mpndz
Member
- Sep 28, 2011
- 80
- 46
Ni ujingaHabarini wakuu,
Unajua Dunia imejaa mengi sana, yakustaajabisha na kusikitisha pia. Binafsi nilikuwa nahitaji kujua hivi mtu au watu wasioamini uwepo wa MUNGU huwaga wapo serious au ni jokes tu?
Kuna mda hadi naogopa, ujasiri wa kukataa hakuna Mungu huwa mtu unautoa wapi?
Je, vipi kuhusiana na Miujiza na athari ya nguvu yake katika maisha yako ya kila siku, mfano mambo ya riziki, maradhi, uhai, kifo etc?
Kuna vitu vya kuviletea UTANI ila sio uwepo wa MUNGU, Kama hauamini uwepo wake basi ni vyema kuwa silent ila sio KUPOTOSHA yakuwa hayupo.
Hivi ujasiri wa kusema MUNGU hayupo mtu unakuwa nao vipi au sisi wengine TUNAE MUAMINI ni waoga?
Na mtu yeyote anaweza kuwa mjinga katika jambo fulani na si kosa!
Tatizo litakuja pale 'mjinga' huyo atakapo elimishwa na akakaendelea na msimamo wake na matokeo yake atakuwa 'mpumbavu'