Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Umejibu swali Moja tu kati ya niliyokuuliza. Naomba na majibu ya mengine tafadhali.

Umetoa dalili za kuwepo Kwa mwenyezi mungu na umetumia Quran kama rejea. Kama Quran tutaitumia kama ushahidi lazima tuwe na uhakika ni kitabu kinachotoa ukweli. Lakini tukisoma Quran kuna vitu ambavyo ni wazi si vya kweli. Mifano hii hapa chini

1. Jua halizami kwenye matope

Quran-18:86: Till, when he (the traveler Zul-qarnain) reached the setting-place of the Sun, he found it going down into a muddy spring…
Quran- 18:90: Till, when he reached the rising-place of the Sun, he found it rising on a people for whom We had appointed no shelter from it.

2. Allah alikuwa anahisi dunia Iko flat kama carpet na milima ipo kuifanya dunia isitisikike (hii science aisee sidhani kama ni kiumbe kinachoelewa physical geography vizuri)

Quran-15:19: And the earth We have spread out (like a carpet); set thereon mountains firm and immovable;
Quran-78: 6-7: Have We not made the earth as a wide expanse, And the mountains as pegs (anchor)?

3. Maziwa ya n'gombe hayatoki kwenye matumbo, mammary glands zinazoleta maziwa ziko mbali na sehemu ambayo Quran inasema maziwa yanatokea. Pia hayo maziwa sio "pure" kama ambavyo Quran inasema Kuna bacteria wakutosha tu ndo maana Kuna kitu tunaita "pasteurization" kwa ajili ya kuyasafisha.

Quran -16:66 :Surely there is a lesson for you in the cattle: We provide you to drink out of that which is in their bellies between the faeces and the blood - pure milk - which is a palatable drink for those who take it.

Chanzo chako cha taarifa kina makosa ya kisayansi, kihistoria. Mungu anaejua kila kitu hawezi kufanya makosa ya hivi, hasa kukosea taarifa kuhusu uumbaji wake mwenyewe. Hii ni dalili wazi kwamba mwandishi wa Quran alikuwa hafahamu science vizuri ukizingatia na wakati alioishi duniani ni zamani sana maendeleo ya science yalikuwa bado. Hii ni wazi hicho kitabu hakijatoka Kwa kiumbe kinachojua kila kitu bali mwanadamu kama sisi na hakiwezi kuwa ushahidi wa uwepo wa mungu.

Turejee kwenye point zako

1. Kuna makosa kuhusu umbile la mbingu na ardhi kwenye Quran (mungu atakoseaje uumbaji wake) hii ni dalili maelezo hayo ya uumbaji ni hadithi tu.

2. Mfano kwenye hii kauli

"Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;
Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima"

Ili uweze kutengeneza kitu lazima uwezo wako wa akili uwe mkubwa kuliko unachotaka kutengeneza. Kama mungu aliumba hii miili yetu na akili zetu tulizonazo (mashine za ajabu kama ulivyosema) maana ake mungu mwenyewe ni mashine ya ajabu yenye uwezo mkubwa kiakili zaidi ya binadamu . Kwa maana hii hata yeye atahitaji mjuzi mwingine wa kumtengeneza hawezi akawa alijileta tu. Hapa lazima sasa utueleze alitengenezwa na nani.

3. Historia ya mwanadamu

Mfano tu nikujulishe leo waisraeli hawajawahi kuwa watumwa misri hakuna ushahidi hata chembe wa kihistoria. Hivyo kuhusu kuangamizwa firauni hadithi tu na ukitaka kuniamini neno Firauni (Pharaoh) lina maana tu ya mfalme Ma Firauni wote walikuwa na majina na historia zao zinafahamika ni Firauni yupi kati ya hawa aliengamizwa (Narmer, Khufu, Hatshepsut, Ramses, Akhenaten, Thutmose) Quran haijatuambia maana mwandishi alihisi pharaoh ni mtu mmoja na hilo ndo jina lake.

4. Kuhusu mitume

Kuna mitume kama Abraham, Moses ambao pembeni na baadhi ya vitabu vya dini hawana ushahidi wowote wa kuwahi kuwepo duniani. Mfano hadithi ya Nuhu inapatikana kwenye hadithi za zamani kabla hata vitabu vya dini ikiwemo biblia na Quran kuandikwa. Utofauti ni kwamba kwenye hizo hadithi za gharika jina la mhusika mkuu sio Nuhu (Soma Epic of Gilgamesh).

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Mkuu nimekuelewa kwanza hongera kwa kuja na hoja zilizo shiba mifano, ila kwa utakacho wewe ni ushahidi ulio hai(Wakuona, wakugusa na kushikika) kitu ambacho ni kigumu.

Waliokapatiwa bahati za kuonesha haya tayari walishapita (Wajumbe wa MUNGU) ambao ndo walikuwa na access uzitakazo, mim n mtu wa kawaida sana kama ulivyo wewe ila tofauti zetu ni IMANI.

Kwa ulimwengu wa leo na toka enzi imani ni kuamini ama kwa kuona, kusoma au kusikia ila kwenye evidence kuna masalia ya mifano yake kama uwepo wa FARAO, Mke wa Nuhu aliyegeuka jiwe la chumvi, Qur'an, Torat, Zaburi, Injil na vitabu vingine.

Ila ukitaka USHAHIDI UUTAKAO, kwakweli mimi ntashindwa kukupa, coz MUNGU hakunipa hyo ACCESS.
 
Hapo huoni kuna tatizo mkuu yani Mungu alilidhihirisha kwa kikundi Cha watu fulani tu ndani ya muda fulani hadi kwa mtume wake wa mwisho (Muhammad) halafu hajaonekana tena. Aliacha maandiko ambayo tafsiri zake zinachanganya watu. Na pia alitoa maagizo tofauti kwa watu mbalimbali kitu ambacho kimepelekea dini tofauti bila kujua ipi ni sahihi. Lakini mwisho wa siku ataadhibu watu kwa kutofata maandiko, dini sahihi na kutilia mashaka uwepo wake hii ni haki kweli ?

Kama yupo ni swala dogo tu la kujidhihirisha kwa wasioamini na waliopotea kwenye dini ya kweli na kusema dini sahihi ni ipi lakini yuko kimya. Mfano kwenye biblia aliwaaminisha manabii wa "baali" kuwa yeye ni mungu wa kweli kwa kushusha moto, kuna vilema waliponywa na yesu. Hizi ishara kwanini hatuzioni sasa?

Waandishi wa vitabu vilivyopo ambavyo unasema ndio ushahidi ni wanadamu kama sisi, tunajuaje walikuwa wanaongea na mungu kweli? lakini pia tunajuaje walikuwa hawaongei na Mungu? swali la pili rahisi sana wanadai kuongea na kiumbe kinachojua kila kitu lakini maandiko yao yamejaa makosa hii ni wazi hawaongei na kiumbe cha hivyo ni wao wenyewe na wanaandika makosa kama wanadamu wengine tu.

Uwepo wa masalia ya miili ya wafalme wa misri (ma Farao) ni ushahidi tu kwamba watu wa misri walikuwa na njia za kutunza miili ya watu kwa muda mrefu bila kuoza (inaitwa mummification) na sio ushahidi wa kutosha wa matukio yaliyoandikwa kuhusu misri kuitumikisha israeli. waandishi wa vitabu vya dini fulani walijua hii njia ya kutunza miili ya wafalme wa misri wakadai Farao (kwanza walihisi Farao ni jina la mtu na ni mmoja) hakuoza kwasababu mungu alitaka kumuadhibu kitu ambacho ni hadithi tu, vipi sasa miili mingine ambayo sio wa Farao iliyotunzwa kama wa Farao na masalia yapo wao pia walimuudhi Mungu?

MAANDIKO SIO USHAHIDI. KILICHOFANYIKA NI KUCHOMEKA CHEMBE CHEMBE KIDOGO ZA UKWELI KWENYE HADITHI ZA KUFIKIRIKA. NDO MAANA MIUJIZA ILIYOANDIKWA KAMA WATU KUFUFUKA, VILEMA KUTEMBEA KWA KUOMBEWA HATUIONI SABABU NI VITU VISIVYOKUWEPO KWENYE UHALISIA.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Yuko wapi sasa kama hajajificha?
Malizia kujibu swali.

Mola wetu yupo juu ya mbingu ya saba, amestawi juu ya Arshi yake.

Siku ya malipo, wale walio fanya wema watalipwa ziada ya kukuona Mola wetu, kama vile tuonavyo jua la saa sita mchana. Hizi ni habari zisizo na shaka kabisa.
Unafikiri kunipa uhai kutakuwa ni jambo la msingi kama uhai huo alionipa sita enjoy nao kwa shida za ulimwengu alizoziweka?
Ukiona sio jambo la msingi jiue, hakuna huzuni inayo dumu kijana.

Kila kitu kina sababu zake.
Si tuna ona kwa wanao omba na hakuna respond yeyote kutoka kwake
Hili ndio huwa tatizo la watu kama nyinyi, yaani kila mnapo mjadili Mola, lazima mkosee sababu hamumjui.

Mola anampa mtu kile anachostahiki, na unaweza kuombwa hili ukapewa bora lililo zaidi na ukanyimwa lile ulilo omba. Unaweza kuombwa mali ukapewa afya njema.

Mtu kama wewe huwezi kuona utendaji kazi wa Mola sababu hamjui.
Kwanini ameruhusu?
Sababu ziko nyingi miongoni mwazo ni kuwazindua waja wajue lengo la wao kuishi hapa duniani, kadhalika ni adhabu.
Kama hakumbushwi basi kupiga dua kwa ajili ya kuomba lolote kutoka kwake ni kupoteza muda tu
Si kupotezwa muda sababu yeye ameelekeza ya kuwa na ukitaka msaada basi muombe yeye, na yeye anapenda kuombwa na ni mwepesi wa kujibu maombi ya waja.

Sasa vipi inakuwa kupoteza muda wakati watu wanajibiwa Dua zao kila uchwao ?
 
Hapo huoni kuna tatizo mkuu yani Mungu alilidhihirisha kwa kikundi Cha watu fulani tu ndani ya muda fulani hadi kwa mtume wake wa mwisho (Muhammad) halafu hajaonekana tena. Aliacha maandiko ambayo tafsiri zake zinachanganya watu. Na pia alitoa maagizo tofauti kwa watu mbalimbali kitu ambacho kimepelekea dini tofauti bila kujua ipi ni sahihi. Lakini mwisho wa siku ataadhibu watu kwa kutofata maandiko, dini sahihi na kutilia mashaka uwepo wake hii ni haki kweli ?

Kama yupo ni swala dogo tu la kujidhihirisha kwa wasioamini na waliopotea kwenye dini ya kweli na kusema dini sahihi ni ipi lakini yuko kimya. Mfano kwenye biblia aliwaaminisha manabii wa "baali" kuwa yeye ni mungu wa kweli kwa kushusha moto, kuna vilema waliponywa na yesu. Hizi ishara kwanini hatuzioni sasa?

Waandishi wa vitabu vilivyopo ambavyo unasema ndio ushahidi ni wanadamu kama sisi, tunajuaje walikuwa wanaongea na mungu kweli? lakini pia tunajuaje walikuwa hawaongei na Mungu? swali la pili rahisi sana wanadai kuongea na kiumbe kinachojua kila kitu lakini maandiko yao yamejaa makosa hii ni wazi hawaongei na kiumbe cha hivyo ni wao wenyewe na wanaandika makosa kama wanadamu wengine tu.

Uwepo wa masalia ya miili ya wafalme wa misri (ma Farao) ni ushahidi tu kwamba watu wa misri walikuwa na njia za kutunza miili ya watu kwa muda mrefu bila kuoza (inaitwa mummification) na sio ushahidi wa kutosha wa matukio yaliyoandikwa kuhusu misri kuitumikisha israeli. waandishi wa vitabu vya dini fulani walijua hii njia ya kutunza miili ya wafalme wa misri wakadai Farao (kwanza walihisi Farao ni jina la mtu na ni mmoja) hakuoza kwasababu mungu alitaka kumuadhibu kitu ambacho ni hadithi tu, vipi sasa miili mingine ambayo sio wa Farao iliyotunzwa kama wa Farao na masalia yapo wao pia walimuudhi Mungu?

MAANDIKO SIO USHAHIDI. KILICHOFANYIKA NI KUCHOMEKA CHEMBE CHEMBE KIDOGO ZA UKWELI KWENYE HADITHI ZA KUFIKIRIKA. NDO MAANA MIUJIZA ILIYOANDIKWA KAMA WATU KUFUFUKA, VILEMA KUTEMBEA KWA KUOMBEWA HATUIONI SABABU NI VITU VISIVYOKUWEPO KWENYE UHALISIA.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Well, twende side B ili tutumie formula ya attack from Beginning kujibu hoja yako.

Unaamini uwepo wa Lucifer na kazi zake ??
 
Anashughuli gani ya maana inayo muweka huko?
Nafkiri ungeanza kwanza kutaja shughuli yako ya maana inayokufanya ukae huku duniani, alafu nikujibu kinachomfanya MUNGU akae hko alipo.
 
Siku ya malipo, wale walio fanya wema watalipwa ziada ya kukuona Mola wetu, kama vile tuonavyo jua la saa sita mchana. Hizi ni habari zisizo na shaka kabisa.
Okay na yeye kwa kuumna ulimwengu mbovu unaosababisha watu wasiokuwa na hatia wafe, siku ya malipo naye atawajibika kwa uzembe huo?

Au kuna double standard?
 
Okay na yeye kwa kuumna ulimwengu mbovu unaosababisha watu wasiokuwa na hatia wafe, siku ya malipo naye atawajibika kwa uzembe huo?

Au kuna double standard?
Atawajibishwa na nani, au umoja wa MATAIFA ??
 
Back
Top Bottom