Kila mtu anaamini uwepo WA nguvu ya asili inayoongoza ulimwengu
Nguvu hiyo ya asili ndiyo ilifanya, unafanya, na itafanya Kila kitu kiwe
Nguvu hiyo ya asili imepewa majina tofauti tofauti na wengine kuigawa ktk makundi tofauti tofauti.
Manabu zetu waliita mizimu ,na dini kutoka mashariki ya wao wakaziita Mungu.
Duniani hayupo asiyeamini juu ya uwepo huu, isipokuwa tunawaita wapagani wale tu wasiomini tunachokiamini Kwa kuwa nasi ni pagans Kwa kile tusichokiamini kuhusu wao.
Nguvu hii ya asili ndiyo imetawala mifumo mizima ya maisha yetu na shughuri zetu,
Ni ngumu sana kupata majibu sahihi ukiuliza kama Mungu yupo au la?
Kwanza ni Mungu yupi, wako au wangu , naweza kusema duniani hakuna Mungu mwingine isipokuwa wangu. Kwakuwa ndiye najua ni nguvu ipi naiamini kuwa ndiyo nguvu inayofanya Kila kitu kiwe.
Kwa hiyo Mungu WA kweli yule unaeamini wewe yupo, sio unaeminishwa yupo, kama utaamini kwenye mizimu, basi misingi na Sheria za maisha yako zipo huko, vile vile Kwa dini zingine.
Linapokuja swala la uumbaji ndipo unakuja ubishano Mungu ni nani, na tuna miungu wangapi, India Wana Mungu wao, china Wana Mungu wao wakristo na waisilamu hivyo hivyo. Sasa swali ni Kwa kwamba licha ya kuwa na miungu mwingi duniani n inaweza kana vipi wote wawe na creation ya binadamu inayofanana
Je, Mungu ni mmoja ila dini tofauti??
na kama hivo vipi kuhusu India Kwa wabudha na wahindu, vipi kuhusu china, vipi kuhusu ukristo na uislamu kuwa na mitume tofauti?
sasa Mungu ni yupi?
ukweli ni kwamba katika mataifa ambayo yamekuwa na dini Toka zamani ndo mataifa yenye utajiri kiliko mataifa yaliyoletewa dini(Afrika).
Mungu ni yupi?
Mungu wako utamjua tu pale ambapo huhitaji kitu chochote kile iwe fedha chakula, nyumban n.k. Kwa wengi tunatafuta miungu pale tunapokuwa na shida. Utaenda huku na huku ili upate msaada.
Je, kusingukwa na jehanamu, wangapi wangeamini Mungu yupo (Afrika)
je kusingekuwa na taabu, njaa, magonjwa, na vifo wangapi mngemjua Mungu?
sasa kama mmemjua Mungu kupitia shida, Mungu wenu ni yupi?
(.....)