Kutongoza ni tusi au?

Kutongoza ni tusi au?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
 
Jacobus

Kutongoza siyo Tusi. Ni neno la Kiswahili Fasaha kabisa linaloongelea hali ya Mtu kumshawishi mtu/watu wengine juu ya kufanya/kukubaliana juu ya suala fuilani.

Tongoza = Seduce

Seduce = 1 shawishi; potoa. 2 tongoza
 
Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
Kutongoza si tusi...
Ila unatakiwa uwe makini wapi unalitumia; huwezi litumia kwa nduguzo wakaribu ukaeleweka kwa jamii kuwa ulikuwa na maana ya kushawishi.
Mfano: Nimemtongoza dada/mama anipe kitu fulani...
 
Kutongoza siyo tusi. Ni kiswahili sanifu cha zamani sawa na shawishi
 
Aksanteni sana wanajamvi sasa mheshimiwa Tundu Lisu kalitumia neno hili bungeni juzijuzi tu na kushutumiwa na hasahasa mheshimiwa Ole Sendeka, je inakaaje hii?
 
hakuna tusi hapo ni watu kushindwa kuelewa fasihi.
 
Ukija Mvita waeza kuambiwa "mvua inakunya", wabara waona tusi.

Vivyo vivyo "kutongoza".

Waeza kuambiwa "nitongozee muuza duka anipe mkopo", kwa maana ya "nishawishie kwa bashasha muuza duka anipe mkopo".

Kiswahili kipana.
 
Huyo Mbunge aliyesema ni tusi bila shaka ni wa bara na hafahamu Kiswahili fasaha wala fasihi ya Kiswahili.
 
Huyo Mbunge aliyesema ni tusi bila shaka ni wa bara na hafahamu Kiswahili fasaha wala fasihi ya Kiswahili.

Tena aliyesema kuwa neno KUTONGOZA sio mahali pake kutumiwa bungeni ni OLE MADEYE...na alijitapa kuwa ni Mwalimu wa Kiswahili....it was a shame na kichwa chake nadhani kilijaa mawazo ya ngono tuu....over!!
 
Msingi wa neno hilo si tusi

Lakini kwa taratibu na adabu za Kiswahili, sio kila neno ambalo si tusi basi linatumika katika mazingira yeyote tu

Chukulia kwa mfano, jee unaweza kulitumia kuhusisha baba/mama yako?

"Baba yetu ni hodari wa kutongoza wanawe" au "ni rahisi kwangu kumtongoza mama"
 
Jacobus wabunge wa CCM ni mafisadi viwembe, wasikutishe wala usiwashangae
Juzi katika bunge letu mheshimiwa Tundu lisu alitumia neno 'kutongoza wapiga kura', sasa baadhi ya wabunge wa CCM wakamshutumu kwa kutumia neno hilo.
Nawaomba wajuzi wa kiswahili kuliweka neno hili sawa kwa wanaJF.
 
Last edited by a moderator:
Msingi wa neno hilo si tusi

Lakini kwa taratibu na adabu za Kiswahili, sio kila neno ambalo si tusi basi linatumika katika mazingira yeyote tu

Chukulia kwa mfano, jee unaweza kulitumia kuhusisha baba/mama yako?

"Baba yetu ni hodari wa kutongoza wanawe" au "ni rahisi kwangu kumtongoza mama"

Katika kuzungumza ama kuandika lugha huwa kuna:

- Matumizi ya maneno ipasavyo (appropriate wording), ndiyo maana huwezi kusema kumtongoza mwana

- Matumizi ya maneno ili jambo lieleweke zaidi (clear wording)

Kwa hiyo, nadhani wabunge wana ufinyu wa kuelewa lugha.
 
Kutongoza sio tusi ni kiswahili fasaha kabisa cha kumaanisha kumshawishi mtu akubaliane na wewe au kumbembeleza.sema kwa sababu halitumiwi mara kwa mara katika jamii yetu mpaka pale inapohusu mwanaume kumtaka mwanamke ndo maana imechukuliwa kama tusi.
 
Ukija Mvita waeza kuambiwa "mvua inakunya", wabara waona tusi.

Vivyo vivyo "kutongoza".

Waeza kuambiwa "nitongozee muuza duka anipe mkopo", kwa maana ya "nishawishie kwa bashasha muuza duka anipe mkopo".

Kiswahili kipana.
Ndo kuna ile methali ya "Msimulia mvua ilimnyea". Japo watu wengi kwenye hilo neno la mwisho wanaweka neno "ilimnyeshea".
 
Ndo kuna ile methali ya "Msimulia mvua ilimnyea". Japo watu wengi kwenye hilo neno la mwisho wanaweka neno "ilimnyeshea".

Kwa sie tunaoangalia "etymology" ya neno, mzizi wa neno, mzizi wa kunyeshea na kunyea ni "nye", ni muendelezo tofauti wa neno lile lile.

Ukienda chooni next time, in high society, ku obscure maana, unaweza kusema "naenda kunyeshea" lol.
 
Basi mtu anaweza akasema mvua imeninyenyekea. Na mwingine aweza kusema naenda msalani kunyenyekea.
 
Back
Top Bottom