Kuua ni laana hata vitabu vya vidini vimesema hivyo, usikubali kubebeshwa dhambi hiyo

Kuua ni laana hata vitabu vya vidini vimesema hivyo, usikubali kubebeshwa dhambi hiyo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nafahamu kuna Watu hawajui Jambo hili. Nimeandika ili wajue. Hata hivyo hata kama hawajui lakini wakafanya mauaji haitaondoa Laana Kwa namna yoyote.

Elewa kuna Makosa àmbayo kamwe Mungu hawezi kukusamehe hata ungetubu kwa namna gàni.

Sheria za Mungu zîpo wazi, HAKI. Ukiua lazima nawe uuawe. Hakuna Kosa baya kama KUUA MTU, kumwaga damu ya Mtu.

Hapa nazungumzia KUUA MTU asiye na HATIA. Mtu hajakukosea kitu wewe unamuua. Hiyo Laana yake siô lelemama.

Matajiri wakubwa na weñye akili husafisha Mikono yao kwa kutumia Watu Wengine.

Hawawezi kuua Mtu kwa Mikono Yao wènyewe Kwa sababu wanajua kuua MTU NI Laana kûbwa na kosa ambalo halisameheki.

Hivyo hutumia Mikono ya Watu Wengine kuua mahasimu wao huku Mikono yao ikibaki kuwa Safi pasipo kumwaga damu za watu. Hasa wale ambao hawana HATIA.

Kitendo cha Mtu kumtumia Mtu Mwingine Kuua huitwa kusafisha Mikono yake isichafuliwe na damu ya Mtu.

Vijana najua mnaweza kuvuta Bange zenu, madawa ya kulevya, vilevi au Aina yoyote ya vitu vinavyosisimua ili kuondoa Ûtu wenu. Na kujikuta mnakuwa na Àkili za kinyama na kikatili.

Huyo anayekutuma kuua yeye Wala haitahesabika kiroho kuwa aliua, wewe uliyetumia Mikono yako KUUA ndîo utakuwa upo kwèñye database ya wauaji na wéwe ndîo utakayepata Làana huku mwenzako aliyekutuma akiendelea kuneemeka yeye na familia na kizazi chake.

Aliyekutuma ataomba Msamaha tuu na atasamehewa Kwa sababu kosa lake siô Kuua Bali kukutuma.

Làana ya Kuua hukuandama wewe na kizazi chako huku Yule aliyekutuma akiwa nje ya mfumo wa Laana.

Watu wengi hujiuliza mbona watawala na matajiri wengi licha ya kuhusishwa na mauaji lakini waô hawapati madhara na wanazidi kuneemeka kizazi hata kizazi.

Basi jibu la swali hilo NI kuwa watawala na matajiri weñye Akili wanapokabiliana na mahasimu wao ikafikia hatua wakaona Hapa Suluhu na kumwua Mtu na Mtu huyo Hana Kosa lipasalo kuuawa. Basi hutumia Mbinu ya kusafisha Mikono Yao Kwa kuwabebesha Wengine Làana ya Mauaji Kwa kuwatuma kufanya Mauaji.

Watawala na matajiri hutuma vibaraka waô, waliochini Yao àmbao wanawajua Kabisa Fulani NI muovu, na yupo Radhi kuuza Roho yake au kufanya chochote kwaajili ya Pesa. Basi Watu hao ndîo hutumwa kwaajili ya kufanya Mauaji na kujibebea Làana ya kumwaga damu ya Mtu asiye na HATIA.

Watawala na matajiri hawawezi kukutama kufanya Mauaji kama wewe sio MUUAJI. Wanajua Watu waliochini Yao fika kuwa Fulani NI mwema hawezi kukubali kufanya hili dili. Na yupo tayari hata kupoteza Kazi lakini siô kukubali Amri Yao.
Lakini wanajua pia waovu àmbao huwatumia Kwa shughuli za kiovu.

Mwisho wa Siku, Yule aliyetumwa endapo akimwendea mtawala au tajiri aliyemtuma kufanya Mauaji akataka kumlaumu. Tajiri au mtawala atasema nilikulipa Kwa Kazi hiyo. Tenà nilikuuliza utahitaji kiasi gani.
Na ukapokea. Sikukulazimisha kwenda.
Alafu mbona Fulani alikataa na sikumfanya chochote na hajaenda? Wewe tamaa yako ndîo iliyokupeleka Kuua na wala siô Mimi. Usinisingizie.

Kijana, elewa hakuna Mtu yeyote, WA cheo chochote, WA hadhi yoyote Hapa Duniani àmbaye anayomamlaka ya kukulazimisha kutenda uovu. Unatenda uovu Kwa hiyari yako mwenyewe.
Bila kujali unafanya Kazi gani, íwe ni Polisi, Askari, mwanajeshi, mwanausalama, Mwalimu, hakimu, Jaji, Tabibu n.k. Amri yoyote inayokutaka ufanye uovu au uhalifu ni Amri batili na wéwe ndiye utakayewajibika kimwili na kiroho.

Usikubali Mtu akakuchezea shere akawa mwerevu kukushinda. Ati yeye hataki Kuua ila anataka kukutumia wewe. Làana unaibeba wewe.

Kama unaakili, mlete huyo anayetaka Kuuawa, mwambie amuue yeye mwenyewe.

Hata hivyo kûna wale Wauaji, Killers werevu yàani Professional Killers àmbao kama akibaini aliyetumwa kumwua Hana hatia Basi hujifanya amemuua mhusika na kwenda kumtupa Porini huku akimwacha akiwa HaI mtu Yule.

Kama atakufa hiyo NI juu yake na yeye hakumwua. Mbinu hiyo hutumiwa na professional Killers.

Mbinu hii pia ilitumika na Waisrael walipotaka kumwua ndugu Yao Yusufu, katika mjadala wakasema huyu ni ndugu yetu, na Makosa Hana.

Tumtupe kwèñye shimo ili damu yake ísiwe juu ya Mikono yetu. Hao ni waovu weñye Akili wanaojua kuwa KUUA MTU asiye na HATIA NI dhambi mbaya kuliko zote.

Soma
Kumbukumbu la Torati 27:25
[25]Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.
Cursed be he that taketh reward to slay an innocent person. And all the people shall say, Amen.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Kuna makabila ukijichanganya ukaua mtu wao aisee utapata tabu Sana.

Huku kwetu kuna kijana aliuaua Kisha wenye kijana wakafanya yao.
Unaambiwa huyo kijana alienda na wauaji Jino kwa jino wakadondoka mmoja mmoja mpaka wakaisha
 
Back
Top Bottom