Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya mambo ambayo yanaudhi wakati mwingine ni watu kutolea maoni jambo ambalo hawalijui au hata kuchukua muda kulijua hasa kama liko ndani ya uwezo wao. Katika mechi hii ya leo goli la kwanza la Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba limezua sokomoko uwanjani nan je ya uwanja. Maoni ya wengi ambao wanalipinga goli hilo ni madai kuwa refa “kawabeba” Yanga kwa sababu goli lile lilifungwa baada ya mchezaji kuunawa mpira yaani, kugusa mkono mpira wakati anapokea pasi.

Ni wazi kuwa wengi ambao wanafikiria mchezaji alifanya kosa lililohitaji faulu (free kick) wanafanya hivyo kwa sababu hawajui sheria za soka zinazohusu kuunawa mpira. Refa alikuwa sahihi kutokutoa faulu pale kwani hakukuvunjwa sheria zozote.

Kuelewa kama mchezaji alifanya kosa ni lazima turejee Kanuni za Mchezo ambazo zinatumika kuongoza mchezo wa Soka duniani. Kanuni hizi zimepitishwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na kama mtu hatosoma na kuelewa basi basi anaweza kufanya makosa ambayo mtu yeyote anayejua kanuni za mchezo huu hawezi kuyafanya. Bahati nzuri – nafahamu mchezo wa soka vizuri – na ninaweza kutolea maoni ambayo makocha na wachezaji wengine watakubaliana name kuhusiana na kutokuwepo kosa katika goli la kwanza la Yanga.

Kanuni za soka zinazohusu faulu mbalimbali (Kanuni ya 12) katika ukurasa wa 119 inaeleza wazi kuwa “Handling the ball involves a deliberate act of a player making contact with the ball with his hand or arm” yaani “Kuugusa mpira kwa mkono inahusisha kitendo cha mchezaji kwa makusudi kugusana na mpira kwa kiwiko chake au mkono”.

Sasa mojawapo ya mambo ambayo mwamuzi anatakiwa kuangalia kuhusiana na hili na ni jambo la kwanza kabisa – na ninaamini ndilo lililofamya refa kutokutoa faulu – ni kuangalia “mwelekeo wa mkono uliko mpira siyo wa mpira uliko mkono”. Hii ina maana kuwa endapo mpira unapigwa na mkono wa mchezaji hauufuati mpira – kama kuuzia, kubadilisha mwelekeo wake n.k – na mpira ukaenda ukagusa mkono bila kuonesha kusudio la mchezaji kuugusa mpira huo basi ni vigumu kutoa faulu au hata penati.

Ukielewa kanuni hii na ukipata muda kuangalia video ya goli la Yanga na ukimsikiliza mtangazaji unaweza kuamini kosa la mchezaji ni kuugusa mpira kwa mkono. Kosa kama hilo halipo kwenye kanuni za Soka! Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuona video ile na kudai kuwa ilikuwa ni kosa na refa hakuibeba Yanga bali amesimamia kanuni zinazoongoza mpira. Ni vizuri mashabiki, wachezaji na watu wengine wanaotolea maoni soka watumie muda kujifunza kanuni za mpira ili wasije kujikuta wanasababisha mambo ya aibu kama yaliyotokea leo uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii.

Ni muhimu kujua sheria hizi ili kuondoa ulazima wa kufanya mambo ya uharibifu yaliyotokea uwanjani ambayo asili yake ni kutokujua kanuni za mchezo. Mashabiki wanapopata hasira kwa kitu ambacho hawakijui – wenyewe wakidhani wanazijua sheria zote za mchezo – ni aibu na kashfa kwa watu wote wanaopenda kandanda.

Upande wa pili, tumeona pia goli zuri, nono na tamu lilifungwa na Simba kupitia kona. Ni goli liliotumia nafasi ya uzembe wa golikipa kukaa kwenye kona. Bahati nzuri miaka yangu nikicheza soka nilicheza kama golikipa na goli kama hili linamuuma sana golikipa kwani anajua kosa lake ni kukaa mbali na posti ya goli wakati wa kona. Golikipa yeyote mzuri anajua wakati wa kona anatakiwa awe nyuma ya wachezaji wake wote kwani ni rahisi kwake kuupima mpira unaokuja kutoka kwenye kona na kuweza kukimbia mbele kwenye eneo lolote kuukoa. Ni vigumu sana kwa golikipa kukaa mbele ya wachezaji, au katikati na mpira ukajaa juu yake kama ilivyotokea leo; ni vigumu kurudi kinyume nyume kuuwahi mpira unaokuja kwenye posti. Hapa ndio uzuri wa goli hili ulipo.

Nje ya hapo, ni kweli tuna matatizo kwenye soka letu lakini inawezekana siyo tu tatizo la uchezaji lakini pia tatizo la kutokujua kanuni za mpira. Yeyote anayetaka kufundisha soka, kucheza au kushangilia soka ni vizuri ajifunze kanuni za msingi za mpira.

Unaweza kupata kanunizamchezo kwa kubonyeza hapa.
 

Attachments

Acheni kuchambua kimahaba Mpira ulipunguzwa kasi na mkono, otherwise ungesema refa akishaamua Iwe sawa au sio inapaswa kukubali lakini kiuhalisia refa alikosea japo si kigezo cha kufanya vurugu kwa washabiki wa Simba.
 
Uzuri nilikuwa nimekaa karibu sana na goli alilofunga Tambwe, niliona vizuri sana lile tukio halipo kama unavyoeleza wewe, hata camera za TV hazijachukua tukio vizuri zimechukua kwa Pembeni sana, hapakuwa na utata Ile mpira haujaufata mkono kama unavyodhani, Tambwe aliivuta mpira ukabaki mikononi sec kadhaa kabla ya kutua Chini
 
Ingepatikana video ya goli ingesaidia walau,
 
TANGU UWE MCHUMIA TUMBO UMEKUWA UNAJIPENDEKEZA SIJAJUA UNATAKA NAFASI YA MURO

YANI MTU NA AKIL ZAKE TIMAMU ANAPINGA KUWA HAIKUWA KOSA ET REFA YUKO SAHIHI KAMA UMEZOEA KUFATILIA CHANETA NI HUKOHUKO
 
Zungumzia Goli LA Ajib. Tatizo lilianzia hapo?
 
Jinsi tukio la tambwe lilivyofanyika katika speed ya 4g hata Colina angeweka kati tu,mbona henry kashafanyaga hizo mambo mara nyingi tu,hawa wanalalamika kama mwanamke aliyepewa ujauzito bar.
 

Chaplin acha uongo yaani wewe uliona vizuri kuliko camera,duh sasa basi utakuwa na jicho la mwewe
 
Arsenal leo usiku laurent koscielny kapiga goli la mkono live na Burnley hawavunja viti. Haya matimu ya Tanzania mengi washabiki wake vichwa maji
 
Umeandika mengi kumbe utumbo mtupu, mkono ndo ulifata mpira na akauseti mpira kwenda mbele kwa chini ili apige shuti. Tena alitakiwa kupigwa red.
Kacheki goli la leo alilofunga koscielny dhidi ya Burnley ndio utajua upeo wako wa uelewa ulipoishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…