Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Toka siku niliposikia kuwa WIZARA ya Fedha ingetoaa ufafanuzi kuhusu tozo ya miamala ya simu na benki, nimekuwa nikiota ndoto.
Kuna ndoto na kuna ndoto. Kuna ndoto za usiku na kuna ndoto za mchana.
Ndoto za usiku ama ni za kuleta tumaini au kutia hofu na ingawa kwa muda huweza kuleta tumaini, hazitekelezeki!
Kuna ndoto unaaamka kwa hofu na inakuchukua muda kuamini ni ndoto tu na kushukuru kwa kutokuwa kweli.
Kuna ndoto unaamka kwa furaha na inakuchukua muda kuamini ni ndoto tu na kulaani kwa nini haikuwa kweli.
Binadamu tumejaaliwa akili zinazotuwezesha kupanga namna ya kuendesha maisha yetu hapa duniani.
Mipango kama hii ni ndoto pia lakini ni ndoto za mchana na tofauti na za usiku uwezo wa kuzitekeleza tunao.
Tumaini langu hadi jana lilikuwa ni kujiuzulu kwa Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu Nchemba PhD kwa tuhuma zilizomkabili.
Tuhuma za kusimamia, kwa niaba ya dola, zoezi la kutuibia sisi walipa kodi wa taifa hili kupitia kinachoitwa tozo!
Pamoja na leo kuamka kwa furaha kubwa, imenichukua toka asubuhi kuamini kuwa tumaini langu hilo halikutimia.
Ngoja niendelee kulaani tu kwa nini halikutimia...