Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Pia mimi sikufunga....ila mwanzo ni mgumu sana as unakua huelewi...unadhani kila siku unauza tu...kuna siku huuzi hata boxer..cha msingi uvumilivu.
Biashara nzuri ni ya mwenzako,
Unaweza uwe umepakana na mwenzako anauza bidhaa tofauti na yako, ukaona Huyu mbona anauza sana,
Jidanganye ubadilishe....,
Kuna watu wanaamua kuuza kwa bei ya hasara ili mzigo umuondokee.

Kiufupi tamaa za namna hio hazifai,
Na unapofungua biashara mpya jipe mda wateja wapafahamu na kuzoea duka lako,
Ndio maana Kutouza sio sababu ya kufunga Biashara,
Kikubwa tuu wateja wawe wanakuja hata kuulizia bei na kuangalia, Ni suala la muda tuu na upepo.
 
Biashara nzuri ni ya mwenzako,
Unaweza uwe umepakana na mwenzako anauza bidhaa tofauti na yako, ukaona Huyu mbona anauza sana,
Jidanganye ubadilishe....,
Kuna watu wanaamua kuuza kwa bei ya hasara ili mzigo umuondokee.

Kiufupi tamaa za namna hio hazifai,
Na unapofungua biashara mpya jipe mda wateja wapafahamu na kuzoea duka lako,
Ndio maana Kutouza sio sababu ya kufunga Biashara,
Kikubwa tuu wateja wawe wanakuja hata kuulizia bei na kuangalia, Ni suala la muda tuu na upepo.
Kabisa yaani...maana wateja walivyozoea wakaanza kuniagiza niwaletee mzigo wanaotaka wao hata kama dukani haupo...au naweza chukua mzigo nikiwalenga watu fulani kisha nawapigia simu waje kucheck...taratibu tu mambo yanakua poa hususan ukishaanza kuwa na wateja wako wakudumu lakini inachukua muda.
 
Someni hapo

According to the U.S. Bureau of Labor Statistics (BLS), this isn't necessarily true. Data from the BLS shows that approximately 20% of new businessesfail during the first two years of being open, 45% during the first five years, and 65% during the first10 years. Only 25% of new businesses make it to 15years or more.
Aisee, somo kubwa hili.
 
Inategemeana na aina ya biashara, ila kuna biashara kukosa kabisa mteja ni jambo lisilowezekana..

Ila mwisho wa siku biashara ni stress sana, mimi toka biashara yangu ya hardware ilivyokufa sina hamu kabisa na hizi "physical business"....kifupi siwezi wekeza hela yangu mtaani.
Mkuu biashara yako ya hdw imekufanye mkuu nipe mbinu na mm nisje kuzika yangu
 
Mkp sas hijawai kwenda kwa babu
Nipo kwenye hii biashara, usemayo ni kweli na mimi yalinikuta hivyo hivyo, na baadhi ya siku yanajirudia,
Ila sikukata tamaa, kikubwa tuu mwisho wa mwezi sikosi faida baada ya malipo yote.
Ila Kiukweli kuna kipindi nilitaka nifunge.
sa hujasaas
 
Uko dukani kwako unalala Hii ni tabia ya wadada wengi, hawaheshimu Biashara zao kabisa. Unaingia dukani unakuta kaweka kadoro, katandika kiko chini kalala, Ulishawahi kwenda Benki ukakuta wamelala kwakua tu hawana wateja, halafu Biashara zenyewe hizi tunafanya ni za kuibiana wateja, sasa wewe waje wakuamshe kweli?hata kama hamna wateja, weka kiti kaa, kulala dukani ni bora ufunge duka
Mteja anakuja unaongea na simu, tena umbea na porojo hata si kitu cha maana, badala ya kumuambia subiri nitakucheki baadaye eti unamuangalia mteja akichagua.wateja Wengine wakikuona hivyo wanaona kama dharau wanaondoka. Hata kama una kitu cha muhimu unaongea na cha lazima, zima simu kisha muombe samahani mteja, tafuta namna ya kuaga hudumia mteja. Ila kumuangalia mteja wakati unaongea na simu ni ishara ya dharau na watakukimbia.
Unamuelekeza mteja bidhaa ukiwa umekaaa; Naingia dukani kwako, nataka labda nguo, eti badala unyanyuke kunielekeza, utembee na mimi, kama ni nguo unionyeshe na kunishushia, umekaa unaniekeleza, angalia ile pale juu, saizi yako ile sijui nini! Ndugu yangu Biashara ilivyo ngumu tangu asubuhi hujauza kitu unakaa ili nini, ni dharau wakati una shida ndiyo maana uko hapo, nyanyuka ongea na mteja mpaka aone aibu kutokununua.
Kujaza marafiki zako dukani kwako hakuna sehemu ya kupita; Nakuja dukani kwako, mlangoni kuna marafiki zako, wamekaa mlangoni, halafu hata hawajiongezi, mtu anataka kununua tight yake ya mahips hatakiw atu wajue wao wapo tu, hata hawatoki. Biashara yako ni kijiwe cha kupigia stori, tena wanawake ndiyo unakuta wakati wanakula wametandika na mkeka wamekaa hapo unakuja mpaka unafikiri hili ni duka au kuna maulidi hapa! Aisee inaboa, labda kama unauza Figo ila kama ni hivi vitu vya kawaida wateja utawasikia kwenye taarifa ya habari!
Kukaa kwenye maduka ya watu mteja akija mpaka akuite; Aisee hii kitu inaniboa mpaka basi, unaenda dukani, unaingia eti mpaka umuite mtu, anakuja alikua anapiga umbea kwingine. Aisee kama haupo dukani kwako unapoteza wateja wengi sana kwani watanzania wengi hawendi dukani kununua bali kushangaa, hivyo anapokukosa dukani huondoka na anaogopa kukuita kwakua hakupanga kununua, ila kama upo atakuja, atashangaa utampiga viswahili atanunua. Mimi nikiingia kwako halagfu ndiyo naona unanikimbilia hata kama nimependa kitu ukifika tu na mimi naondoka bila kusema chochote!
Kutokumkumbuka mteja ambaye ameshakuja zaidi ya mara mbili; Kama unauza vitu na unataka kutengeneza wateja wa kudumu basi kumbuka wateja wako. Si lazima kukumbuka jina au alinunua nini lakini kumbuka hata sura. Akirudi tena mchangamkiwe na kama unataka kumkosha zaidi kumbuka na vitu anavyopenda. Lakini najua sio wote mnaoweza kukumbuka hivyo kila mteja mchangamkie na akikukumbuka basi changamka kama unamjua vile na si anakuambia anakujua wewe unauliza uliza na kujifanya humjui!
Kudharau mteja ambaye unaona hana kitu mbaye ya ambaye unamuona ana kitu na kauli mbovu; Rafiki yangu mmoja ana hii tabia, anaangalia mteja ana pesa kiasi gani, ana muonekano gani ndiyo amheshimu. Mteja wa hali ya chini akija anamjibu mbovu, kwa dharau, aisee kama uko hivi acha. Kwanza huyo unayemdharau anaweza kuwa Bosi au anajuana na mabosi akakukimbizia wateja. Pili mtu mwenye akili akiona unahdarau mtu wa chini anakuchukia, anakuona una dharau na anaweza hata yeye asije kununua.
Kukaa katikati ya mlango; Ni duka lako, uko peke yako lakini umekaa katikati ya mlango, mtu anakuja hajui kama wewe ni muuzaji au mtu amekaa, mbaya zaidi ukiona mteja hunyanyuki. Hapana, kaa pembeni kidogo, sehemu ambayo unaonekana lakini si katikatio ya mlango. Tena wadada ndiyo hata haweki kiti anakaa chini kabisa na mmiguu kanyoosha kiasi kwamba mteja kuja kuingia ni mpaka usimame hivyo anakata tamaa kabla ya kuingia kwakua kama hana mpango wa kununua siku hiyo anaona ni kero kukuamsha tu.
Kufunga funga duka kila mara; Kwakua unaona kuwa hakuna wateja unadfunga duka, watu wanakuja hata huwaoni labda hujafunga ila umeondoka. Hii inakimbiza wateja, wakishajua kuwa hufungui wanakuona kama hufanyi Biashara, labda ausbuhi hufungui sijui mpaka baada ya muda gani basi inakimbiza sana wateja. Ukishaamua kufanya Biashara basi zingatia sana muda, watu wajue kuwa duka la flani linafunguliwa muda falani na flani na si kuwa unafungua kwa kubeep tu.
Kila ukipata muda kaa mwenyewe kwenye Biashara yako; Kama umeajiri mtu basi kila ukipata muda penda kukaa wewe zaidi. Kwanza inakusaidia kusimamia Biashara yako vizuri kupunguza kuibiwa, pili inakukutanisha na wateja, wanakuzoea na unatengeneza wateja wako na tatu ni kuwa wewe ndiyo una uchungu zaidi na hiyo Biashara, mdfanyakazi biahsara ikifa anahamia kwingine wewe ikifa unarudi nyumbani, hapana simama wewe kila wakati katika Biashara yako kila unapopata muda.
Kwa Kweli mzee umeongea ukweli mtupu kuanzi Sasa HV sitoki nje ya ofc yangu na uzuri Nina tabia nzuri Sana mteja akija dukani nasimamaga nahakikisha Nampa maelezo ya kutosha na Hili la kusimam limenilipa sana
 
Asilimia kubwa ya sisi Watanzania hufanya biashara kimazoea, hatutafuti maarifa mapya ya kukuza mtaji wala mbinu za kuvutia wateja.
Utakuta mtu anafanya biashara lakini ana lugha mbovu kwa mteja, na wengine hufikia hata kumdharau mteja wakihisi hana pesa!
Huenda hata wewe uko hivyo, wateja wanaenda kupata huduma sehemu nyingine.
Kuna wateja pia wanadharau
 
Back
Top Bottom