Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Hebu ziweke hapa hizo mbinu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Asilimia kubwa ya sisi Watanzania hufanya biashara kimazoea, hatutafuti maarifa mapya ya kukuza mtaji wala mbinu za kuvutia wateja.
Utakuta mtu anafanya biashara lakini ana lugha mbovu kwa mteja, na wengine hufikia hata kumdharau mteja wakihisi hana pesa!
Huenda hata wewe uko hivyo, wateja wanaenda kupata huduma sehemu nyingine.
Ww inaonekana hujawah kufanya biashara km ungefnya biashara wala usingeandika hayo, biashara bongo ni ndago Sana ndo unaenda
 
My advice to you jaribu kufanya maombi kabla ya kufungua biashara yako au tumia Neno mungu nisaidie siku Ya leo niuze japo kiasi kadhaa fanya hivi kila ufunguoapo alafu usisahau kunipa feedback ok
okey.
 
Uko dukani kwako unalala Hii ni tabia ya wadada wengi, hawaheshimu Biashara zao kabisa. Unaingia dukani unakuta kaweka kadoro, katandika kiko chini kalala, Ulishawahi kwenda Benki ukakuta wamelala kwakua tu hawana wateja, halafu Biashara zenyewe hizi tunafanya ni za kuibiana wateja, sasa wewe waje wakuamshe kweli?hata kama hamna wateja, weka kiti kaa, kulala dukani ni bora ufunge duka
Mteja anakuja unaongea na simu, tena umbea na porojo hata si kitu cha maana, badala ya kumuambia subiri nitakucheki baadaye eti unamuangalia mteja akichagua.wateja Wengine wakikuona hivyo wanaona kama dharau wanaondoka. Hata kama una kitu cha muhimu unaongea na cha lazima, zima simu kisha muombe samahani mteja, tafuta namna ya kuaga hudumia mteja. Ila kumuangalia mteja wakati unaongea na simu ni ishara ya dharau na watakukimbia.
Unamuelekeza mteja bidhaa ukiwa umekaaa; Naingia dukani kwako, nataka labda nguo, eti badala unyanyuke kunielekeza, utembee na mimi, kama ni nguo unionyeshe na kunishushia, umekaa unaniekeleza, angalia ile pale juu, saizi yako ile sijui nini! Ndugu yangu Biashara ilivyo ngumu tangu asubuhi hujauza kitu unakaa ili nini, ni dharau wakati una shida ndiyo maana uko hapo, nyanyuka ongea na mteja mpaka aone aibu kutokununua.
Kujaza marafiki zako dukani kwako hakuna sehemu ya kupita; Nakuja dukani kwako, mlangoni kuna marafiki zako, wamekaa mlangoni, halafu hata hawajiongezi, mtu anataka kununua tight yake ya mahips hatakiw atu wajue wao wapo tu, hata hawatoki. Biashara yako ni kijiwe cha kupigia stori, tena wanawake ndiyo unakuta wakati wanakula wametandika na mkeka wamekaa hapo unakuja mpaka unafikiri hili ni duka au kuna maulidi hapa! Aisee inaboa, labda kama unauza Figo ila kama ni hivi vitu vya kawaida wateja utawasikia kwenye taarifa ya habari!
Kukaa kwenye maduka ya watu mteja akija mpaka akuite; Aisee hii kitu inaniboa mpaka basi, unaenda dukani, unaingia eti mpaka umuite mtu, anakuja alikua anapiga umbea kwingine. Aisee kama haupo dukani kwako unapoteza wateja wengi sana kwani watanzania wengi hawendi dukani kununua bali kushangaa, hivyo anapokukosa dukani huondoka na anaogopa kukuita kwakua hakupanga kununua, ila kama upo atakuja, atashangaa utampiga viswahili atanunua. Mimi nikiingia kwako halagfu ndiyo naona unanikimbilia hata kama nimependa kitu ukifika tu na mimi naondoka bila kusema chochote!
Kutokumkumbuka mteja ambaye ameshakuja zaidi ya mara mbili; Kama unauza vitu na unataka kutengeneza wateja wa kudumu basi kumbuka wateja wako. Si lazima kukumbuka jina au alinunua nini lakini kumbuka hata sura. Akirudi tena mchangamkiwe na kama unataka kumkosha zaidi kumbuka na vitu anavyopenda. Lakini najua sio wote mnaoweza kukumbuka hivyo kila mteja mchangamkie na akikukumbuka basi changamka kama unamjua vile na si anakuambia anakujua wewe unauliza uliza na kujifanya humjui!
Kudharau mteja ambaye unaona hana kitu mbaye ya ambaye unamuona ana kitu na kauli mbovu; Rafiki yangu mmoja ana hii tabia, anaangalia mteja ana pesa kiasi gani, ana muonekano gani ndiyo amheshimu. Mteja wa hali ya chini akija anamjibu mbovu, kwa dharau, aisee kama uko hivi acha. Kwanza huyo unayemdharau anaweza kuwa Bosi au anajuana na mabosi akakukimbizia wateja. Pili mtu mwenye akili akiona unahdarau mtu wa chini anakuchukia, anakuona una dharau na anaweza hata yeye asije kununua.
Kukaa katikati ya mlango; Ni duka lako, uko peke yako lakini umekaa katikati ya mlango, mtu anakuja hajui kama wewe ni muuzaji au mtu amekaa, mbaya zaidi ukiona mteja hunyanyuki. Hapana, kaa pembeni kidogo, sehemu ambayo unaonekana lakini si katikatio ya mlango. Tena wadada ndiyo hata haweki kiti anakaa chini kabisa na mmiguu kanyoosha kiasi kwamba mteja kuja kuingia ni mpaka usimame hivyo anakata tamaa kabla ya kuingia kwakua kama hana mpango wa kununua siku hiyo anaona ni kero kukuamsha tu.
Kufunga funga duka kila mara; Kwakua unaona kuwa hakuna wateja unadfunga duka, watu wanakuja hata huwaoni labda hujafunga ila umeondoka. Hii inakimbiza wateja, wakishajua kuwa hufungui wanakuona kama hufanyi Biashara, labda ausbuhi hufungui sijui mpaka baada ya muda gani basi inakimbiza sana wateja. Ukishaamua kufanya Biashara basi zingatia sana muda, watu wajue kuwa duka la flani linafunguliwa muda falani na flani na si kuwa unafungua kwa kubeep tu.
Kila ukipata muda kaa mwenyewe kwenye Biashara yako; Kama umeajiri mtu basi kila ukipata muda penda kukaa wewe zaidi. Kwanza inakusaidia kusimamia Biashara yako vizuri kupunguza kuibiwa, pili inakukutanisha na wateja, wanakuzoea na unatengeneza wateja wako na tatu ni kuwa wewe ndiyo una uchungu zaidi na hiyo Biashara, mdfanyakazi biahsara ikifa anahamia kwingine wewe ikifa unarudi nyumbani, hapana simama wewe kila wakati katika Biashara yako kila unapopata muda.
Aisee mkuu.. salute sana.. umeongea vingi vya maana... Mpaka nimejiuliza kama una degree ya biashara za maduka.

Yaani umelenge kwenye consumer behavior unaiunganisha na namna muuzaji anatakiwa a behave.. kwa ufupi wewe utakuwa umekomaa sana kwenye biashara
 
Kwa biashara halali nikiwa na maana isiyo na ndumba hicho ni kitu cha kawaida.

Nini cha kufanya

Usifikirie wateja kwanini hawaji maana hauna ahadi nao Wewe fikiria mambo yako mengine.

Usitegemee biashara moja uwe na mbili au tatu au hata zaidi haziwezi kukutupa zote lakini ukiwa na moja ikibuma ndo kama hivyo.
Umeongea point sana
 
Miradi ya serikali malipo yaweza kuchukua mwaka mzima, kuna jamaa alikuwa na stationery kubwa sana akawa anapewa tenda serikalini (halmashauri moja) malipo ilikuwa kimbembe...
Ukitaka biashara ife mapema jiingize kwenye miradi ya serikali. Unaweza lipwa baada ya miaka 2
 
Mkuu siri yenyewe ni hii,watu wengi wenye viduka vya hardware ni wajanja wajanja wanawafanyia wateja ukanjanja kwa kuwauzia vitu vya low grade/quality kwa bei ya ubora,mfano nondo reject kwa bei ya nondo imara na kupata super profit.
Hapo ndo umeongea sasa siri.. na hii kweli ni siri aisee.. sema sasa kujua unapata wapi hizo reject ndo utofauti unapoanzia hapo..
 
Nilianza biashara ya nguo miaka kadhaa nyuma,na nikawa nasimama mwenyewe golini as hiyo ndo ilikua ishu yangu ya kunitoa.

Siku ya kwanza nikauza nguo moja,nikaanza kutetemeka sababu nilidhani nikiweka tu pamba watu watakuja.

Siku ya pili sijauza kitu kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku,roho iliniuma sana sikulala usiku,huku nikiwaza ni bora niajiriwe maana biashara si rahisi.

Siku ya tatu,mpaka saa mbili jioni sijauza kitu,nikaanza kuwaza uchawi na uthubutu wa kwenda kwa babu,ghafla akatokea mshikaji mmoja hivi na demu wake,wakafanya shopping ya laki mbili na nusu nilitamani nifunge muda huo,nakuanzia hapo ndo nikajua biashara siyo poa poa kama wanavyosema insipirational speakers.
 
Nilianza biashara ya nguo miaka kadhaa nyuma,na nikawa nasimama mwenyewe golini as hiyo ndo ilikua ishu yangu ya kunitoa.

Siku ya kwanza nikauza nguo moja,nikaanza kutetemeka sababu nilidhani nikiweka tu pamba watu watakuja.

Siku ya pili sijauza kitu kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku,roho iliniuma sana sikulala usiku,huku nikiwaza ni bora niajiriwe maana biashara si rahisi.

Siku ya tatu,mpaka saa mbili jioni sijauza kitu,nikaanza kuwaza uchawi na uthubutu wa kwenda kwa babu,ghafla akatokea mshikaji mmoja hivi na demu wake,wakafanya shopping ya laki mbili na nusu nilitamani nifunge muda huo,nakuanzia hapo ndo nikajua biashara siyo poa poa kama wanavyosema insipirational speakers.
Hii biashara siiiachi hivi hivi nitakomaa mayo hadi kodi yangu ya Fremu iishe ndio notafanya tathmini

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Huenda wanga walifanyia mkutano kwenye baraza yako ya biashara na kujamba sana.
 
Kwenye biashara changamoto nyingine ambayo n kubwa mikopo.
 
Nikishaitoa siyo siri tena! Lengo la kusema kuna siri, kama upeo wako wa kuchambua mambo, huwezi kuelewa!
Unatakiwa ufahamu kuwa biashara si kila mtu anaweza kuifanya, kukaa kwangu kimya kunaweza kusiwe msaada kabisa! Ila kwa kusema walao kuna hiyo siri kutamfanya yule anayetaka kuingia/kuanza ama yule anayefanya(na hajui) kama atasoma nilichoeleza afanye utafiti wa kina juu ya biashara anayotaka kuifanya ili asije kupata hasara kabla ya kuona matunda yake!
Wafanya biashara wakubwa na wa kati wote wana siri kubwa sana, juu ya biashara zao na kamwe huwezi kuzikuta zimeanikwa hadharani, na mtu kujua kuwa wanasiri hizo basi kutamfanya atafiti zaidi ajue kuna nini ndani ya hizo biashara!
Hivyo mimi kusema hivyo tayari ni faida, kama hujiongezi ni shauri yako!

Lakini pia nilichosema kama uliona kuwa hakina msaada kwako basi na wewe ungepita kimya kimya bila kuniqoute!
Mara nyingi ukisikia ni siri, ujue ni mambo ya kishirikina. Labda unikosoe mkuu.
 
Back
Top Bottom