Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Uko dukani kwako unalala Hii ni tabia ya wadada wengi, hawaheshimu Biashara zao kabisa. Unaingia dukani unakuta kaweka kadoro, katandika kiko chini kalala, Ulishawahi kwenda Benki ukakuta wamelala kwakua tu hawana wateja, halafu Biashara zenyewe hizi tunafanya ni za kuibiana wateja, sasa wewe waje wakuamshe kweli?hata kama hamna wateja, weka kiti kaa, kulala dukani ni bora ufunge duka
Mteja anakuja unaongea na simu, tena umbea na porojo hata si kitu cha maana, badala ya kumuambia subiri nitakucheki baadaye eti unamuangalia mteja akichagua.wateja Wengine wakikuona hivyo wanaona kama dharau wanaondoka. Hata kama una kitu cha muhimu unaongea na cha lazima, zima simu kisha muombe samahani mteja, tafuta namna ya kuaga hudumia mteja. Ila kumuangalia mteja wakati unaongea na simu ni ishara ya dharau na watakukimbia.
Unamuelekeza mteja bidhaa ukiwa umekaaa; Naingia dukani kwako, nataka labda nguo, eti badala unyanyuke kunielekeza, utembee na mimi, kama ni nguo unionyeshe na kunishushia, umekaa unaniekeleza, angalia ile pale juu, saizi yako ile sijui nini! Ndugu yangu Biashara ilivyo ngumu tangu asubuhi hujauza kitu unakaa ili nini, ni dharau wakati una shida ndiyo maana uko hapo, nyanyuka ongea na mteja mpaka aone aibu kutokununua.
Kujaza marafiki zako dukani kwako hakuna sehemu ya kupita; Nakuja dukani kwako, mlangoni kuna marafiki zako, wamekaa mlangoni, halafu hata hawajiongezi, mtu anataka kununua tight yake ya mahips hatakiw atu wajue wao wapo tu, hata hawatoki. Biashara yako ni kijiwe cha kupigia stori, tena wanawake ndiyo unakuta wakati wanakula wametandika na mkeka wamekaa hapo unakuja mpaka unafikiri hili ni duka au kuna maulidi hapa! Aisee inaboa, labda kama unauza Figo ila kama ni hivi vitu vya kawaida wateja utawasikia kwenye taarifa ya habari!
Kukaa kwenye maduka ya watu mteja akija mpaka akuite; Aisee hii kitu inaniboa mpaka basi, unaenda dukani, unaingia eti mpaka umuite mtu, anakuja alikua anapiga umbea kwingine. Aisee kama haupo dukani kwako unapoteza wateja wengi sana kwani watanzania wengi hawendi dukani kununua bali kushangaa, hivyo anapokukosa dukani huondoka na anaogopa kukuita kwakua hakupanga kununua, ila kama upo atakuja, atashangaa utampiga viswahili atanunua. Mimi nikiingia kwako halagfu ndiyo naona unanikimbilia hata kama nimependa kitu ukifika tu na mimi naondoka bila kusema chochote!
Kutokumkumbuka mteja ambaye ameshakuja zaidi ya mara mbili; Kama unauza vitu na unataka kutengeneza wateja wa kudumu basi kumbuka wateja wako. Si lazima kukumbuka jina au alinunua nini lakini kumbuka hata sura. Akirudi tena mchangamkiwe na kama unataka kumkosha zaidi kumbuka na vitu anavyopenda. Lakini najua sio wote mnaoweza kukumbuka hivyo kila mteja mchangamkie na akikukumbuka basi changamka kama unamjua vile na si anakuambia anakujua wewe unauliza uliza na kujifanya humjui!
Kudharau mteja ambaye unaona hana kitu mbaye ya ambaye unamuona ana kitu na kauli mbovu; Rafiki yangu mmoja ana hii tabia, anaangalia mteja ana pesa kiasi gani, ana muonekano gani ndiyo amheshimu. Mteja wa hali ya chini akija anamjibu mbovu, kwa dharau, aisee kama uko hivi acha. Kwanza huyo unayemdharau anaweza kuwa Bosi au anajuana na mabosi akakukimbizia wateja. Pili mtu mwenye akili akiona unahdarau mtu wa chini anakuchukia, anakuona una dharau na anaweza hata yeye asije kununua.
Kukaa katikati ya mlango; Ni duka lako, uko peke yako lakini umekaa katikati ya mlango, mtu anakuja hajui kama wewe ni muuzaji au mtu amekaa, mbaya zaidi ukiona mteja hunyanyuki. Hapana, kaa pembeni kidogo, sehemu ambayo unaonekana lakini si katikatio ya mlango. Tena wadada ndiyo hata haweki kiti anakaa chini kabisa na mmiguu kanyoosha kiasi kwamba mteja kuja kuingia ni mpaka usimame hivyo anakata tamaa kabla ya kuingia kwakua kama hana mpango wa kununua siku hiyo anaona ni kero kukuamsha tu.
Kufunga funga duka kila mara; Kwakua unaona kuwa hakuna wateja unadfunga duka, watu wanakuja hata huwaoni labda hujafunga ila umeondoka. Hii inakimbiza wateja, wakishajua kuwa hufungui wanakuona kama hufanyi Biashara, labda ausbuhi hufungui sijui mpaka baada ya muda gani basi inakimbiza sana wateja. Ukishaamua kufanya Biashara basi zingatia sana muda, watu wajue kuwa duka la flani linafunguliwa muda falani na flani na si kuwa unafungua kwa kubeep tu.
Kila ukipata muda kaa mwenyewe kwenye Biashara yako; Kama umeajiri mtu basi kila ukipata muda penda kukaa wewe zaidi. Kwanza inakusaidia kusimamia Biashara yako vizuri kupunguza kuibiwa, pili inakukutanisha na wateja, wanakuzoea na unatengeneza wateja wako na tatu ni kuwa wewe ndiyo una uchungu zaidi na hiyo Biashara, mdfanyakazi biahsara ikifa anahamia kwingine wewe ikifa unarudi nyumbani, hapana simama wewe kila wakati katika Biashara yako kila unapopata muda.

Ebu mpe credit CONTROLA umecopy maelezo yake mpaka nukta
 
Dah usiombe biashata inakufia unaiona afu bora ianze slow ije ichanganynye mbele huko ila unaanza fresh af chaa wateja wanaanza kupotea unajipa matumain labd kesho labda kesho ukistuka mzigo ushakata
 
Nikishaitoa siyo siri tena! Lengo la kusema kuna siri, kama upeo wako wa kuchambua mambo, huwezi kuelewa!
Unatakiwa ufahamu kuwa biashara si kila mtu anaweza kuifanya, kukaa kwangu kimya kunaweza kusiwe msaada kabisa! Ila kwa kusema walao kuna hiyo siri kutamfanya yule anayetaka kuingia/kuanza ama yule anayefanya(na hajui) kama atasoma nilichoeleza afanye utafiti wa kina juu ya biashara anayotaka kuifanya ili asije kupata hasara kabla ya kuona matunda yake!
Wafanya biashara wakubwa na wa kati wote wana siri kubwa sana, juu ya biashara zao na kamwe huwezi kuzikuta zimeanikwa hadharani, na mtu kujua kuwa wanasiri hizo basi kutamfanya atafiti zaidi ajue kuna nini ndani ya hizo biashara!
Hivyo mimi kusema hivyo tayari ni faida, kama hujiongezi ni shauri yako!

Lakini pia nilichosema kama uliona kuwa hakina msaada kwako basi na wewe ungepita kimya kimya bila kuniqoute!
Sijui akina Bilgates waliroga wakati wakuanzisha biashara ya Microsoft, au Benzos alimuona babu wakati anaanzisha Amazon.... Uwa najiuliza sana hili swali!
Ila kila sehemu ina njia zake, Tanzania tunaamini kwa babu wenzetu wanaamini katika tafiti na data. Watu kabla ya kuanzisha biashara wanatumia mamilion ya fedha kufanya utafiti na hata baada ya kuanzisha biashra. Utasikia mwaka huu Microsoft katumia dollar billion 5 kwenye utafiti, Amazon katumia dollar bilion 6 kwenye utafiti. Sisi tumetumia uzoefu kwenye utafiti hata kama mtu una biashara ya mabilion ya Tshs.
 
Asante motivation speaker , ila jifunze kua na akiba ya maneno usione wenzio vilaza
 
Asilimia kubwa ya sisi Watanzania hufanya biashara kimazoea, hatutafuti maarifa mapya ya kukuza mtaji wala mbinu za kuvutia wateja.
Utakuta mtu anafanya biashara lakini ana lugha mbovu kwa mteja, na wengine hufikia hata kumdharau mteja wakihisi hana pesa!
Huenda hata wewe uko hivyo, wateja wanaenda kupata huduma sehemu nyingine.
Ni kweli mkuu, hii inaweza kuwa ni sababu mojawapo ingawa mimi naamini zaidi katika ubunifu. Unajua baadhi ya wafanya biashara kwa kuwa labda biashara yake ipo kwenye population kubwa anakuwa akijiaminisha kuwa Hana haja ya kuprovide good custermer care. Hi imani potofu kabisa. Mteja mmoja anathamani sana. Fikiria mfano mteja uliemchukulia poa yeye kila Baada ya mwezi 1 hununua bidhaa yenye thamani ya 20000/= unayoiuza. Kwa mwaka huyu mteja atakuwa amekuingizia 240000/=. Sasa kwa wateja wawili wa Aina hii ni 480000/=.
Anyway Custumer care inalipa jamani kwa sababu huwezi jua ni mteja yupi atakuwa ni benefit kwa kiwango gani kwako.
All in all biashara pia ni ngumu maana kiukweli mtaani ni pagumu.
 
Kifupi naweza sema ni uchumi tu wa watu uliyumba na ujenzi ulipungua, maana wakati naanza nilikuwa na wateja wa kutosha tu na nikawa nafuata mzigo DSM karibia kila mwezi hiyo ilikuwa 2014/15, ila kuanzia 2016 ndipo shida ilipoanza wateja waliisha kabisa, ilifika muda nikawa nauza elf 15 kwa siku.

Alafu ni kipindi ambacho nilikuwa nimechukua mkopo wa 10m ili nipanue biashara. Ebu fikiria hizo stress zake yani dukani una mzigo wa zaidi ya 15m, alaf unapata mauzo ya siku elf 20..

Hali ilikuwa mbaya zaidi, ikabidi mzigo wote niuze kwa bei ya hasara.
Hizo nyakati hata Mimi ziliniondoa biasharani kabisa nikafunga ofisi kabisa nikarudi kitengo(ajirani)Maana huyo Farao asiyemjua Yusufu alishika nchi akaanza kusumbua Wana wa Israel na watabiri na wachambuzi wa Mambo wanasema miaka Yake 10 itakuwa ni miaka iliyoliwa na nzige,tunutu na madumadu ole wao watakaoweka mitaji yao mikubwa Biasharani katika Siku hizo.
 
Hizo nyakati hata Mimi ziliniondoa biasharani kabisa nikafunga ofisi kabisa nikarudi kitengo(ajirani)Maana huyo Farao asiyemjua Yusufu alishika nchi akaanza kusumbua Wana wa Israel na watabiri na wachambuzi wa Mambo wanasema miaka Yake 10 itakuwa ni miaka iliyoliwa na nzige na tunutu ole wao watakaoweka mitaji yao mikubwa Biasharani katika Siku hizo.
Ni muhimu sana kuomba bwana aturejeshee miaka iliyoliwa na nzige, madumadu na tunutu.
 
Tenga muda na ushukuru kwa uchache wa wateja kuja dukani hata kama hawanunui.

Kukosa shukran ni moja ya sababu ya kutopata zaidi au kuondokewa kabisa na kile kichache ulichonacho.
 
Back
Top Bottom