lazima awe yeye hata kama kafeli?