Kutokomezwa kwa corona virus itategemeana sana na ukomavu wa viongozi wetu

Kutokomezwa kwa corona virus itategemeana sana na ukomavu wa viongozi wetu

Wametangaza katika hali isiyo thabiti. Ni kama tahadhari ya kawaida ya hiari badala ya kutangaza kama tahadhari ya dharura ambayo itakuwa enforced kwa kutumia taasisi za serikali.
Hapo ndipo lilipo tatizo la watanzania. Mnaambiwa msiende ufukweni kuna tsunami halafu mnataka polisi wakasimamie msiende huko

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Idadi halisi ni hyo 170.
Kama una idadi nyingine tuambie.
Unadhani Magufuli afiche idadi ana muogopa nani?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
Ni kweli hawaogopi watanzania na anajua kuwa hawajitambui wala hawajielewi kazi yao wao kusifia ujinga tu

Ndio maana alikata kufunga mipaka ili kuzuia international transmission na mpaka Leo hakuna lockdown ili kuzuia local transmission na bado watu wanamsifia kwa kufanya hayo tena sanasana wale wa nguo za kijani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndipo lilipo tatizo la watanzania. Mnaambiwa msiende ufukweni kuna tsunami halafu mnataka polisi wakasimamie msiende huko

Sent from my SM-A720F using Tapatalk

Sawa baba wewe ambaye siye mtanzania kwani unadhani kuwa watanzania wote huenda ufukweni.
 
Endeleeni kubishana badala ya kuingia kwenye kisafina chako
 
Serikali yetu imeshafeli kutulinda tusubiri rehema za Mungu tu

WHO wanasema madhara ya corona yatakayo tokea bara la Africa yatakuwa makubwa sana kuliko mabara yote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hili swala watu wameligeuza LA kisiasa, tuliowapa mamlaka wanasita kuchukua hatua.huko Mbele Ni kilio
 
Nina wasiwasi Korona itatuua sana Tanzania kuliko kipindupindu, HIV-Aids na hata town. Naona kama kumekuwa na ubabaishaji sana katika kusimamia janga hili.

Viongozi wa serikali msifanye mchezo wa kufurahisha watu kuwa maisha ni kama kawaida. Trump alifanya hivyo akaiingiza Marekani katika Janga. Viongozi kuweni seriousi na gonjwa hili ambalo ni tofauti kabisa na HIV ambayo mtu alikuwa anaweza kujitunza asiipate kabisa, lakini gonjwa hili halina cha kujitunza; ukiingia mitaani tu linakuzoa.

Fundisheni watu seriously, siyo hii ya lele mama. Tanzania tumewahi kuumizwa na milipuko ya kipindupindu, HIV-AIDS lakini yote hayo yalikuwa yanategemea matendo yako mwenywe; hili jipya halitegemei matendo yako kabisa bali ni exposure tu. Kqwenye daladala, sokoni, mitaani, madukani na sehemu zote za watu wengi utalizoa.

Tusidananyike kuwa barakoa ndiyo dawa, hapana, hiyo inasaidia kwa kiwango kidogo sana. Kwetu nchi ya jasho, unaweza kuwa na barakoa ukazoa hiyo virus kwenye jasho lako na kubeba wakati unafuta jasho.

Mkuu unafikiri nini kifanyike?
 
Kama mnacho mkitakacho fanyeni wenyewe basi. Ni usalama wenu

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
ungeweka uchama pembeni,alafu uvae viatu,kuna watanzania wa hali ya chini sana innocents wanakwenda kuathilika, corona haikuwa kitu kigeni hapo awali, serikali ilichukuwa hatua gani za kuzuia huu ugonjwa usisambae nchini!
 
unajua kama viongozi wetu walizalau covid-19 ilipo kuwa inaingia nchini,mipaka na airport ziliendelea kufanya kazi, viongozi wachache wakatumia covid kama siasa na kushindana na kukashifiana, na hawa ndio viongozi wetu, wenye uelewa na ufahamu wa aina hiyo! ninapata ukakasi kuamini suruhisho la hili jambo naona kabisa hili janga linasambaha kirahisi, lakini halitaondoka kirahisi ifahamike hivyo.

kwa baadhi ya viongozi wetu wenye dhamana kwa namna hili janga linavyo chukuliwa na aina ya mikakati inavyo pelekwa,naona corona itapiga kambi bongo na kuondoka itatusumbua sana, viongozi wenye dhamana, badilisheni mtazamo,hili ni janga tena janga kubwa, ukizingatia janga halina tiba wala kinga, mbaya zaidi hili janga linapiga yeyote, mtoto, kiongozi, waziri, na wengine wengi.

imeisha...
Kutokomeza ni kupata dawa tu,
Mengine ni story za kijiweni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa taarifa za kisayansi, kirusi chochote si kiumbe hai, hivyo basi kinaweza kutokomezwa kisipokaa kwenye kiumbe hai. Njia sahihi ni kujihakikishia mtu mwenyewe huambukizwi wala kuambukiza.

Kama kilivyo kirusi cha UKIMWI, njia mhimu ya kwanza ni kupima. Kama hujaambukizwa unaacha ngono zembe au unaacha kabisa.

Kwa COVID-19, Serikali iwezeshe kila mtu kupimwa ili walioambukizwa wachukue hatua za kutokuambukiza na wengine tahadhari za kujikinga na maambukizi, kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya.
 
ungeweka uchama pembeni,alafu uvae viatu,kuna watanzania wa hali ya chini sana innocents wanakwenda kuathilika, corona haikuwa kitu kigeni hapo awali, serikali ilichukuwa hatua gani za kuzuia huu ugonjwa usisambae nchini!
Usiwaze siasa kila mahali mkuu, acha tabia ya ulalamishi chukua hatua. Mengi yameshasemwa na hakuna jipya, ni wewe na familia yako sasa.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom