Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya mambo ambayo yanaudhi wakati mwingine ni watu kutolea maoni jambo ambalo hawalijui au hata kuchukua muda kulijua hasa kama liko ndani ya uwezo wao. Katika mechi hii ya leo goli la kwanza la Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba limezua sokomoko uwanjani nan je ya uwanja. Maoni ya wengi ambao wanalipinga goli hilo ni madai kuwa refa “kawabeba” Yanga kwa sababu goli lile lilifungwa baada ya mchezaji kuunawa mpira yaani, kugusa mkono mpira wakati anapokea pasi.

Ni wazi kuwa wengi ambao wanafikiria mchezaji alifanya kosa lililohitaji faulu (free kick) wanafanya hivyo kwa sababu hawajui sheria za soka zinazohusu kuunawa mpira. Refa alikuwa sahihi kutokutoa faulu pale kwani hakukuvunjwa sheria zozote.

Kuelewa kama mchezaji alifanya kosa ni lazima turejee Kanuni za Mchezo ambazo zinatumika kuongoza mchezo wa Soka duniani. Kanuni hizi zimepitishwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na kama mtu hatosoma na kuelewa basi basi anaweza kufanya makosa ambayo mtu yeyote anayejua kanuni za mchezo huu hawezi kuyafanya. Bahati nzuri – nafahamu mchezo wa soka vizuri – na ninaweza kutolea maoni ambayo makocha na wachezaji wengine watakubaliana name kuhusiana na kutokuwepo kosa katika goli la kwanza la Yanga.

Kanuni za soka zinazohusu faulu mbalimbali (Kanuni ya 12) katika ukurasa wa 119 inaeleza wazi kuwa “Handling the ball involves a deliberate act of a player making contact with the ball with his hand or arm” yaani “Kuugusa mpira kwa mkono inahusisha kitendo cha mchezaji kwa makusudi kugusana na mpira kwa kiwiko chake au mkono”.

Sasa mojawapo ya mambo ambayo mwamuzi anatakiwa kuangalia kuhusiana na hili na ni jambo la kwanza kabisa – na ninaamini ndilo lililofamya refa kutokutoa faulu – ni kuangalia “mwelekeo wa mkono uliko mpira siyo wa mpira uliko mkono”. Hii ina maana kuwa endapo mpira unapigwa na mkono wa mchezaji hauufuati mpira – kama kuuzia, kubadilisha mwelekeo wake n.k – na mpira ukaenda ukagusa mkono bila kuonesha kusudio la mchezaji kuugusa mpira huo basi ni vigumu kutoa faulu au hata penati.

Ukielewa kanuni hii na ukipata muda kuangalia video ya goli la Yanga na ukimsikiliza mtangazaji unaweza kuamini kosa la mchezaji ni kuugusa mpira kwa mkono. Kosa kama hilo halipo kwenye kanuni za Soka! Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuona video ile na kudai kuwa ilikuwa ni kosa na refa hakuibeba Yanga bali amesimamia kanuni zinazoongoza mpira. Ni vizuri mashabiki, wachezaji na watu wengine wanaotolea maoni soka watumie muda kujifunza kanuni za mpira ili wasije kujikuta wanasababisha mambo ya aibu kama yaliyotokea leo uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii.

Ni muhimu kujua sheria hizi ili kuondoa ulazima wa kufanya mambo ya uharibifu yaliyotokea uwanjani ambayo asili yake ni kutokujua kanuni za mchezo. Mashabiki wanapopata hasira kwa kitu ambacho hawakijui – wenyewe wakidhani wanazijua sheria zote za mchezo – ni aibu na kashfa kwa watu wote wanaopenda kandanda.

Upande wa pili, tumeona pia goli zuri, nono na tamu lilifungwa na Simba kupitia kona. Ni goli liliotumia nafasi ya uzembe wa golikipa kukaa kwenye kona. Bahati nzuri miaka yangu nikicheza soka nilicheza kama golikipa na goli kama hili linamuuma sana golikipa kwani anajua kosa lake ni kukaa mbali na posti ya goli wakati wa kona. Golikipa yeyote mzuri anajua wakati wa kona anatakiwa awe nyuma ya wachezaji wake wote kwani ni rahisi kwake kuupima mpira unaokuja kutoka kwenye kona na kuweza kukimbia mbele kwenye eneo lolote kuukoa. Ni vigumu sana kwa golikipa kukaa mbele ya wachezaji, au katikati na mpira ukajaa juu yake kama ilivyotokea leo; ni vigumu kurudi kinyume nyume kuuwahi mpira unaokuja kwenye posti. Hapa ndio uzuri wa goli hili ulipo.

Nje ya hapo, ni kweli tuna matatizo kwenye soka letu lakini inawezekana siyo tu tatizo la uchezaji lakini pia tatizo la kutokujua kanuni za mpira. Yeyote anayetaka kufundisha soka, kucheza au kushangilia soka ni vizuri ajifunze kanuni za msingi za mpira.

Unaweza kupata kanunizamchezo kwa kubonyeza hapa.
Na kuongeza zaidi kwenye ilo uliloongelea pia waangalie goli la Arsenal la 2/2016 na mkono wa Laurent Koscielny na bado Burnley hawajalalamika
 
Umekuwa biased sana,..
Vipi kuhusu goli lililokataliwa la Ajib?
Ilikuwa offiside kweli au la..!?
Na kwa nini hukulielezea..??

goli la Ajibu ni offside. Tatizo watu tunajifanya tunajua kila kitu wakati refa yule ndio professionalism yake ile kaona ile ni offside na ukifatilia move inaonekana kabisa ni offside. Tatizo kituo cha Azam wanazi wa simba ni wengi wanaonyesha slow motion ktk eneo kabla ya offside kutokea lakini hawaonyeshi mundelezo wa movement mpaka offside ilipotokea.
 
Ata kwenye kampeni Nape alisikika akisema ata kwa bao la mkono mtashinda,

sasa kila mahali mnatafuta ushindi kwa bao la mkono,

Utakuwa ni mtu wa ajabu sana kukubaliana na lile bao la Yanga.
Kaangalie goli la Arsenal v. Burnley alichofanya Laurent Koscielny na hujasikia malalamishi
 
Siku za hivi karibuni Arsenal nao wamekuwa kama Yanga wanabebwa sana.
Ohooooo?? Wewe kila team inabebwa? Kwa namna hiyo ukishajenga mentality hiyo huwezi kuamini team yako inachofanya maana utaona unaonewa kila mara
 
... Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. ...

Kama haikuwa makusudi, ni kwa nini aukunje mkono kuubeba mpira?

tmb.jpg
 
Kwenye siasa umekosa hata ujumbe wa nyumba kumi harafu leo naona umeanza kumsujudia MANJI. Hivi utajidhalilisha mpaka lini
 
Jinsi tukio la tambwe lilivyofanyika katika speed ya 4g hata Colina angeweka kati tu,mbona henry kashafanyaga hizo mambo mara nyingi tu,hawa wanalalamika kama mwanamke aliyepewa ujauzito bar.
Tehe Tehe
 
Sasa refa kafungiwa kwa nin hii TZ bana...[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mleta mada kafanya uchambuzi mzuri sana unaozidi kutuhakikishia kua ni kweli goli la tambwe lilikubaliwa kimakosa!
 
simba waliondoka na matokeo yao kwenda taifa tambwe aliwasuprise walipohamaki wakaanza kucheza na viti mara ya pili wanakimbilia viti badala ya kuhamasisha wachezaji wao wakomboe magoli
 
Mleta mada kafanya uchambuzi mzuri sana unaozidi kutuhakikishia kua ni kweli goli la tambwe lilikubaliwa kimakosa!


makosa yapo ktk mpira na yanatokea sana refa sio mungu nigeria walikataliwa goli la penati la victor ikpeba ktk fainali na cameroon mwaka 2000 baade walikili ni makosa maradona anawapa ubingwa argentina kwa style hiyo uvumilivu na wered wenzetu vinawabeba ila vilabu vyetu vichanga lazima ucheze na viti
 
Back
Top Bottom