Kutokupata wateja kuanzia asubuhi hadi jioni baadhi ya siku

Pia mimi sikufunga....ila mwanzo ni mgumu sana as unakua huelewi...unadhani kila siku unauza tu...kuna siku huuzi hata boxer..cha msingi uvumilivu.
Biashara nzuri ni ya mwenzako,
Unaweza uwe umepakana na mwenzako anauza bidhaa tofauti na yako, ukaona Huyu mbona anauza sana,
Jidanganye ubadilishe....,
Kuna watu wanaamua kuuza kwa bei ya hasara ili mzigo umuondokee.

Kiufupi tamaa za namna hio hazifai,
Na unapofungua biashara mpya jipe mda wateja wapafahamu na kuzoea duka lako,
Ndio maana Kutouza sio sababu ya kufunga Biashara,
Kikubwa tuu wateja wawe wanakuja hata kuulizia bei na kuangalia, Ni suala la muda tuu na upepo.
 
Kabisa yaani...maana wateja walivyozoea wakaanza kuniagiza niwaletee mzigo wanaotaka wao hata kama dukani haupo...au naweza chukua mzigo nikiwalenga watu fulani kisha nawapigia simu waje kucheck...taratibu tu mambo yanakua poa hususan ukishaanza kuwa na wateja wako wakudumu lakini inachukua muda.
 
Aisee, somo kubwa hili.
 
Mkuu biashara yako ya hdw imekufanye mkuu nipe mbinu na mm nisje kuzika yangu
 
Mkp sas hijawai kwenda kwa babu
Nipo kwenye hii biashara, usemayo ni kweli na mimi yalinikuta hivyo hivyo, na baadhi ya siku yanajirudia,
Ila sikukata tamaa, kikubwa tuu mwisho wa mwezi sikosi faida baada ya malipo yote.
Ila Kiukweli kuna kipindi nilitaka nifunge.
sa hujasaas
 
Kwa Kweli mzee umeongea ukweli mtupu kuanzi Sasa HV sitoki nje ya ofc yangu na uzuri Nina tabia nzuri Sana mteja akija dukani nasimamaga nahakikisha Nampa maelezo ya kutosha na Hili la kusimam limenilipa sana
 
Kuna wateja pia wanadharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…