Inabidi uelewe hivi vitu kabla haujaendelea na hoja yako
1)Library kuu inayotumika kwenue AI na ML ni Tensorflow ambayo imeandikwa "PRIMARILY" katika C/C++ hizo Tensoflow za Python, Java, javascirpt etc ni "WRAPPERS" tu. Hivyo ili kupata real flavor ya Tensorflo inabidi utumie C/C++ (Few geeks experience this flavor BTW)
2)C/C++ ndio language ambayo wataalam wanarecomend itumike kwenye ML na AI kwa sababu operations zake ni "resource - Intensive", kwa kutumia low level languages kama C/C++ inasaidia kuongeza speed ya hizo operations. Python inakua slow sana na ndio maana kuna "Cython" inayosaidia kuongeza speed kdg kwenye scripts za python
3)Python mwanzo kabisa ilikua na lengo la kuwa scripting language ya systems zinazotumia C/C++ ili kurahisisha vitu kama text processing, I/O, etc.. ambavyo havikua na ulazima wa kuanza kutumia C/C++ tena coz kiukweli C/C++ ni ngumu ukilinganisha na python. Hivyo python ilipozidi kupata user base kubwa ndipo developers wakazidi kuitumia kutengeneza wrappers za mambo ambayo yanafanyika vigumu sana kwa c/c++ ila ukitumia python yanafanyika kwa urahisi zaidi. Ndo maana utaona kuna libs kama numpy, keras etc ambazo zinasaidia sana kwenye ML dev, japo ukiingia kiundani zaidi 'original' Tensorflow iloandikwa kwa c/c++ inaweza kufanya vitu vyote peke yake kwenye ML & AI dev kuanzia kutengeneza model, kutengeneza data pipeline(kwa python wengi hutumia pandas, lkn TF inajiweza sana kwa hili na inaifanya vzr zaidi ya pandas), kufeed data kwenye model, kutengeneza loss fn etc.....(Read Tensoflow documentation for more)
So kama umenielewa hapo juu C/C++ is the best for AI & ML development lakini python inatumika kwa sababu ya urahisi wake kwenye scripting na ndio maana ina wrappers nyingi za mambo ambayo unaweza fanya hata kwa C/C++(but with more sweat). Na Tensoflow og ya C/C++ inaweza kufanya kila kitu sema tu inabidi uwe umesoma documentation kwelikweli la sivyo utakuwa unakutana na errors ambazo hazijawekewa solution kwenye dev communities. Wengi wanatumia Tensorflow ya Python ambayo ni wrapper tu lakini ina community support kubwa, hivyo hata ukikumbana na error unajua wapi pa kupatia solution.
Kama unataka kuwa geek wa ML & AI endelea na C/C++ then R then Python, lakini kama unataka tu kuwa dev wa kawaida kwenye ML & AI kama walivyo wengi endelea na Python achana na C/C++ itakupotezea time bure. Kwa maoni yangu syllabus kama inatumia C++ basi naiunga mkono.
~Kali Linux