Kutokuwepo kwa umeme kila siku asubuhi na jioni mpaka usiku, tatizo ni nini?

Mimi naishi Mwanza ni kweli unachosema Mkuu.Jana Ilemela Umeme umekatika kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 6 usiku!!
 
Ukweli ni kwamba kukosa watu wenye maono, uwezo, ubunifu na ujuzi unaotakiwa kwenye vitengo vya umma, ni laana kubwa na iliyo dhahiri, na inaliangamiza Taifa kwa speed kubwa.

Hata kazi ya bodaboda aliyoisema Lema ni laana, ukweli ni zao la laana ya kukosa uongozi ulio bora kila eneo la ofisi za Serikali, mashirika ya umma, na taasisi nyingi za Serikali.

Kikubwa kabisa tulichokikosa kama Taifa ni UONGOZI BORA. Na ukikosa uongozi bora, hata vile vitatu vilivyobakia vinakuwa havina msaada.
 
Bodi ya TANESCO iliyojaa Bankers wakina Mchechu,Mafuru etc et al wakiongozwa na DG Maharage Chande muuza vifurushi vya Bongo movie Mstaafu wa DSTv.
Mungu aturehemu Watanzania!
 
Rushwa nia adui wa haki,na matabaka huangamiza taifa.
 
Kutokana na upungufu WA umeme kwenye Gridi.

Hii ni kwenye Grupu la wasapu la Tanesco Halmashauri Fulani hifii
 
Nashauri ukagombee urais la sivyo hata wewe ni walewale ambao hawana uchungu na nchi.
 
Mkuu sema kweli,kumuona Rais milioni 200 mpaka 400 !!!
Ndiyo maana jamaa wapo tayari Watanzania wafe Ili wao watajirike!
 
Tatizo ni akili, toka miaka ya 90 naanza kupata ufahamu umeme ni tatizo, miaka 30 mbele bado shida ni ile ile alafu tuseme tuna akili kweli?

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Naweza kukubaliana na wewe kwa kiasi fulani...!

Kwa mfano mtu anapozungumzia kuweka SMART METERS wakati umeme hauaminiki, huyu mtu atakuwa na akili za namna gani?!
 
Mkuu nimekuwa nilisikia hili neno 'tafakuri' ila Huwa silielewi. Hivi ni tafakuri au tafakari
 
Mimi Naamini TANESCO wanamhujumu SSH.
Mawazo yangu yananituma hivyo.
Kama sivyo basi mabosi wa TANESCO wanafanya biashara ya kuuza mafuta, Sola ama majenereta!
Sijui SSH bado tu hajazibaini njama hizo?
Piga chini huyo kijana,anakuhatibia sanaaa.
 
Hatari sanaa Mkuu. Naamini Watu wake wamesoma hapa. JF ni lidude kuubwaaaa mnooo
 
Haya mambo yapo kweli? Ndiyo nasoma leo. Aisei! Kumuona Mhe. Rais milioni 200? Huyo anayetoa milioni 200 ana biashara gani kuilipa hiyo pesa na kumpa faida kwa kumuona Mhe. Rais? Kama ni mwekezaji taasisi nyingine si zipo? πŸ™πŸ™πŸ™
 
Pwani siku ya pili leo ndio mchezo unaoendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…