LGE2024 Kutopiga kura ni dhambi mbele za Mungu, dhambi ya kutotimiza wajibu!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
346
Reaction score
522
Kupiga kura ni njia muhimu ya kutimiza wajibu wa kijamii na kisiasa.

Ni fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi yanayoathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla.

Kutoshiriki inaweza kupelekea kukosa sauti katika mambo yanayohusiana na maisha yetu.
katika mitazamo mingi ya kidini, mamlaka zote zinachukuliwa kama zikitoka kwa Mungu.

inasisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka na kutimiza wajibu wetu kama raia.

Heshima hii inajumuisha kupiga kura na kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.

Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuchangia katika ujenzi wa jamii bora.

Kila la heri kwenye mchakato huu muhimu sana kwa taifa letu 🙏
 
Kupiga kura ni njia muhimu ya kutimiza wajibu wa kijamii na kisiasa.
Ni fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi yanayoathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla.
Kutoshiriki inaweza kupelekea kukosa sauti katika mambo yanayohusiana na maisha yetu.
katika mitazamo mingi ya kidini, mamlaka zote zinachukuliwa kama zikitoka kwa Mungu.
inasisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka na kutimiza wajibu wetu kama raia.
Heshima hii inajumuisha kupiga kura na kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuchangia katika ujenzi wa jamii bora….

Dhambi yangu wanaichukua wanaoiba kura.
 
Kwa uongozi huu mbovu wa kijinga siwezi kupiga kura bora nifanye yangu, tunasukumana kwenye foleni kuchagua watu wanaojali matumbo yao tu,hapana kwa sasa mtu hapati kura yangu
 
Tusilazimishane bhana siendi na haitatokea labda Mambo yabadilike
 
Hahaha kwani Mamlaka za uteuzi zimeshindwa?

Rais Magufuli aliweza kuteuwa wenyeviti wa vitongoji nchi nzima 2019, kumetokea nini kwa Rais Samia kufanya/Kuendeleza waliyoyaanzisha yeye na Mtangulizi wake?

Mnatuhamasisha kujiandikisha, hatutaki na mnapotulazimisha saana tunajiandikisha, sasa itakuwaje siku ya kupiga kura, mtatufuata majumbani?
 
Nina passport,tin number, Brela name, health insurance,
Siwezi kuwa na vitambulisho kama cha vote id vinavyo halalisha wizi wa ccm , ..

Mimi sio mjinga .

Katiba ifanyowe reviews Kwanzaa.
 
Kupiga kura ni njia muhimu ya kutimiza wajibu wa kijamii na kisiasa.
Ni fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi yanayoathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla.
Kutoshiriki inaweza kupelekea kukosa sauti katika mambo yanayohusiana na maisha yetu.
katika mitazamo mingi ya kidini, mamlaka zote zinachukuliwa kama zikitoka kwa Mungu.
inasisitiza umuhimu wa kuheshimu mamlaka na kutimiza wajibu wetu kama raia.
Heshima hii inajumuisha kupiga kura na kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuchangia katika ujenzi wa jamii bora….
Kila la heri kwenye mchakato huu muhimu sana kwa taifa letu 🙏
Kumbuka pia kuwa sio kila mamlaka imewekwa na Mungu.
Ukiona mamlaka imeingia madarakani kwa Rushwa, ulaghai nk haitokqni na Mungu.
 
Mkapige kura mkafanye representative democracy kwa sie ambao tutakua na mamb mengne
 
Dhambi kubwa zaidi ni kuchagua wanasiasa of whom 90% ni majizi ambao wakishapata dhamana wanageuka fimbo ya kuchapia waliowapa nafasi hiyo
 
Kupiga kura ni haki ya kila raia wa Tanzania ndio lakin hai iyo haiondoi haki ya mtu kuamua kutokupiga kura kwasababu anazoziona yeye , mimi binafsi Nina walakini na mamlaka zinazosimamia uchaguzi hazitendei haki maamuzi ya umma Bali zinalinda maslai ya waajii wao. Nitapiga pindi mfumo wa upigaji kura utakapobadilika na kuwa wa kidigitari
 
Unampigia mwanasiasa kura,anaenda kucheka unapotekwa.anasema ni drama
Patamu hapo
 
Back
Top Bottom