Kutoroka kwa Wafungwa, mapya yaibuka

Kutoroka kwa Wafungwa, mapya yaibuka

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
UPDATE:

August 22, 2024

KUTOROKA KWA WAFUNGWA: SHAHIDI ADAI WALITOKEA MLANGO MKUU KWA KUTEMBEA

Taarifa mpya zinaeleza Wafungwa 13 walitembea na kutoka kupitia mlango mkuu wa kituo cha Polisi wakiwa chini ya uangalizi wa maafisa wawili wa polisi waliokuwa zamu usiku

Idadi ya Wafungwa ni 13, wakiwemo Raia 12 wa Eritrea. Shuhuda ameshuhudia kumuona Mmoja wa Polisi aliyekuwa zamu kupokea fedha kutoka kwa Mmoja wa Waeritrea

Alithibitisha kuwa Polisi wa zamu alihesabu wafungwa wote dakika chache baada ya saa Sita usiku ambapo baada ya hesabu aliondoka bila kufunga Milango ya Mahabusu

Citizen TV imeripoti kwamba maafisa wawili waliokuwa zamu, mlinzi wa seli na afisa wa zamu, wanachunguzwa kwa tuhuma za kusaidia kutoroka kwa watuhumiwa hao.

Mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa kwa makosa ya udanganyifu na kuwekwa katika Mahabusu za kituo hicho usiku huo wa tukio, aliwaambia wachunguzi kwamba watuhumiwa hawakutoroka kwa kukata waya wa chuma kama ilivyokuwa imedhaniwa awali

Amesema Baada ya kupewa pesa na Waeritrea, maafisa hao walisema wanakwenda kantini.
Kwa kuwa maafisa hao wawili waliondoka, watuhumiwa 13 walipata fursa ya kutembea kuelekea uhuru kupitia dawati la ripoti na kutoweka gizani

Majira ya Saa 12 asubuhi mtu anayehusika na kuwahudumia Wafungwa, aliripoti kutokuwepo kwa baaadhi yao. Hadi sasa hakuna Mfungwa aliyepatikana huku msako mkali ukiendelea

............................

UPDATE: POLISI 8 WAKAMATWA, MAMLAKA YASEMA ILIKUWA KAZI YA NDANI

Maafisa 8 wa Polisi Wamesimamishwa Kazi baada ya Wafungwa 13 akiwemo Mshukiwa wa Mauaji ya Kware, Collins Jumaisi, Kutoroka katika Kituo cha Polisi cha Gigiri, asubuhi ya Agosti 20, 2024

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli alielezea tukio hilo kama "Kazi ya Ndani" ambapo amesema Kamanda wa Kaunti Ndogo ya Gigiri, Afisa Mkuu wa Kituo (OCS) na Maafisa waliokuwa zamu ni miongoni mwa wale waliosimamishwa na wako chini ya ulinzi wa polisi

Masengeli amesema msako unaendelea na anamini wote waliotoroka watakamatwa

...............................................

Kamanda wa Kaunti ya Nairobi, Adamson Bunge amesema Wafungwa 13, akiwemo Mshukiwa wa Mauaji ya Kware, Collins Jumaisi, wametoroka katika Kituo cha Polisi cha Gigiri

Ingawa Collins alikataa kuhusika na Mauaji ya Kware akidai kuteswa ili akubali, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilikanusha madai ya mateso na kuomba muda zaidi ili kuwatafuta Mashahidi na familia za waathirika

Tokea sakata la Miili kuokotwa Kware, kumekuwa na maoni Mtandaoni kuwa Miili hiyo ni ya Wasndamanaji waliouawa na Polisi katika Maandamano ya Reject Finance Bill, na Collins anatumika kufunika Ukatili wa Polisi

Source: Nation.Africa
 
Kenya wako vizuri.
Hivi wale wanawake wa rombo walioenda kuzaa na wanaume wa kenya, wale watoto wako wapi?
 
Collins Jumaisi, ambaye ni mshukiwa wa mauaji ya Kware, ameripotiwa kutoroka kutoka Kituo cha Polisi cha Gigiri akiwa pamoja na washukiwa wengine 12 mnamo Agosti 20, 2024. Collins Jumaisi alikuwa anahusishwa na kesi ya mauaji ya watu kadhaa katika eneo la Kware, ambapo miili yao ilipatikana. Tukio hili la kutoroka kwa wafungwa limezua maswali kuhusu usalama wa vituo vya polisi na uadilifu wa uchunguzi unaofanywa kuhusiana na mauaji hayo.

Tukio hili limeongeza hofu miongoni mwa wananchi, na serikali inatarajiwa kutoa taarifa zaidi kuhusu hatua zitakazochukuliwa ili kuwakamata tena wafungwa hao na kuhakikisha usalama wa jamii.
unnamed.png
reakNews
 
View attachment 3074851reakNews
Huyu jamaa anaoneshq ni jambazi sugu
 
Nimeona hii taarifa Citizen Tv / Al jazeera news na hadi sasa maafisa 8 wa Polisi wamesimamishwa Kazi

Chonde chonde IGP mipakani Ulinzi uimarishwe huyo Jambazi ni Muuwaji hatari sana
 
Nilinusa harufu ya samaki zamani....
Waache kuhadaa wananchi
 
Nimeona hii taarifa Citizen Tv / Al jazeera news na hadi sasa maafisa 8 wa Polisi wamesimamishwa Kazi

Chonde chonde IGP mipakani Ulinzi uimarishwe huyo Jambazi ni Muuwaji hatari sana
Maigizo, Polisi wa Kenya wamemtorosha Collins Jomaisi, baada ya uongo wao kufichuka.... Waliouwawa ni waandamanaji...
 
Back
Top Bottom