Kutokuaminiana katika mahusiano

Kutokuaminiana katika mahusiano

MoneyHeist4

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2017
Posts
2,134
Reaction score
3,192
Hi wana JF natumaini mko wazima wa afya kabsa.
Mimi ni member wa siku nyingi sana huku JF na nimekuwa wa kujifunza mambo mengi tu kupitia humu ila leo nimeamua kuja na hili swala la kutokuaminiana katika mahusiano.

Mpenzi wangu kusema ukweli haniamini kabsa nisipopokea simu analeta maneno kibao, kiasi kwamba mpaka ananikosesha amani, kwa sasa nimeamua tusiwasiliane kwa wiki 2 na leo ni siku ya tatu hatuwasiliani.

Nahitaji mawazo yenu wana jf kama maamuzi yangu yako sahihi au nitakuwa nimekosea kufanya hayo maamuzi??

Tukumbuke huu msemo *KAMA AMESHIDWA KUKUAMINI VILE VILE HAWEZI KUKUPENDA*
 
Acha porojo, kama Ulizoea kupokea simu ya mwenzio hata kabla haijaita wakati mnaanza mahusiasno sasa leo iweje uache kuipokea simu yake!?

Ulijenga mnara mzuri kwa njia ya mawasiliano imara ila sasa , unajitoa ufahamu kwa kumpotezea huyo Mwenzio.

Kumbuka, ukijenga mnara,, usiivunje ngazi ya kupandia juu.
 
Acha porojo, kama Ulizoea kupokea simu ya mrembo hata kabla haijaita wakati unatupia ndowano sasa leo iweje uache kuipokea simu yake!?

Ulijenga mnara mzuri kwa njia ya mawasiliano imara ila sasa , unajitoa ufahamu kwa kumpotezea huyo binti.

Kumbuka, ukijenga mnara,, usiivunje ngazi ya kupandia juu.

Nampenda na staki kumpoteza ila kero zimezidi sana hata ukiwa kazini ukishindwa kupokea simu ni shida tupu anakuwazia mengine kabsa ambayo hata huyafikirii.
 
Nampenda na staki kumpoteza ila kero zimezidi sana hata ukiwa kazini ukishindwa kupokea simu ni shida tupu anakuwazia mengine kabsa ambayo hata huyafikirii.

Kaa naye mweleze Kwa upole na mwambie majukumu yako kazini.

Pia, nawe usiwe kiazi ukiwa na muda Mtafute, mtumie ujumbe hata mfupi ili ajue upo naye japo umebanwa na kazi.
 
Kaa naye mweleze Kwa upole na mwambie majukumu yako kazini.

Pia, nawe usiwe kiazi ukiwa na muda Mtafute, mtumie ujumbe hata mfupi ili ajue upo naye japo umebanwa na kazi.

Tunachat sana ila akipiga usipopokea tu anajua niko na mchepuko
 
Back
Top Bottom