Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Kutomuamini Mungu ni ujasiri?

Basi usahihi ni kuwa ni jambo la msingi. Thibitisha wapi Mungu hakuwasaidia wakati anawapa uhai na mengine yote, kingine usichokijua hata wewe unaweza usiwepo na hao wanao kutegemea wakaishi tena wakaishi maishi mazuri kuliko Sasa, sababu Allah ndio mpangaji na muendesha mambo.
Kwani ni watoyo wangapi wamezaliwa na wakafa siku hiyo hiyo?

Kwanini asiwasaidie hao kwanza?

Wengine wanafia tumboni hata fursa ya kuiona dunia hawaipati, huyo Mungu anakuwa wapi wakati hayo yanafanyika?
 
Weka mfano halisi mfano ulio utoa ni mfano mfu.
Mfano mfu?

Kwani haya mabaya ya huu ulimwengu yapo kwa bahati mbaya au kwa makusudi?

Je "mabaya" ni mabaya kiasi iwe kosa endapo itabainika kuwa kuna mabaya?

Au mabaya sio jambo baya hivyo ni jambo zuri na tunapaswa kufurahi tunapoyaona?

Kama mabaya ni mabaya in any sort basi msababishi wa kwanza wa mabaya ndio "Mbaya"

Sasa binadamu hawezi kuingizwa kwenye hii lawama kwasababu yeye sio chanzo cha ubaya.

Mungu aliyeumba huu ulimwengu wenye kuruhusu mabaya kwa lengo la kuwatahini watu wake, ndio mbaya.

Ukisema Mungu hawezi kuwa mbaya licha ya kwamba yeye kuumba ulimwengu wenye kuruhusu mabaya basi hapo hapo tutakubaliana kuwa binadamu anayefanya ubaya uliokuwa sehemu ya asili yake hawezi kulaumiwa kivyovyote.
 
Kutoamini Mungu ni ujasiri wa kijinga, tuchukulie mfano tu wa kiakili wa kibinadamu, mwanadamu anapozaliwa ni kiumbe dhaifu sana lakini anakuwa amekingwa vizuri toka mimba yake inapoingia katika mwili wa mama yake, anazaliwa amepangika vizuri mwili wake, ana mwili wenye kichwa, kifua, tumbo, mikono na miguu, kichwa chenye nywele macho, pua mdomo na masikio, mikono yenye vidole na miguu yenye vidole kamili, kutokana na udhaifu wake anahitaji usaidizi wa wazazi wake kwa kipindi chote anapokuwa hana uwezo wa kujihudumia kutokana na mwili wake hauna nguvu za kujimudu na pia akili yake haiwezi kutambua vizuri kwa kuwa haijapevuka katika kung'amua zuri na baya. Anazoeshwa kusema na kupewa maarifa mbalimbali ambayo yatakuyomuezesha kuishi kwa usalama wake na wa wengine pamoja na mazingira yake na kuweza kujikimu ili apate naye kuwa binadamu bora atakayeweza kuendeleza mazuri atakayofunzwa na kukemea maovu atakayojifunza na kuongeza binadamu wengine kwa njia sahihi iliyokubaliwa na jamii husika, mwishowe uhai wake unakwisha bila ya yeye kujua lini ataumaliza uhai huo. Huu ni mfano mdogo sana wa kujua kuwa kuna nguvu inayoyafanya haya yote yatendeke, je ni nani ambaye anayeyafanya haya yote yafanyike? Na tunajua kuwa kuna mambo mengine yanatokea kinyume na nidhamu tuliyoizoea. Hivi haya yote yanatokea kwa bahati mbaya?
Ndiyo maana akili iliyo salama inatambua kuwa kuna Muumba wa viumbe na mwenye kuendesha mambo ya ulimwengu wetu huu yupo. Watu wengi wenye kupinga uwepo wa Mungu ni wahanga wa kukumbwa na matatizo ambayo walikosa suluhisho baada ya kumuomba Mungu na kutotatuliwa shida zao, au kuona watu wanawaomba miungu tofauti tofauti na wengine kujiona Mungu wao ndiyo wa kweli na mwenye nguvu kuliko miungu mingine, hivyo kufanya watu wengine waone kuwa swala la Mungu ni lenye mgongano. Lakini GT ni yule atakayedadisi hiyo miungu je kweli wana sifa za kuwa uwezo mkuu wenye kuweza na usiyowezwa? Kwani sayansi haipingi uwepo wa Mungu bali inapinga aina ya miungu.
Unalazimisha Mungu awepo tu, hyo ni hypothesis tu kwenye mambo ya asili usiyoyaelewa.

Wewe umeyatungia hadithi na unayaforce yawe kweli.

Tunaprove vipi hiyo hypothesis yako ili tuthibitishe pasina shaka!?

Unaweza thibitisha Mungu yupo!?
 
Mola alipo tuumba akatupa uhuru, tukipenda tumshukuru na tukiamua tukufuru, huo uhuru uko nao wewe pia.
Unaelewa mantiki ya uhuru haiambatani na adhabu?

Unampa mtoto uhuru wa kuchagua kula Biriani au Pizza, huo ndio uhuru.

Kumuambia mwanamke unaye mtongoza achague kati ya kukupenda wewe au kutokupenda halafu ukasema akichagua kutokupenda wewe utamuua. Huo sio uhuru wa kuchagua

Hiyo ni amri.

Sasa Mungu anasema amekupa uhuru wa kuchagua mema na mabaya, ukichagua mabaya unaenda motoni kuchomwa milele.

Huo sio uhuru hiyo ni amri yenye kitisho.

Ameweka kitisho kilichowalazimisha watu wawe wanafki wafanye anayotaka ilimradi tu wasichomwe moto.
 
Swali zuri, kwa kawaida matatizo kama maradhi ni sehemu ya ibada kwa mwanadamu kwa maana n moja ya kipimo cha imani ya mwanadamu kwa MOLA wake mlezi.

Hence, matatizo humrejesha mwanadamu kuongeza unyenyekevu kwa mola wake ili kupata msaada juu ya yamkabiliyo.
How matatizo (mabaya) ni moja ya kipimo cha imani ya mwanadamu!?

Kwanini kuamini kumefanywa kuwa muhimu sana kuliko kujua!?
 
Kwa maana hiyo unataka kusema kwamba kwa kuwa kuna matatizo duniani basi maana ake lazima kuna Mungu anatupima imani ili tumkumbuke si ndio?

Kwa maana hiyo nikikutana na matatizo kwenye maisha yangu ni Mungu tu ananipima imani sasa vipi kuhusu matatizo ya kujitakia kama vile mtu kushindwa kulipa ada za watoto kwasababu ya kutumia mshahara kulewa pombe na kufanyia starehe zilizopitiliza na hii pia ni kipimo cha imani?

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Mungu mjuzi wa yote anapimaje imani ya mtu!?

Au Mungu wao hajui yote?
 
Allah anajua hata kile ambacho hakipo kikiwepo kingekuwaje.

Ana njia nyingi za kuwazindua watu bali hata angetaka wote tumuamini angefanya hivyo, ila ameweka utaratibu huu ili tufikie lengo la kuwepo duniani.
Wakati anafanya hivyo, lengo lake si lilikuwa kuufanya ulimwengu uwe bora?

Sasa kama aliweza kuona yatayojiri kabla hayajatokea maana yake aliona imperfections zote.

Na alikuwa na uwezo wa kubadili au kuboresha kuondoa hizo imperfections lakini akaziacha.

Maana yake huu ulimwengu wenye njaa, masunami, vimbunga, matetemeko, magonjwa, yanayoua mamilioni ya watu ikiwemo watoto wadogo wasiojua baya na zuri.

Kwa Mungu huu ndio ulikuwa ulimwengu bora kwake wakati anachagua aina gani ya ulimwengu bora kwa ajili ya viumbe wake anaosema anawapenda kwa upendo wote.

Kwa maana hiyo sasa ndio tunarudi kwenye hoja yangu kuwa ni Mungu anayetengeneza ugonjwa kisha anataka umlilie ili akupe dawa.

Halafu ukipona uanze kumsifia kuwa anakujali wakati kiuhalisia yeye ndiye aliyekutengenezea tatizo.

So Mungu huyu ana inferiority haamini kwenye kupendwa bila kutengeneza drama, haamini kuwa anaweza kusifiwa bila kutengeneza tatizo ili umrejee kumlilia.

Ni Mungu wakijinga anayependa sifa za kishamba.
 
Dalili Za Kuwepo Mwenyezi Mungu (S.W).

Dalili nyingi zimedhihirishwa ndani ya Qur’an katika maeneo makuu matano ambamo uchunguzi wa kina na kutafakari vikifanyika vilivyo mtu atayakinisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pasina shaka yeyote. Maeneo hayo ni haya yafuatayo;

1.Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.

2.Nafsi (Dhati) ya mwanaadamu.

3.Historia ya mwanaadamu.

4.Maisha ya mitume.

5.Mafundisho ya mitume.

1.Umbile la Mbingu na Ardhi na Vyote Vilivyomo.

Maumbile mbali mbali kama vile udongo, milima, mabonde, maji, mimea, wanyama, jua, mwezi, nyota, n.k ambavyo ni ishara kubwa inayoonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w). Ishara hizo ni hizi zifuatazo;


(a) Umbile la Mbingu na Ardhi;

Tukichunguza maumbile mbali mbali ya dunia na sayari zote jinsi yalivyoundwa na kupangika kwa namna iliyo maalum kama vile jua, mwezi, nyota, n.k ni ishara tosha kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (41:9-12), (7:54), (32:4-5), (70:4), (21:30), (46:33) na (79:30).



(b) Jua, Mwezi na Nyota;
Kuwepo kwa mfumo wa ajabu uliopangika wa Jua, mwezi na Nyota na kila kimoja kina njia yake pasina kutokea mgongano au mvurugano wa aina yeyote kati yao ni ishara kubwa za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (6:96), (7:54), (2:29), (10:5), (14:33), n.k.



(c) Usiku, Mchana, Mwanga na Giza;
Kupatikana na kubadilishana kwa usiku na mchana, mwanga na giza ni ishara tosha za kuthibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wenye akili.
Rejea Qur’an (2:164), (3:190), (17:12) na (28:71-72).



(d) Bahari, Maziwa na Mito;
Wingi wa maji yasiyo na mfano, kutofautiana ladha yake, na kutengana kati ya maji matamu na chumvi bila ya kizuizi chochote na pia vyombo vizito na vikubwa kupita juu yake bila kuzama ni dalili nyingine ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (25:53), (2:264), (10:22), (14:32), (16:14), (17:66), (22:65) na (53:12).



(e) Milima na Mabonde;
Milima, majabali na mabonde ambavyo vinaifanya ardhi iwe madhubuti na isiyumbe wakati wa mitetemeko na mzunguko kati ya jua, mwezi na nyota ni ishara kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (21:31), (13:3), (15:9), (16:15), (27:61), (31:10), (50:7), (77:27), (35:27), (78:7) na (88:19).



(f)Upepo, Mawingu, Mvua, Radi na Ngurumo;
Upepo, mawingu, radi, ngurumo na mvua ni vitu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa ajabu unaopelekea mvua kunyesha sehemu inayohitajika. Vyote hivi ni dalili tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (10:22), (13:17), (2:19-20), (2:164) na (25:48).



(g)Matunda, Mimea na Vyakula (Riziki);
Mimea na matunda mbali mbali hustawi katika aina tofauti za udongo na kutoa mazao ambayo ni riziki (chakula) kwa viumbe hai na kila kimoja kinategemea kingine katika kustawi kwake. Hii ni ishara kwa wenye akili.
Rejea Qur’an (67:21), (11:6), (29:60), (6:95,99) na (13:4).



(h)Wanyama, Ndege na Wadudu;
Viumbe vyote hivi kutokana na kutembea, kuruka kwao na kupata kwao riziki bila ya wao kujipikia na kumiliki rasilimali yeyote, bado wanaishi bila shida yeyote. Hii ni kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye pekee anayewaruzuku.
Rejea Qur’an (16:5-7), (16:79) na (3:190-191).



2.Nafsi (Dhati) ya Mwanaadamu.
Kutokana na nafsi ya mwanaadamu mwenyewe tukichunguza na kutafakari kwa makini kuna ishara nyingi zinazoonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kama ifuatavyo;



(a) Asili, Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu;
Uhai, hatua alizopitia na mfumo wa maisha ya mwanaadamu, vipi na lini alianza atamaliza kuishi, nini sababu ya kifo chake na kitatokea wapi na nani anayedhibiti maisha yake yote ya kila siku, tunadhibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (2:28), (30:20-21), (22:5), (75:36-40), (23:14) na (56:81-87).



(b) Mwanaadamu kutofautiana na Wanyama;
Wanaadamu kutofautiana na wanyama kimaumbile na kimalengo, ambapo lengo la mwanaadamu ni kuwa Khalifah, na wanyama ni kumtumikia mwanaadamu. Mwanaadamu amepewa akili, uhuru, vipawa na utambuzi kinyume na wanyama.
Rejea Qur’an (2:29-30), (15:28-29), (95:4) na (16:78).

c) Kuumbwa wanaume na wanawake na kuwa na mapenzi baina yao;
Asili ya wanaadamu wote ni moja, lakini wanatofautiana kimaumbile, kihisia na kisaikolojia. Hii ni kwa ajili ya kutegemeana, kuhurumiana na kuvumiliana kimahitaji kati yao kimwili na kisaikolojia. Zote hizi ni ishara tosha za kuwepo Allah (s.w).

d) Mwanaadamu kutofautiana lugha, rangi, kabila na taifa;
Pamoja na wanaadamu kufanana katika viungo mbali mbali vya miili yao kama ulimi, mdomo, koromeo, n.k lakini wanazungumza lugha tofauti bila ya kufunzwa na mtu yeyote. Hii ni kuwa utofauti wao ni kwa ajili ya kujuana tu, na hii ni dalili tosha.
Rejea Qur’an (30:22) na(49:13).

e) Kutofautiana vipaji na riziki na mgawanyo wake miongoni mwa wanaadamu;
Vipaji vya wanadamu vimetofautiana mmoja na mwingine kama vile udaktari, uhandisi, ualimu, n.k. pia upatikanaji wa riziki miongoni mwao ambao hautegemei ujanja, fani au ujuzi wa mtu bali mgao maalum ili waweze kutegemeana.
Rejea Qur’an (80:24-32).

f) Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;
Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima.
Rejea Qur’an (30:30).

g) Usingizi, Umbo, sura na vazi la mwanaadamu;
Umbo au sura aliyonayo mwanadamu hana uwezo wa kuibadilisha na anaridhika nayo. Tofauti na wanyama wanaadamu wana mavazi ya kujisitiri uchi na kujikinga na baridi na pia kupata usingizi pasina yeye kutaka au kujua chanzo na mwisho wake.
Rejea Qur’an (7:26), (82:6-8), (95:4) na (45:4).

h) Mwanaadamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) wakati wa matatizo;
Wakati wa matatizo mwanaadamu ni mwepesi sana kurejea na kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) na kuhitajia msaada wake, hata wale wanaokana kuwepo kwake wanakiri uwepo wake bila ujanja. Hizi zote ni ishara za kuwepo kwake.
Rejea Qur’an (6:63) na (10:90).

3.Historia ya Maisha ya Mwanaadamu.

Mchakato wa maisha na historia ya mwanaadamu tangu zama za kale hadi zama hizi umeambatana na matukio makubwa yaliyovunja na kusambaratisha falme na dola mbali mbali zilizotikisha dunia vita na majeshi. Yafuatayo ni baadhi tu ya matukio hayo;

a) Kuangamizwa watu wa (kaumu ya) Lut, Thamud, Ad na Firauni;
Pamoja na nguvu kubwa za kijeshi na ulinzi imara waliokuwa nao watu hawa, haikuwa chochote ilipofika muda wa kuangamizwa kwao. Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zisizokifani aliwafutilia mbali kwa kutumia majeshi yake ya upepo, maji, n.k.
Rejea Qur’an (89:6-13), (30:9), (20:128) na (22:45-46).

b) Kuangamizwa kwa jeshi la Abraha, Gavana wa Yemen;
Abraha aliandaa jeshi kubwa la askari na tembo waliofunzwa barabara kwa ajili ya kwenda kuibomoa Al-Ka’abah (Nyumba Tukufu ya Makka), lakini alisambaratishwa na jeshi dogo na dhaifu kabisa la ndege, na hatimaye ikawa ndio mwisho wao.
Rejea Qur’an (105:1-5).

(c) Kufutika na kutoweka Viongozi na Wafalme maarufu Duniani;
Viongozi na wafalme wengi waliowahi kuitawala na kuitikisa dunia na kusababisa uharibifu, mauaji, kutokana nguvu kubwa ya kijeshi waliokuwa nayo na hata wengine kufanywa miungu. Mfano akina Hitler, Mussolini na wengineo ambao mwisho wao walifutika duniani na kushindwa kujinusuru pamoja na majeshi yao.
Rejea Qur’an (56:81-87) na (67:20).


4.Maisha ya Mitume;

Kwa kuzingatia maisha ya mitume hasa waliobainisha nadni ya Qur’an, jinsi walivyofikisha ujumbe kwa watu wao kinadharia na kimatendo ni ishara tosha juu ya uwepo wa Allah (s.w). Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo;

(a) Kuwepo na kujieleza kwao kwa watu wao kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w);
Mitume wote walithibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w), na vile vile wote walitoa dai lilelile la kuwa wao ni mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) ijapokuwa walikuja nyakati na sehemu tofauti.
Rejea Qur’an (7:59-61), (7:65-67), (16:36), (40:78) na (35:24).

b) Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na mazingira ya jamii;
Mitume wengi walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili, kishirikina na kuabudu masanamu, lakini na walikuwa na mienendo na tabia nzuri isiyo kuwa na mfano katika jamii husika. Hii ni ishara kuwa yupo Mlezi na Mjuzi, naye ni Allah (s.w).
Rejea Qur’an (57:25).

(c) Miujiza kuthibitisha utume wao;
Mitume walikuja na miujiza tofauti tofauti ya kuthibitisha utume wao kwa watu wao. Kila mtume alikuja na miujiza kutoka kwa Allah (s.w) kama ishara ya kufikisha ujumbe kwa watu wake iliyokuwa tofauti na uchawi, viini macho na mazingaumbwe.
Rejea Qur’an (57:25), (28:29-32), (5:110), (15:9) na (4:82).

d) Kuhimili na kujitoa kwao muhanga;
Mitume walikuwa wavumilivu na wenye subira dhidi ya mateso, kupigwa, kufungwa gerezani, kutiwa kizuizini au kuuawa na kupata madhila, lakini hawa kukata tama na kufikisha ujumbe wao. Hii ni yupo alikuwa anawaliwaza, naye ni Allah (s.w).
Rejea Qur’an (3:21), (3:181), (4:157-158), (21:69) na (59:8).

e) Ujasiri wa mitume mbele ya viongozi na jamii za kishirikina;
Pamoja na vitisho na viburi vya wafalme na watawala wa kishirikina, mitume hawakumchelea mtu yeyote katika kumfikishia ujumbe wao. Hii ni ishara kuwa Mwenyezi Mungu ndiye waliokuwa wanamtegemea.
Rejea Qur’an (19:42-46) na (21:57-67).

(f) Ushindi wa mitume dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w);
Mitume na wafuasi wao walikuwa wachache, dhaifu na wanyonge mbele ya maadui wa Allah (s.w) waliokuwa wengi na wenye nguvu, lakini katika mapambano mitume na wafuasi wao ndio waliopata ushindi kwa msaada kutoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (71:25), (7:72), (26:60-68) na (8:9-10).



(g) Mitume kutohitaji malipo kutoka kwa watu wao;
Mitume walifanya kazi ngumu na nzito bila ya kuhitajia malipo yeyote kutoka kwa watu wao kinyume na viongozi wengi ambao huhitajia malipo kwa jamii zao. Mitume walikuwa na uhakika wa kupata ujira tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.
Rejea Qur’an (26:127).

5.Mafundisho ya Mitume.
Hili ni eneo jingine linaloonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) katika vipengele vifuatavyo;

(A) Umoja wa ujumbe wa mitume;
Mitume walitumwa sehemu na nyakati tofauti lakini ujumbe wao ulifanana, kila mtume alifundisha Tawhiid, lengo la kuumbwa kwao, kuwahofisha na adhabu na kuwabashiria malipo mema pia. Hii ni kuwa ujumbe wao ulitoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (7:59, 65, 73, 85, 158), (16:36) na (19:36).



(B) Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira;
Mitume karibu wote walitokea katika jamii za kishirikina na kijahili, lakini kamwe hawakuwahi kuchanganya mafundisho yao na utamaduni wa kijahili hata kama jamii nzima ilisimama dhidi yao.
Rejea Qur’an (109:1-6).

C) Upeo wa Elimu waliokuwa nayo Mitume;
Mitume walikuwa na upeo, fikra na hekima ya hali juu katika kutatua na kuendea mambo kuliko mtu yeyote katika jamii zao, japokuwa hawakupitia vyuo au taasisi zozote za elimu. Hii ni dalili kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliyewafunza.
Rejea Qur’an (34:10-12), (27:15-19), (43:2-3) na (25:53).
Kwamba Allah aliweka milima ili kuweka stability dunia isiyumbishwe!?

Yani mtu anakwambia kwamba nyota ni mapambo!?

Mungu huyo hajui hata kuwa jua ni nyota then unakuja kutaka kuhadaa watu hapa waamini na unawaita wajinga wasioamini?

Kabisa Homo sapiens wa karne ya 21 unakubali mambo hayo?

Imani za kidini ni shambulio la akili
 
Umejibu swali Moja tu kati ya niliyokuuliza. Naomba na majibu ya mengine tafadhali.

Umetoa dalili za kuwepo Kwa mwenyezi mungu na umetumia Quran kama rejea. Kama Quran tutaitumia kama ushahidi lazima tuwe na uhakika ni kitabu kinachotoa ukweli. Lakini tukisoma Quran kuna vitu ambavyo ni wazi si vya kweli. Mifano hii hapa chini

1. Jua halizami kwenye matope

Quran-18:86: Till, when he (the traveler Zul-qarnain) reached the setting-place of the Sun, he found it going down into a muddy spring…
Quran- 18:90: Till, when he reached the rising-place of the Sun, he found it rising on a people for whom We had appointed no shelter from it.

2. Allah alikuwa anahisi dunia Iko flat kama carpet na milima ipo kuifanya dunia isitisikike (hii science aisee sidhani kama ni kiumbe kinachoelewa physical geography vizuri)

Quran-15:19: And the earth We have spread out (like a carpet); set thereon mountains firm and immovable;
Quran-78: 6-7: Have We not made the earth as a wide expanse, And the mountains as pegs (anchor)?

3. Maziwa ya n'gombe hayatoki kwenye matumbo, mammary glands zinazoleta maziwa ziko mbali na sehemu ambayo Quran inasema maziwa yanatokea. Pia hayo maziwa sio "pure" kama ambavyo Quran inasema Kuna bacteria wakutosha tu ndo maana Kuna kitu tunaita "pasteurization" kwa ajili ya kuyasafisha.

Quran -16:66 :Surely there is a lesson for you in the cattle: We provide you to drink out of that which is in their bellies between the faeces and the blood - pure milk - which is a palatable drink for those who take it.


Chanzo chako cha taarifa kina makosa ya kisayansi, kihistoria. Mungu anaejua kila kitu hawezi kufanya makosa ya hivi, hasa kukosea taarifa kuhusu uumbaji wake mwenyewe. Hii ni dalili wazi kwamba mwandishi wa Quran alikuwa hafahamu science vizuri ukizingatia na wakati alioishi duniani ni zamani sana maendeleo ya science yalikuwa bado. Hii ni wazi hicho kitabu hakijatoka Kwa kiumbe kinachojua kila kitu bali mwanadamu kama sisi na hakiwezi kuwa ushahidi wa uwepo wa mungu.

Turejee kwenye point zako

1. Kuna makosa kuhusu umbile la mbingu na ardhi kwenye Quran (mungu atakoseaje uumbaji wake) hii ni dalili maelezo hayo ya uumbaji ni hadithi tu.

2. Mfano kwenye hii kauli

"Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;
Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima"

Ili uweze kutengeneza kitu lazima uwezo wako wa akili uwe mkubwa kuliko unachotaka kutengeneza. Kama mungu aliumba hii miili yetu na akili zetu tulizonazo (mashine za ajabu kama ulivyosema) maana ake mungu mwenyewe ni mashine ya ajabu yenye uwezo mkubwa kiakili zaidi ya binadamu . Kwa maana hii hata yeye atahitaji mjuzi mwingine wa kumtengeneza hawezi akawa alijileta tu. Hapa lazima sasa utueleze alitengenezwa na nani.

3. Historia ya mwanadamu

Mfano tu nikujulishe leo waisraeli hawajawahi kuwa watumwa misri hakuna ushahidi hata chembe wa kihistoria. Hivyo kuhusu kuangamizwa firauni hadithi tu na ukitaka kuniamini neno Firauni (Pharaoh) lina maana tu ya mfalme Ma Firauni wote walikuwa na majina na historia zao zinafahamika ni Firauni yupi kati ya hawa aliengamizwa (Narmer, Khufu, Hatshepsut, Ramses, Akhenaten, Thutmose) Quran haijatuambia maana mwandishi alihisi pharaoh ni mtu mmoja na hilo ndo jina lake.

4. Kuhusu mitume

Kuna mitume kama Abraham, Moses ambao pembeni na baadhi ya vitabu vya dini hawana ushahidi wowote wa kuwahi kuwepo duniani. Mfano hadithi ya Nuhu inapatikana kwenye hadithi za zamani kabla hata vitabu vya dini ikiwemo biblia na Quran kuandikwa. Utofauti ni kwamba kwenye hizo hadithi za gharika jina la mhusika mkuu sio Nuhu (Soma Epic of Gilgamesh).

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Yes the epic of Gilgamesh,

Hapo unamkuta Atrahasis ndiye mhusika mkuu (Noah wa biblia)

Nakumbuka alikuwa ni Mungu wa maji anajulikana kama Enlil ndiye alimwambia Atrahasis atengeneze safina kwani anataka kukata bomba.

"Kwasababu suala la kiimani limekaa kisaikolojia zaidi, utawaskia tu waamini wakisema kuwa sisi tunafanya kazi ya shetani kupotosha ukweli"
 
Mkuu nimekuelewa kwanza hongera kwa kuja na hoja zilizo shiba mifano, ila kwa utakacho wewe ni ushahidi ulio hai(Wakuona, wakugusa na kushikika) kitu ambacho ni kigumu.

Waliokapatiwa bahati za kuonesha haya tayari walishapita (Wajumbe wa MUNGU) ambao ndo walikuwa na access uzitakazo, mim n mtu wa kawaida sana kama ulivyo wewe ila tofauti zetu ni IMANI.

Kwa ulimwengu wa leo na toka enzi imani ni kuamini ama kwa kuona, kusoma au kusikia ila kwenye evidence kuna masalia ya mifano yake kama uwepo wa FARAO, Mke wa Nuhu aliyegeuka jiwe la chumvi, Qur'an, Torat, Zaburi, Injil na vitabu vingine.

Ila ukitaka USHAHIDI UUTAKAO, kwakweli mimi ntashindwa kukupa, coz MUNGU hakunipa hyo ACCESS.
Je makosa ya kisayansi yaliyoandikwa kwenye quran unayachukuliaje?

Mungu hajakupa access ya kuyaona!?
 
Hapo huoni kuna tatizo mkuu yani Mungu alilidhihirisha kwa kikundi Cha watu fulani tu ndani ya muda fulani hadi kwa mtume wake wa mwisho (Muhammad) halafu hajaonekana tena. Aliacha maandiko ambayo tafsiri zake zinachanganya watu. Na pia alitoa maagizo tofauti kwa watu mbalimbali kitu ambacho kimepelekea dini tofauti bila kujua ipi ni sahihi. Lakini mwisho wa siku ataadhibu watu kwa kutofata maandiko, dini sahihi na kutilia mashaka uwepo wake hii ni haki kweli ?

Kama yupo ni swala dogo tu la kujidhihirisha kwa wasioamini na waliopotea kwenye dini ya kweli na kusema dini sahihi ni ipi lakini yuko kimya. Mfano kwenye biblia aliwaaminisha manabii wa "baali" kuwa yeye ni mungu wa kweli kwa kushusha moto, kuna vilema waliponywa na yesu. Hizi ishara kwanini hatuzioni sasa?

Waandishi wa vitabu vilivyopo ambavyo unasema ndio ushahidi ni wanadamu kama sisi, tunajuaje walikuwa wanaongea na mungu kweli? lakini pia tunajuaje walikuwa hawaongei na Mungu? swali la pili rahisi sana wanadai kuongea na kiumbe kinachojua kila kitu lakini maandiko yao yamejaa makosa hii ni wazi hawaongei na kiumbe cha hivyo ni wao wenyewe na wanaandika makosa kama wanadamu wengine tu.

Uwepo wa masalia ya miili ya wafalme wa misri (ma Farao) ni ushahidi tu kwamba watu wa misri walikuwa na njia za kutunza miili ya watu kwa muda mrefu bila kuoza (inaitwa mummification) na sio ushahidi wa kutosha wa matukio yaliyoandikwa kuhusu misri kuitumikisha israeli. waandishi wa vitabu vya dini fulani walijua hii njia ya kutunza miili ya wafalme wa misri wakadai Farao (kwanza walihisi Farao ni jina la mtu na ni mmoja) hakuoza kwasababu mungu alitaka kumuadhibu kitu ambacho ni hadithi tu, vipi sasa miili mingine ambayo sio wa Farao iliyotunzwa kama wa Farao na masalia yapo wao pia walimuudhi Mungu?

MAANDIKO SIO USHAHIDI. KILICHOFANYIKA NI KUCHOMEKA CHEMBE CHEMBE KIDOGO ZA UKWELI KWENYE HADITHI ZA KUFIKIRIKA. NDO MAANA MIUJIZA ILIYOANDIKWA KAMA WATU KUFUFUKA, VILEMA KUTEMBEA KWA KUOMBEWA HATUIONI SABABU NI VITU VISIVYOKUWEPO KWENYE UHALISIA.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app

Maandiko ni hadithi za uongo tu. Zisizo na uhalisia.

"Right kama sio utandawazi, waisrael wangetunga Exodus part 2 juu ya Holocaust kumtoroka farao wa kijerumani."
 
Umeandika mengi kuonyesha Kwamba Qur'an imekosea, kwa bahati mbaya badala ya ku disprove Qur'an umedhihirisha tu ujinga juu ya Qur'an (means huijui ila umekariri articles ukaona ndiyo ushajua Qur'an tayari)

Kwa mfano hapo juu unadai kwamba Qur'an inasema "Earth has been spread out like a carpet"

Ipo hivi, Kiswahili ni lugha ambayo imechukua baadhi ya maneno ya kiarabu, na miongoni mwa maneno hayo ni neno "Ardhi"

Sasa, kwenye hiyo Aya limetumika neno la kiarabu ARDHI" Kwamba ardhi imetandazwa kama carpet...

Sasa nikuulize, ardhi haijatandazwa kama carpet?!,

Kwenye English sometimes Ardhi inakua referred as to Earth (Dunia), na hiyo ndiyo iliyokupeleka chaka.... Lakini kwenye kiarabu "DUNIA" na "ARDHI" ni vitu viwili tofauti kama ilivyo kwenye kiswahili...

NB: Sidhani kama ikiwa kitabu ni cha uongo, itabidi utunge tena uongo dhidi yake,... Bali utatumia uongo ambao tayari umeugundua ku disprove kitabu hicho, so mpaka hapo usha prove failure
Vipi kuhusu milima kutengeneza stability dunia isiyumbishwe?

Vipi kuhusu nyota kuwa ni mapambo?
 
Siyo kwamba mtu anayeamini kwa hofu ya kutishwa na jambo ndiye mtu hatari zaidi katika uso wa dunia hii ukilinganisha na mtu aliye mwema na anafanya yaliyo mema pasipo kuwekewa vitisho?

Viongozi Wangapi wanaamini Mungu na wanahudhuria msikitini na makanisani lakini ni mafisadi na wanatenda yasiyo mazuri!?

Main issue is to respect humanity.

Watu hawaamini kwasababu Mungu hayupo tu, wala siyo issue ya maadili!!

Hata kama nkikubali idea yako ya kwamba watu wawe na hofu ya Mungu ili wawe wema

Swali linabaki habari ya Mungu ni kweli au si kweli!?
Habari ya Mungu ni kweli na ushahidi upo..

Kwa sisi waislam, Qur an imeeleza vitu vingi ambavyo tunajionea wenyewe sasa hivi na wanasayansi wanazidi kugundua vitu ambavyo Qur'an ilishavielezea miaka 1400+ iliyopita.

Hata mimi nishawahi kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Mungu na juu ya imani yangu. Ila baada ya kusoma Qur'an na kuifuatilia pamoja na kufuatilia vitu vilivyogunduliwa na wanasayansi basi shaka yangu yote iliondoka
 
Habari ya Mungu ni kweli na ushahidi upo..

Kwa sisi waislam, Qur an imeeleza vitu vingi ambavyo tunajionea wenyewe sasa hivi na wanasayansi wanazidi kugundua vitu ambavyo Qur'an ilishavielezea miaka 1400+ iliyopita.

Hata mimi nishawahi kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Mungu na juu ya imani yangu. Ila baada ya kusoma Qur'an na kuifuatilia pamoja na kufuatilia vitu vilivyogunduliwa na wanasayansi basi shaka yangu yote iliondoka
Vitabu vya dini havithibitishi hata kwa 1% uwepo wa Mungu.
 
Umesoma Qur'an au unaleta ujuaji?
Sijasoma! Ila najua haiwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu. Kama unalielewa neno "thibitisha" utajua namaanisha nini.

Hakuna ushahidi wa kuweza kuthibitisha uwepo wa Mungu. Hata mimi siwezi kuthibitisha kama kweli Mungu hayupo. Tofauti ni kwamba wewe unaishi kwa imani wakati mimi nimekosa imani kwa mambo ambayo hayana ushahidi.

Kabla ya kuuliza kama naleta ujuaji inabidi uwe open-minded kujadili mada kama hizi. Kila mtu ana mtazamo wake linapokuja suala la uwezekano wa kuwepo na Mungu.
 
Hofu ya matokeo fulani ukifanya vitendo vya hovyo lazima iwepo Ili kutunza amani. Ndio maana tuna sheria za nchi.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
Kwahy unaamini bila ya sheria za nchi hakuna amani??

Na vip kabla ya mambo ya nchi hapo kale watu hawakuwa na amani ?? Je, ilisababishwa na hofu ya nani??
 
Back
Top Bottom