Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kutongoza si tusi...Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
Huyo Mbunge aliyesema ni tusi bila shaka ni wa bara na hafahamu Kiswahili fasaha wala fasihi ya Kiswahili.
Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
Msingi wa neno hilo si tusi
Lakini kwa taratibu na adabu za Kiswahili, sio kila neno ambalo si tusi basi linatumika katika mazingira yeyote tu
Chukulia kwa mfano, jee unaweza kulitumia kuhusisha baba/mama yako?
"Baba yetu ni hodari wa kutongoza wanawe" au "ni rahisi kwangu kumtongoza mama"
Ndo kuna ile methali ya "Msimulia mvua ilimnyea". Japo watu wengi kwenye hilo neno la mwisho wanaweka neno "ilimnyeshea".Ukija Mvita waeza kuambiwa "mvua inakunya", wabara waona tusi.
Vivyo vivyo "kutongoza".
Waeza kuambiwa "nitongozee muuza duka anipe mkopo", kwa maana ya "nishawishie kwa bashasha muuza duka anipe mkopo".
Kiswahili kipana.
Ndo kuna ile methali ya "Msimulia mvua ilimnyea". Japo watu wengi kwenye hilo neno la mwisho wanaweka neno "ilimnyeshea".
Basi mtu anaweza akasema mvua imeninyenyekea. Na mwingine aweza kusema naenda msalani kunyenyekea.Kwa sie tunaoangalia "etymology" ya neno, mzizi wa neno, mzizi wa kunyeshea na kunyea ni "nye", ni muendelezo tofauti wa neno lile lile.
Ukienda chooni next time, in high society, ku obscure maana, unaweza kusema "naenda kunyeshea" lol.